Mfanyakazi/Mwajiriwa sasa kupewa TIN Number ili kutambulika kama mlipa kodi kupitia PAYE

kwenye hili TRA wananiwinda... wamenipata sasa maskini... iko hivi....

Nilifungua biashara yangu miaka 10 nyuma ila nikaja kuifunga mwaka juzi baada ya hasara, sasa kule nadaiwa kodi pesa nyingi.. kosa langu wakati wa kufunga biasharar yangu sikuwaandikia barua.. sasa kodi inajizalisha hadi majuzi ndiyo nikashituka nikaandika kusitisha biashara ila kodi ni balaa - sasa nikimpa HR hiyo TIN si watanikamata kama kuku bandani? yaani nimejipeleka mwenyewe na wataanza kunikata kwenye mshahara ?

Kodi nayodaiwa hata kwa miaka 20 sitaweza kuilipa - nafikiria kuacha kazi lakini si kuitoa tena ile TIN number kwao.
 
Mimi mda wa kutunza pesa kwenye mabenki sina ,ntakachokuwa nafanya ili kupunguza kuwa na cash kubwa ni kwenda biuro de chenji kupata pesa za kigeni afu nakaa nazo na sifungui acc yoyote ya pesa za kigeni hadi cash azidi kiasi fulani
 
CCM wamekula pesa za corona wanatafuta namna ya kupata pesa za kufidia huo ufujaji
Utaratibu wa kutumia TIN kwa watu wote ni mzuri sana! Kila mtu lazima alipe kodi. Kwa ujumla ni wokovu kwa watu fulani ambao wamekuwa ni waathirika wa waajili wao. Sekta ya mahoteli nchini inawaumiza waajiliwa wao bila sababu kwa kuwalipa mishahara isiyo rasmi na bila kuwaingiza kwenye mifuko ya pensheni.

Tatizo ni kama mleta mada alivyoandika, lugha iliyotumika na TRA ni ya kizembe! Ndo lugha inayotumika kwa wafanyabiashara na matokeo yake kila leo ni kubishana na kutoelewana. Tunawajua TRA kwa rushwa na ndo msingi wa lugha yao ambayo sasa inavuka mipaka hadi kwa waajiliwa wasio na uhusiano wa moja kwa moja na TRA. TRA ni sehemu ya serikali, ilistahili kuwasiliana na waajili siyo waajiliwa maana wanaotuma TIN siyo waajiliwa ni waajili.
 
Kimsingi TRA huwa wanawasilisha taarifa zao kwa vitisho hivyo hivyo haijalishi anamuandikia nani,sijajua sheria iliyoianzisha TRA imewapa meno kiasi gani.Unakuta barua kasini meneja wa TRA mkoa na anamuandikia meneja mwenzie wa mkoa kwenye taasisi nyingine kumuamuru awasilishe taarifa za walipa kodi wa wateja anaowahudumia,the same to TAKUKURU.Nadhani sheria zimewapa nguvu zaidi hawa jamaa
 
Mkuu mimi nitadili na vitu vya kilimo na mifugo basi,mambo ya biashara za kufuatiliwa na TRA siwezi
 
Waajiriwa taarifa wanazo tangu Julai 2020 na deadline ilikuwa September.

Kwa taarifa yako/yenu haichukui nusu saa mtumishi kuwa na TIN number ilimradi awe na kitambulisho cha taifa NIDA.

Watumishi wa Umma 99% wanavyo vitambulisho au number za nida
Habari za hapo TRA!
 
We mtu umenikumbusha somo la mawasiliano, communication skills. kilicholalamikiwa ni kingine, wewe unaeleza mengine. Huoni huyo mwandishi anaijua TIN? Tatizo ni mawasiliano yaliyotoka TRA. Unamtisha mwajiliwa wakati anayetakiwa kukuletea TIN ni mwajili? btw., vitisho vya nini? Nani kakukosea wewe TRA? Nani kasema waajiliwa hawana uelewa wewe TRA?
 
We mtu umenikumbusha somo la mawasiliano, communication skills. kilicholalamikiwa ni kingine, wewe uneleza mengine. Huoni huyo mwandishi anaijua TIN? Tatizo ni mawasiliano yaliyotoka TRA. Unamtisha mwajiliwa wakati anayetakiwa kukuletea TIN ni mwajili? btw., vitisho vya nini? Nani kakukosea wewe TRA? Nani kasema waajiliwa hawana uelewa kama wewe TRA?
 
Ngoma inogire....[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Wewe salama yako ni kuikimbia hiyo ajira yako fasta, vinginevyo unaenda KUIBULIWA kwenye uhujumu uchumi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…