Mfanyakazi/Mwajiriwa sasa kupewa TIN Number ili kutambulika kama mlipa kodi kupitia PAYE

Mfanyakazi/Mwajiriwa sasa kupewa TIN Number ili kutambulika kama mlipa kodi kupitia PAYE

kwenye hili TRA wananiwinda... wamenipata sasa maskini... iko hivi....

Nilifungua biashara yangu miaka 10 nyuma ila nikaja kuifunga mwaka juzi baada ya hasara, sasa kule nadaiwa kodi pesa nyingi.. kosa langu wakati wa kufunga biasharar yangu sikuwaandikia barua.. sasa kodi inajizalisha hadi majuzi ndiyo nikashituka nikaandika kusitisha biashara ila kodi ni balaa - sasa nikimpa HR hiyo TIN si watanikamata kama kuku bandani? yaani nimejipeleka mwenyewe na wataanza kunikata kwenye mshahara ?

Kodi nayodaiwa hata kwa miaka 20 sitaweza kuilipa - nafikiria kuacha kazi lakini si kuitoa tena ile TIN number kwao.
 
Wazo kuu ya hili swala ni kubaini wanaokwepa kodi.Sasa itakuwa ni rahisi kubainiwa,kwa sababu record yako ya kulipa kodi ipo,inalinganishwa na mwenendo wa account zako,kama haziendani,wanajua unaibia serikali.Mfano,wewe ni mwajiriwa na ina vibiashara vyako kadhaa,ela zako pia unatunza bank,wataona ela ni nyingi kuliko kodi wanayokusanya kwako.Utaitwa kutoa maelezo.Hapo ndio mtaelewana,mitano tena..
Pia ukiuza chochote,ela ukalipiwa bank,kodi hukulipa...jua record yako ipo.. mambo ya muda tuu...
Mimi mda wa kutunza pesa kwenye mabenki sina ,ntakachokuwa nafanya ili kupunguza kuwa na cash kubwa ni kwenda biuro de chenji kupata pesa za kigeni afu nakaa nazo na sifungui acc yoyote ya pesa za kigeni hadi cash azidi kiasi fulani
 
CCM wamekula pesa za corona wanatafuta namna ya kupata pesa za kufidia huo ufujaji
Utaratibu wa kutumia TIN kwa watu wote ni mzuri sana! Kila mtu lazima alipe kodi. Kwa ujumla ni wokovu kwa watu fulani ambao wamekuwa ni waathirika wa waajili wao. Sekta ya mahoteli nchini inawaumiza waajiliwa wao bila sababu kwa kuwalipa mishahara isiyo rasmi na bila kuwaingiza kwenye mifuko ya pensheni.

Tatizo ni kama mleta mada alivyoandika, lugha iliyotumika na TRA ni ya kizembe! Ndo lugha inayotumika kwa wafanyabiashara na matokeo yake kila leo ni kubishana na kutoelewana. Tunawajua TRA kwa rushwa na ndo msingi wa lugha yao ambayo sasa inavuka mipaka hadi kwa waajiliwa wasio na uhusiano wa moja kwa moja na TRA. TRA ni sehemu ya serikali, ilistahili kuwasiliana na waajili siyo waajiliwa maana wanaotuma TIN siyo waajiliwa ni waajili.
 
Kimsingi TRA huwa wanawasilisha taarifa zao kwa vitisho hivyo hivyo haijalishi anamuandikia nani,sijajua sheria iliyoianzisha TRA imewapa meno kiasi gani.Unakuta barua kasini meneja wa TRA mkoa na anamuandikia meneja mwenzie wa mkoa kwenye taasisi nyingine kumuamuru awasilishe taarifa za walipa kodi wa wateja anaowahudumia,the same to TAKUKURU.Nadhani sheria zimewapa nguvu zaidi hawa jamaa
 
Naomba nitoe mfano kidogo tu ,nilikuwa na duka sikulipa kodi kwa miez sita baada ya mda wa mwanzo kifika ,nikawa na bajaji ikakamatwa nilipokwenda Sumatra walinitaka nifike tra kulipoa leseni .kuingiza tin yangu ilionekana na biashara nyingine ya duka nadaaiwa hivyo ilibd nilipie kodi ya duka na bajaj ndo niruhusiwe kuondoka nayo.

Kiufupi tin ni nzuri lakn wafanyakaz mjipange kulipa kodi kiufasaha kabsa kwa kila mnachofanya kuongeza kipato.pia biashara yako .na mda wa kufanya biashara bila kuzingatia mda wa serikal unaolipwa mshahara pia nao utafuatiliwa vizur

Nendeni kachukueni tin mtimize malenho ya serikal lakn mjue kuishi kiujanja ujanja na kukwepa kwedi itakuwa mwisho

Kwa pamoja tuijenge nchi

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Mkuu mimi nitadili na vitu vya kilimo na mifugo basi,mambo ya biashara za kufuatiliwa na TRA siwezi
 
Waajiriwa taarifa wanazo tangu Julai 2020 na deadline ilikuwa September.

Kwa taarifa yako/yenu haichukui nusu saa mtumishi kuwa na TIN number ilimradi awe na kitambulisho cha taifa NIDA.

Watumishi wa Umma 99% wanavyo vitambulisho au number za nida
Habari za hapo TRA!
 
Mkuu unahitaji elimu, suala la TRA kutaka kila mwajiriwa awe na Tin ni jambo la busara sana. Kumekuwa na ukwepaji wa kodi mkubwa sana utakuta kampuni inawajiri hta 100 alafu paye wanasema wana waajiri 50. Huenda hata wewe hapo ulikuwa unakatwa paye kwenye msahara lakn haifiki serikalini muhasibu au mwajir anafaidi anakula.

Huu mfumo mpya ni mzuri kabisa kwasababu mfanyakazi nae analipa kodi ukiachana na mfanyabiashara tena kuna wafanyakazi wanalipa kodi kubwa kushinda hata hao wafanyabishara.

TRA ni chombo cha serikali hivo kinapokea maagizo kutoka juu. Na suala la kutumia TIN taarifa ilitoka muda sana.ulikua wapi boss??
We mtu umenikumbusha somo la mawasiliano, communication skills. kilicholalamikiwa ni kingine, wewe unaeleza mengine. Huoni huyo mwandishi anaijua TIN? Tatizo ni mawasiliano yaliyotoka TRA. Unamtisha mwajiliwa wakati anayetakiwa kukuletea TIN ni mwajili? btw., vitisho vya nini? Nani kakukosea wewe TRA? Nani kasema waajiliwa hawana uelewa wewe TRA?
 
Mkuu unahitaji elimu, suala la TRA kutaka kila mwajiriwa awe na Tin ni jambo la busara sana. Kumekuwa na ukwepaji wa kodi mkubwa sana utakuta kampuni inawajiri hta 100 alafu paye wanasema wana waajiri 50. Huenda hata wewe hapo ulikuwa unakatwa paye kwenye msahara lakn haifiki serikalini muhasibu au mwajir anafaidi anakula.

Huu mfumo mpya ni mzuri kabisa kwasababu mfanyakazi nae analipa kodi ukiachana na mfanyabiashara tena kuna wafanyakazi wanalipa kodi kubwa kushinda hata hao wafanyabishara.

TRA ni chombo cha serikali hivo kinapokea maagizo kutoka juu. Na suala la kutumia TIN taarifa ilitoka muda sana.ulikua wapi boss??
We mtu umenikumbusha somo la mawasiliano, communication skills. kilicholalamikiwa ni kingine, wewe uneleza mengine. Huoni huyo mwandishi anaijua TIN? Tatizo ni mawasiliano yaliyotoka TRA. Unamtisha mwajiliwa wakati anayetakiwa kukuletea TIN ni mwajili? btw., vitisho vya nini? Nani kakukosea wewe TRA? Nani kasema waajiliwa hawana uelewa kama wewe TRA?
 
Huu utaratibu ulianza toka mwanzoni mwa mwaka huu nadhani kama sio February/March huko

Na kodi hapa inayotafutwa ni ya wale walioajiriwa sekta binafsi

Wafanyakazi was maduka,madereva,walinzi no

Yaani Yale maswala ya kulipana mshahara kwenye bahasha laki 2 na nusu halafu sie waajiri tunaingiza mshahara kwenye matumizi tunapigiwa hesabu ya kodi tunalipa ndio mwisho

Inatakiwa na mshahara wa muajiriwa ukatwe PAYE kama wanavyofanyiwa watumishi wa umma halafu Kofi ipelekwe TRA ikiainisha na TIN ya muajiriwa wako

Patamu sana hapa
Ngoma inogire....[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
kwenye hili TRA wananiwinda... wamenipata sasa maskini... iko hivi....

Nilifungua biashara yangu miaka 10 nyuma ila nikaja kuifunga mwaka juzi baada ya hasara, sasa kule nadaiwa kodi pesa nyingi.. kosa langu wakati wa kufunga biasharar yangu sikuwaandikia barua.. sasa kodi inajizalisha hadi majuzi ndiyo nikashituka nikaandika kusitisha biashara ila kodi ni balaa - sasa nikimpa HR hiyo TIN si watanikamata kama kuku bandani? yaani nimejipeleka mwenyewe na wataanza kunikata kwenye mshahara ?

Kodi nayodaiwa hata kwa miaka 20 sitaweza kuilipa - nafikiria kuacha kazi lakini si kuitoa tena ile TIN number kwao.
Wewe salama yako ni kuikimbia hiyo ajira yako fasta, vinginevyo unaenda KUIBULIWA kwenye uhujumu uchumi tu.
 
Back
Top Bottom