Kweli kabisa hutwo tubilioni tuwili ni tuela twa mboga tu! (joke).Haya mambo NMB ni kawaida ina wafanyakazi wezi wezi wanaajiriana kwa madili.. siwezi kuweka pesa yangu NMB hata juzi nimetoka kuweka mil 700 Exim bank coz nawaamini, hata balays toka mwaka juzi wamanitunzia bil 2 kiuaminifu kabisa. Bil 2 ni fedha ndogo ndio maana nimeitunza tu
Huna unachokijua khusu ATM CARD.....tulia hivyohivyooooHuwa hawafanyi hivyo.
Wanajifanya mteja mwenye account alikuja kuomba atm card mpya. Wanamjazisha fomu kisha wanatengeneza card mpya . Kisha anajifanya tena mteja alikuja kufata card yake na amemkabidhi hiyo card mpya.
Kumbe card hiyo anayo yeye mwenyewe mfanyakazi wa bank
Hapo ndipo anaanza ku draw pole pole via ATM kwa kutumia hiyo card yenye jina la mteja mwenye account
Muamala wa benki lazima uache nyayo. Pesa ikitoka lazima ionekane imetolewa kwa mtindo gani.Hivi inawezekana wakaiba kwny acc yako alafu ule muamala usionekane kwny bank statement yako?? Tuseme tukio lilitokea 2021...
James alienda kesho...[emoji848][emoji3][emoji1]Hivi hiki kiswahili kiko sahihi? [emoji848]
Ungeomba statement ya bankNi kweli. Kuna kesi nyingi za warithi kudhulumiwa na kudanganywa kuhusu kiasi cha fedha kilichokuwa kwenye account ya marehemu.
Binafsi mzee wangu alikuwa anafanya shughuli zake na alikuwa anaweka fedha benki pia Alikuwa mstaafu so alikuwa analipwa Pension yake via NMB. Mwaka ambao mzee alifariki, alivuna mpunga na akauza gunia zaidi ya 500 ambazo alipeleka benki. Baada ya kufariki na tulikaa muda mrefu kupata utaratibu wa mirathi kwenda benki tunaambiwa mzee alikuwa na laki saba tu benki.
Unaenda kula nazo burger halafu unajionaa mjanja na kuwaringishia waswahili wenzako huko Mwalusembe nimekula burgerMi nakusanya data kuna kahela ka mboga nakachungulia tu wanavyokapitia.
Tutaonana huko mbele
Nimecheka balaaa hadi machozi yamenitoka. Nigga ni mtu moja hovyo sana mchafu siyo honest. Bure kabisa.Japokuwa me ni member wa hizi harakati
Black panther
Civil rights movement
Back to africa movement
Lakini linapokuja swala la kumuamini mtu mweusi najivua hayo magamba kwa muda.
Umetaja mfano mzuri sana 🤣James alienda kesho...[emoji848][emoji3][emoji1]
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 dahnwe acha , mimi mwenyewe nitawawashia moto soonMi nakusanya data kuna kahela ka mboga nakachungulia tu wanavyokapitia.
Tutaonana huko mbele
Miaka minne niliacha million 3 kcb ,ATM card ilivunjika nikakosa muda wa kuingia counter ,gafla scholarship hii hapa,nikaeda masomoni nimerudi nikaenda counter mzigo umeongezeka Laki kadhaa ,imefanya niipende hii bankMfanyabiashara maarufu katika mikoa ya Arusha, Dar na Dodoma Joseph Kalugendo mkazi wa Moshoni jijini Arusha, ameibiwa fedha zake zaidi ya milioni 100 katika benki ya NMB tawi la Clock Tower Arusha na mtumishi wa benki hiyo.
Taarifa ambazo zimethibitishwa na Mfanyabiashara huyo amedai kuwa siku za usoni alienda katika benki hiyo kwa ajili ya kuchukua fedha ndipo alipopigwa na butwaa kukuta kitita hicho hakipo.
Meneja wa benki hiyo Kanda ya Kaskazini Praygod Mphuru alipohojiwa alikiri kuwepo kwa tukio hilo akidai tayari wamemsimamisha kazi mfanyakazi wao Samweli na kwamba suala hilo linafanyiwa kazi na kuomba suala hilo lisitangazwe.
Pia vigogo wa benki hiyo kwa sasa wanahaha kutafuta mchawi aliyetoa taarifa hizo kwa waandishi wa habari na tayari baadhi ya wafanyakazi wameitwa na kuhojiwa juu ya taarifa hizo za ndani kufika kwa wanahabari
Joseph ambaye hufanya biashara za bar na kusambaza vyakula kwenye kambi za jeshi anadaiwa kulundika kiasi hicho cha fedha kwa muda mrefu bila kutoa kiasi, na kwamba mfanyakazi huyo aliona huenda anayeimiliki alishakufa na kuanza kuchomoa kidogo kidogo na kufikia zaidi ya Tsh. Milioni 100.
Hata hivyo baada ya taarifa hizo kubainika uongozi wa benki ulifanya kikao kizito na kubaini kwamba mfanyakazi wao aliyefahamika kwa jina moja la Samweli ndiye aliyehusika na wizi huo kwa kuchomoa fedha hizo kidogo kidogo hadi kufikia hicho cha fedha.
Uongozi wa benki hiyo tayari umemsimamisha kazi lakini suala hilo bado lipo kimya huku Mfanyabiashara huyo akilalamikia hatima ya fedha zake, maana benki hiyo kuwa kimya na haimpi jibu linaloeweka namna ya kurejeshewa.
Hizo pesa labda nyingi kwako sio kwa Nshomire larugendo aseeIla mtu unakuaje na kiasi kingi hicho cha pesa na wala usifatilie hata balance asee. Daah kweli tuko tofauti.
Hivi Matako bar ni ya huyu mhaya?? Nasikia Angelo Mwoleka pia alikuwa mmiliki ila siku hizi imefubaaAlijiaminisha vipi mwenye pesa zake kafa. So stupid and incompetent. Ila Joseph ana hela bwana. Mpaka akazisahau hizi 100M. Sijui matako bar bado ipo? Ilijua kumpatia pesa ndefu 🙌🏾🙌🏾
ikaMbona kesi rahisi sana hiyo bank wanapaswa walipe haraka kanuni ya vicarious liability bank hawachomoki. Kama mna shida kisheria semeni niwasaidie
Inakuwaje pesa zichomolewe asipewe taarifa kwa ujumbe mfupi? Au huyo jamaa alifanya yake zikitolewa asipate taarifa?