Mfanyakazi/Mwajiriwa sasa kupewa TIN Number ili kutambulika kama mlipa kodi kupitia PAYE

Mfanyakazi atakwepaje kodi wakati inakatwa moja kwa moja kutoka kwenye mshahara wake?
 
Wafanya biashara wameshaisoma namba sasa zamu ya waajiriwa na waajiri wao.
 
Umenikumbusha foleni za NIDA na usajili wa SIM cards kwa alama za vidole!!!
Your browser is not able to display this video.
 
Una utoto sana..
Kwamba muajiri nikiamua kuwafanya 50% muwe diwaka nashindwa vipi...
 
Reactions: Cyb
Watu wanaleta ubishi usio na maana. Hata jambo la wazi kama hili unataka ubembelezwe mpaka lini?
TRA wametoa elimu kwa muda mrefu na tangazo la muda mrefu. Kwa hiyo wametoa muda wa kutosha na elimu juu. Sasa Kama mtu hataki kutekeleza ni lazima kutumia enforcement.
Kama muungwana na unaeleweka na 'vitisho' tekeleza ndani ya muda
 
Dah! Kwamba katolewa chambo? TRA ni watu ambao wana majukumu makubwa lakini yako kwa watu wasiojitambua. Tembelea ofisi zao ukiwa na mzigo bandarini ndo utajua umuhimu wa ufahamu. Nadhani kwa muda mrefu wamekuwa wakihangaishana na wafanyabiashara kiasi kwamba kila wanayemuona wanadhani anaweza kutoa chochote.

Nawalinganisha na dereva wa treni ambaye hahitaji ubunifu ili kujua apite wapi kwa usalama wa chombo chake. Hawaoni hata makorongo!
 
Sijui ni stress au kufanya kazi under pressure!! Viongozi wengi msimu huu wako hivyo.
 
Nadhani tatizo siyo kujua maana ya TIN na faida yake, tatizo ni uwasilishaji wa taarifa. Ni kweli TRA wana madaraka juu ya mwajiliwa wa wizara ya Elimu? Wamezoea kufukuzana na wafanyabiashara sasa wanajisahau na kuamini kila mtu ni himaya yao.
Umenikumbusha enzi za kubadilisha namba za magari. Jamaa hawa nao walikuwa wanakaa barabarani wanafukuza magari eti nayo ikiwa ni kazi yao! Bahati mbaya wao wenyewe ndo walijipa kazi na tenda za kihuni kulazimiasha kila mtu apate plate kutoka kwa mtu mmoja tu! Rushwa hizo!
 
Sijui ni stress au kufanya kazi under pressure!! Viongozi wengi msimu huu wako hivyo.
KUna tabia ya kuiga utendaji wa aliyejuu lakini nadhani wao wenyewe walistahili kuondoa elimu mbovu zilizo ndani ya ofisi zao kabla hawajaanza kuhangaika na walio nje ya ofisi zao.
 
Ukishangaa hilo tamko ni kama haujui upepo unapoelekea mkuu tumeshayatimba mzee baba kilichobaki ni kutii tamko lolote bila shuruti
 
Hebu eleza faida ya kuwa na hiyo Tin no. hasa kwa mfanyakazi wa sekta binafsi ambaye anafanya kazi kwa mkataba wa mwaka mmoja au miwili then anarudi zake kitaa baada ya kazi kwisha.
 
Nadhani tatizo siyo kujua maana ya TIN na faida yake, tatizo ni uwasilishaji wa taarifa. Ni kweli TRA wana madaraka juu ya mwajiliwa wa wizara ya Elimu? Wamezoea kufukuzana na wafanyabiashara sasa wanajisahau na kuamini kila mtu ni himaya yao.
Na je TRA wana uwezo wa kuzuia mshahara halali wa mfanyakazi ambaye ametimiza wajibu wake kwa mwezi mzima? Miaka yootee walikuwa wapi na hiyo sheria yao? Nani kawakurupusha huko?
 

TRA wa nayo namlaka ya kufuatilia kama hutaki kulipa kodi,wanakukamatia mali zako
 
Huyu amesahau yaliyompata Kaimu Katibu Mkuu Elimu aliyetangaza mambo ya kukomesha Ajira za walimu wa Cheti pasipo kusoma alama za nyakati. Naamini huyu wa TRA angetoa hii clip tarehe 26/10 mpaka sasa angekuwa keshatenguliwa nafasi, kwa hakika kachemka.
 
Lakini hiyo mbona siyo ufumbuzi? Mfano mie nimeajiri madereva, mikataba yao inaonesha wanalipwa Tz. X. Lakini mimi nawalipa kiukweli Tz. Y., ambapo Y>X, na hiyo tunafanya kwa makubaliano, hiyo TIN itasaidia nini? Maana yenyewe inatumia documentation, na documentation inaonesha Tz. X?
 
Atatenguliwa Sasa Hivi, Subiri Kidogo Uone
Tumeanza Kufokewa Haraka Mno Hata Mwezi Toka November 05
πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜€πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜ƒπŸ˜πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜…πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜πŸ˜πŸ˜‚πŸ€£
Maji Tutaita Mmaa!! Haki Ya Mungu
 
Inaonekana uko huko huko TRA... Kwanza hii issue kuna mkubwa kawakurupusha meaning that hamjui wajibu wenu na hamko creative kubuni New sources za kodi, mmekomaa na kodi za mishahara tuu. Na kukuthibitishia kwamba mmekurupuliwa huko ndiyo maana mmekuja mkuku na kuweka Altmatum kitu ambacho TRA kisheria hamna huo uwezo wa kuzuia mishahara halali ya wafanyakazi. Imagine leo Novemba inaingia wiki ya tatu halafu eti Altmatum till end of December kwa wafanyakazi nchi nzima kweli????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…