Kuna mtu mmoja mpuuzi nilisoma bandiko lake Jana anadai eti, "Unaandamana mwisho uumie Kwa faida ya nani?"
Nilishangaa sana nikaona hapa mabadiliko itakuwa kitendawili.
Mimi nilifanya mageuzi kwenye chuo nilichokuwa nasoma ilinigharimu ila kizazi nilichoacha kilifurahia mabadiliko ya ghafla. Imagine chuo kikuu hakina facilities za kutosha mnahama na viti kwenye venues. Wifi Hamna mnahangaika na ma bundles na system ya usajili hakuna mnapanga foleni siku nzima mnasota kwenye mabenchi.
Yote haya yalifanyiwa changes kabla hata sijamaliza third year ila ni matatizo ambayo yalikuwepo toka naanza certificate management ikawa inaona sawa tu.