Mfanyakazi/Mwajiriwa sasa kupewa TIN Number ili kutambulika kama mlipa kodi kupitia PAYE


Yah ni kweli ila sharti biashara yako iwe na mhasibu ila ukiwa serious ukafuatilia ina unafuu kwa mfanya kazi alafu ukafanya biashara. Maana unakuta mfanyakazi wa basic salary ya mil 3 unalipa PAYE karibia laki 7 na ushee...kwa mwaka ni mil 9...sasa mfanyabishara wa mil 9 kodi tu si mkubwa huyo??
 
HII NI NZURI SANA KWA WAFANYAKAZI
Kweli kabisa boss wangu
1. Itawasaidia wafanya kazi wa serikali kukatwa hela zao Kama Kodi.
2. Itawasaidia waajiriwa wote kutokwepa Kodi na kujiingiza kwenye uhuni.
3. Itawasaidia wafanyakazi hata wa ngazi za chini kujua komputa.
4. Huu ubunifu utaokoa muda kwa madereva wa mabosi wakubwa wakubwa.
 
deceiver, cjakuelewa mkuu
 
Kuna nchi Kila bodaboda Ina kapu la takataka limefungwa karibu na dereva (dustbin) Kama ilivyo kwenye daladala ili kutunza mazingira
 
Sio lazima kuwa na muhasibu.

Declarant anaweza kuwa wewe mwenyewe Taxpayer.!
 
Sahihi kabisa mkuu
 
Kwahiyo waanze tu kuagiza magari kutakuwa na punguzo la Kodi eti.
 
Umetoa ufafanuzi nzuri saana, ila ID hii huwa naichukia, kale kaskendo kako.
 
Lengo linaweza kua zuri, ila swali ni lile lile kua return (interms of social services etc) inaendana na PAYE zetu! ...ingawa nadharia ya ulipaji kodi haitaki utegemee manufaa ya moja kwa moja kwa kodi unayolipa (wanazuoni najua mnaelewa hii)!
 
Ni ujinga tu nchi za wenzetu ukilipa kodi kubwa kuliko kiwango kilichowekwa kulipwa ile extra unarudishiwa,sasa hii inamsaidia nini mfanyakazi?
 
Hii ni kwa ajili ya kukusanya Kodi zaidi kwa serikali. Kuna ajira nyingine hasa makampuni madogo wafanyakazi wanalipwa mishahara na hawalipi hata senti Kama Kodi. Serikali umelenga watu hawa ambao ni wengi Sana ambao Kama wangekatwa paye basi hela nyingi mno ingepatikana.
Pili kupitia TIN hata wanaodaiwa na taasisi Kama bodi ya mikopo ya elimu ya juu ambao wameajiriwa au kujiajiri sekta zisizo rasmi sana itakuwa rahisi kuwanasa.
Kwakifupi mtafutano unaanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…