JABALI LA KARNE
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 3,093
- 5,850
Katika makosa yaliyofanyika hapo nyuma ni kumpa afisa wa kawaida uwezo wa kumfanya mfanyabiashara atakavyo. Hawana busara panapohitaji busara, hawana subira panapohitaji subira, hawana huruma panapohitaji huruma, Hawatumii tena akili endapo hawajafikia lengo wanalokusudia.Kwa mujibu wa yule jamaa sasa hivi maafisa wa TRA wanajipigia tu rushwa kwa sababu hata wakikomaa mdau anapiga simu juu na wao wanaishia kufokewa tu
MATOKEO: Ni kweli Kodi ilikusanywa kwa fujo, magari yalikamatwa, akaunti zikafungwa, wafanyabiashara wakajawa hofu,wengine wakaficha fedha wasijue la kufanya, wale wenye presha wakasidiwa na corona kuaga dunia(Tumezika aisee).
Nina rafiki ambaye alipewa tax position ya zaidi ya m700 bila aibu halafu baadae ikaonekana anadaiwa m25 tu ambayo nayo ingechunguzwa vizuri huenda ni janja janja za kodi, hiyo nyingine palikuwa na makosa wanayosema ni makosa kidogo kwenye mfumo wao wa utunzaji wa taarifa yakazaa kodi kubwa😂😂😂.....
Ila hapo afisa kampiga biti la maaana, kashikilia na gari ni vile tu jamaa alikuwa very smart hakuna document ambayo hana hata ya tsh mia aliyolipa hivyo akawa jasiri akawa mbabe kwa kuandika barua kali na kupeleka ushahidi. kinyume na hapo labda tungezika😂😂 maana afisa alikuwa aggresive. Ushahidi ndo ukamshtua kidogo akawa mpole.