Mfanyabiashara Ramadhan Hamis Ntunzwe, adai TRA hawajatekeleza agizo la Rais. Je, Kamishna Mkuu TRA afukuzwe kazi na Yono ifilisiwe mali zake?

Acheni kusingizia watu.....TRA wanatekeleza maagizo ta rais aliyesema anataka kuona matajiri waishi km mashetani.....

Sasa hapo tra wana kosa gani maana ni maagizo kutoka juu
Sidhani rais anajua huu uhuni wanaofanya TRA. Yaani taasisi ya umma kama kundi la majangili
 

Umeongea pumba sana sikutegemea wewe ni kiazi namna hii. Yaani jamaa kavumilia tangu 2016. Kaibiwa karibu Biliaon 1 kwa kukataa kutoa rushwa ya milion 2 kuwapa TRA.

Dada yake alikufa kwa mshtuko baada ya kuibiwa, mke wake kaugua wehu, watoto hakuna ada ya kuwalipia masomo. Malalamiko yake yamefika mpaka kwa raisi. Halafu unaongea utumbo wa kuku
 
Serikali inashindwa kuwahudumia wananchi halafu inawalaumu CDM?!! Mwisho October.
 
Nimetoa mtazamo wangu na uzoefu wangu katika masuala ya Biashara Mkuu, punguza ukali wa maneno, Sipendi Ligi na mtu yeyote na mimi daima naamini kunguru mwoga huokoa ubawa wake.

Haya sawa Wamlipe hizo Bil. 2 au hata 100 je zitarudisha Dada yake, zitarudisha watoto. Ujuaji mwingi wakati mwingine ni UJINGA na UJUHA anyway kila mtu ana Falsafa zake za Maisha naomba ligi iishe na wewe natengua Kauli, HUYO JAMAA AENDELEE KUKOMAA NAONA NI BONGE YA MJANJA, hapo vipi we Jamaa yangu MUHA utaendelea KUBISHA au bado unakomaa WACHU! I salute u
 

Sawa subiri uteuzi, utateuliwa
 
Hii issue naona hata viongozi wa serikali wanahusika
 

Duu wewe sio mfanyabiashara jamaa anadai haki yake na sio vinginevo
 
Hili Sakata ni la muda kidogo..... Jamaa anajua kujieleza na Ana kumbukumbu kali sana
Hasahau hata nukta.

Alisha zungmza pale Rais alipokutana na wafanyabiashara. Rais alitoa maagizo lkn bado Hao TRA hawajayatekeleza....
Nchi hii ngumu sana, Ukisikia uonevu ndiyo huo

Ova
 
Hizi sheria wanazozipitisha ipo siku zitawafunga kamba mikono
 
Ndio ni muha wa Kigoma, ila anaonekana ana uwezo sana wa akili japo ni std 7. Ni mfanya biashara mkubwa
Kuna mchezo anachezewa,viongozi wa juu wa nchi hawaujuwi

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Outed news.
Mleta mada jitahidi uendane na nyakati Hii habari mbona tulisha itoaga Muda mrefu Sana ulio pita?
 
Outed news.
Mleta mada jitahidi uendane na nyakati Hii habari mbona tulisha itoaga Muda mrefu Sana ulio pita?

Ndugu yangu, hata ingekuwa ya miaka 10 swali liko pale pale, je amelipwa haki yake??. Haya naomba usikilize ya leo hii hapa ambayo haijapitwa na wakati, bofya hapa

 
Huyu jamaa ni wa kitambo na sijui mambo yake yanaendeleaje.

Jamaa anadai karibu bilioni moja sasa kwa awamu hii ni nani aingie hazina achote bilioni moja ampe?...yaani ni bora ibaki hivyo kwamba maagizo ya Wakubwa hayajatekelezwa kuliko hiyo pesa itoke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…