Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 3,585
- 8,106
Mfanyabiashara mwenye maduka ya vinywaji vya jumla na rejareja Mjini Babati, Peter Mushi amekutwa ndani kwake amefariki dunia baada ya kujinyonga.
Afisa Mtendaji wa mtaa wa Sawe, Simon Majura amesema tukio hilo limetokea katika mtaa wa Sawe wilaya ya Babati Mkoani Manyara na kwamba jeshi la polisi lilifika eneo la tukio kuuchukua mwili.
Majirani wanasema hakuwa na ugomvi na mtu yeyote isipokuwa siku za hivi karibuni akikuwa mnywaji wa pombe kupindukia hali iliyokuwa inamlazumu mkewe kuwaomba majirani zake wamsaidie kumbeba na kumrejesha nyumbani.
Mushi ameacha mke mmoja na watoto wawili
Clouds