Mfanyakazi TRA: Toka nianze kazi TRA miaka 8, haupo wakati ukusanyaji kodi ulikubalika kama wa Hayati Magufuli

Kwa mujibu wa yule jamaa sasa hivi maafisa wa TRA wanajipigia tu rushwa kwa sababu hata wakikomaa mdau anapiga simu juu na wao wanaishia kufokewa tu
Katika makosa yaliyofanyika hapo nyuma ni kumpa afisa wa kawaida uwezo wa kumfanya mfanyabiashara atakavyo. Hawana busara panapohitaji busara, hawana subira panapohitaji subira, hawana huruma panapohitaji huruma, Hawatumii tena akili endapo hawajafikia lengo wanalokusudia.

MATOKEO: Ni kweli Kodi ilikusanywa kwa fujo, magari yalikamatwa, akaunti zikafungwa, wafanyabiashara wakajawa hofu,wengine wakaficha fedha wasijue la kufanya, wale wenye presha wakasidiwa na corona kuaga dunia(Tumezika aisee).

Nina rafiki ambaye alipewa tax position ya zaidi ya m700 bila aibu halafu baadae ikaonekana anadaiwa m25 tu ambayo nayo ingechunguzwa vizuri huenda ni janja janja za kodi, hiyo nyingine palikuwa na makosa wanayosema ni makosa kidogo kwenye mfumo wao wa utunzaji wa taarifa yakazaa kodi kubwa😂😂😂.....

Ila hapo afisa kampiga biti la maaana, kashikilia na gari ni vile tu jamaa alikuwa very smart hakuna document ambayo hana hata ya tsh mia aliyolipa hivyo akawa jasiri akawa mbabe kwa kuandika barua kali na kupeleka ushahidi. kinyume na hapo labda tungezika😂😂 maana afisa alikuwa aggresive. Ushahidi ndo ukamshtua kidogo akawa mpole.
 
Waanzishe chama ili wawe Kama membe? Ukishatoka ccm, nguvu zote zinaisha. Wabanane hapohapo Kama wanataka kumtoa mama Samia Ila wasijaribu kuwa nje ya CCM.
Ila hata kina membe walishindwa kumtoa jiwe, kumtoa mwenyekiti sio Mchezo eti
 
Nyalandu pia alihama, alikuwa mwenyekiti Kanda ya Kati.
 
Bado nasema una hoja.Lakini...

...kwanini chama kingine kipya na isiwe CHADEMA na vingine vilivyopo?

....kwa vinara wa kupambania mabadiriko wanakimbia risasi na kwenda kuishi ughaibuni ambapo mabadiriko hayapaswi kufanyikia huko?
Nasema hivyo nikiamini kwamba demokrasia sio lazima muwe chama kimoja cha upinzani. Mbona Maalim alienda ACT ila alimuunga mkono Lissu.

Wewe na hao kina polepole mnaonaje muanzishe chama kipya mpambane na SSH ili tuone kma mko serious kweli. Yaani muwafundishe CHADEMA jinsi ya kuwa wapinzani imara!!! Maana kila siku mnakejeli kuwa hakuna mbadala at the same time mnadai SSH hafai sasa mnataka nini? Si mhame

Tatizo lenu mnaogopa mkihama mali zitaporwa na kwamba maslahi na tender zenu zitasitishwa. Kwa unafiki huu hakuna mabadiliko mtafanikiwa, mnamtukana Mbowe ila nakuambia hapa hakuna mwana CCM anawez aanzisha chama cha upinzani kikamaliza hta miaka 5 kipo hai!!!
 
Lakufunga biashara ilikuwa ni biashara za wapiga dili! Nambie kampuni gani hata ya usafirishaji ilifunga biashara? Maana shop rite walifunga wakati wa kikwete!
Biashara nyingi za kati zilizoajiri watu zilifungwa. Huenda hukuguswa lakini huo ndo uhalisia, zilizopona zipo ambazo zina mzigo mkubwa wa kodi mgongoni.
 
Mliwaibia sana watu, washenzi ninyi.
 
Mwambie aache kasi tupo wengi tulisoma kodi
 
Halafu na hapohapo account za watu za bank zinavamiwa pesa zinachukuliwa na hao hao tra. Umeandika kinyume nyume rudi ukajipange ndugu polepole
 
, mnamtukana Mbowe ila nakuambia hapa hakuna mwana CCM anawez aanzisha chama cha upinzani kikamaliza hta miaka 5 kipo hai!!!
Sijawahi kumkosea adabu Mbowe na kwa faida yako 2001 Mbowe alinisaidia nauli ya kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam "ila usinitangaze."

Namheshimu sana Freeman.
 
Wapiga dili wapo kazini..chief mwanamke anawakenulia meno..zen anaenda kukopa mikopo kwaajili ya zenji..walipaji watanganyika..sawa tutafika tu.

#MaendeleoHayanaChama
Jpm alikopa zaidi ya trilion 30 kimyakimya lakini mama Ni trili moja tu. Sasa Nani mkopaji hapo.
 
Mkuu
Wewe kweli ulifanya biashara awamu ya tano
Hakuna muda Tra walikuwa miungu watu kama awamu hiyo
 
Reactions: Tsh
Mleta Mada katuletea CHAI ya sukuma Gang au ni wale waliowekwa Idara maalumu wachote na kupeleka Chato
Uwanja wa ndege umejengwa na Shemeji yake kabisa bado kina zitto wakalalamika bado Ndugai akaminya na kuzuia wapiga kelele
Katibu Mkuu Fedha kipindi hicho anasaini mikopo kibao leo mnasema hatukukopa
 
Kilio Cha mla rushwa aliyepangwa kitengo ambacho hakina rushwa.
 
Ukusanyaji Kodi wa DHULUMA umezikwa naye pale Chato. Kinondoni peke yake kwa mwaka wafanyabiashara zaidi ya 300 walikuwa wanafunga biashara zao kutokana na HARASSMENT ya TRA na task force.

Kama ni umaskini basi Nchi yetu iendelee kuwa maskini lakini UJINGA wa kudai RISITI kwa kila huduma peleka Chato makaburini. Unadai kodi mpaka kwa mama Nitiliye, je ni lini utamfanya AKUE awe na hoteli?

Nchi zenye akili Zina deal na 20% ya taxpayers ambao ni Big Taxpayers wanaoweza kukupa 80% ya Kodi yako yote. Siyo unaajiri maafisa TRA kuja kukimbizana na Kodi za stationery shop, maduka ya mangi, Mama ntiliye, migahawa, wauza mitumba etc. HUO ni UKICHAA.

Siyo kwamba Rais SSH kashindwa kukusanya kodi, LA HASHA. Bali Magufuli alianzisha mega projects 3 kwa wakati mmoja; SGR, Stiglers Gorge na Dodoma City. Mbali ya projects zingine kama Busisi, hospitals na barabara.

Hizo projects zinahitaji fedha za kujengea na zingine tumeanza kulipa riba wakati hatujaanza kuzalisha
 
Kuteka kina Mo ndo kulipa kwa hiari
 
Unafunga akaunti yenye turnover ya m50 kwa mwaka😀
 
Kwa mujibu wa yule jamaa sasa hivi maafisa wa TRA wanajipigia tu rushwa kwa sababu hata wakikomaa mdau anapiga simu juu na wao wanaishia kufokewa tu

Huyu Suzy Elias amen create hii Akaunti kwa malengo maalum. Prey wake wakubwa ni January Makamba na Rais SSH.

Amen join hapa Nov 9, 2021. Huyu aweza kuwa ni mmoja wa wahanga wa reshuffle ya mwisho ya Rais SSH iliyowatoa akina Kalemani, Ndugulile na Chamuriho. Kimsingi ni member wa Sukuma Gang
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…