Ni unyama na ukatili wa kutisha! Asubuhi ya leo Alhamisi, Juni 12, 2025, maeneo ya Bonyokwa wilayani Ilala jijini Dar, wanandoa ambao majina yao hayakupatikana mara moja, wamekutwa wamekufa kwa kuchinjwa kikatili na kitu chenye ncha kali!
Kwa mujibu wa vyanzo, tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo baada ya watoto kuingia chumbani kwa wazazi wao asubuhi na kukutana na miili iliyokuwa na damu ikiwa imelala sakafuni.
Majirani walioongea katika eneo la tukio ambalo ni jirani na baa moja inayojulikana kwa jina la GK huko Bonyokwa, wamesema kelele za watoto baada ya kuona miili ya wazazi wao ikiwa chini chumbani ndiyo iliyofanya kugundulika kwa mauaji hayo.
Imeelezwa kuwa, marehemu baba wa familia hiyo alikuwa mfanyabiashara mwenye uchumi wa kati.
Hata hivyo, wauaji hao hawakuchukua chochote licha ya madai ya kukutwa kwa pesa nyingi juu ya kitanda chumbani.
Baadhi ya mashuhuda walisikika wakisema huenda mauaji hayo ni ya kisasi cha mambo ya kibiashara hasa baada ya kitendo cha kukutwa kwa pesa nyingi kitandani.
Inaelezwa pia kuwa, siyo msichana wa kazi wala mwanafamilia yeyote mwingine aliyesikia mizozo au kukurukakara zaidi ya miili kukutwa asubuhi.
Polisi walifika eneo la tukio asubuhi kwa ajili ya uchunguzi wa awali na kutwaa miili hiyo kuipeleka hospitali kwa hifadhi ya kusubiri taratibu nyingine. R.I.P.