ryan riz
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 423
- 683
Tusidanganyane mfumo imara hujengwa na watu majasiri,shupavu na walio imara kwenye kusimamia sheria. je hao watu tunao?
Mfumo imara hutegemea wananchi imara wenye kujua sheria na taratibu za nchi zao na hasa haki zao za msingi na iwapo sheria, taratibu na haki zao katika nchi zikivunjwa au kuminywa hujua hatua stahiki inayopaswa kuchukuliwa.
JE, TUNAO HAO WATU?
Mfumo imara sheria zake hazipo kulinda sana viongozi ILA kulinda nchi na ukumbuke wanaopitisha hizo sheria ni hao hao viongozi.
JE TUNAO VIONGOZI AMBAO WAKO TAYARI KWA LOLOTE DHIDI YAO WANAPOKIUKA/VUNJA SHERIA ZA NCHI.?
mfumo imara huwaondoa watumishi wengi wavivu,wasiozalisha au wenye magonjwa ya muda mrefu(mfano kwa muda wa miaka mitatu na kuendelea katika utumishi) je watumishi wa serikali wako tayari kwa hilo?
mfumo imara hupelekea kuawawa kwa viongozi na watu wenye ushawishi pale maslahi ya nchi yanapokuwa na tishio dhidi yao.
JE, HAWA WATU WAKO TAYARI?
Mfumo imara hupelekea vitu kufanyika kwa uangalizi wa karibu sana (na hapa watendaji wengi wa serikali huwa hawapendi kufuatiliwa utendaji wao wa kila siku na chuki huanzia hapa, japo hao hao ndio wanaolilia mifumo imara..?)
Mfumo imara uruhusu vyombo vya habari kuwa huru na kuruhusu habari za kiuchunguzi kufanyika taasisi za kiserkali na kibinafsi na kuwalinda waandishi hao isipokuwa zile habari tu ambazo zinaweza kuwa ni tishio kwa nchi kuwekwa kwa umma japo pia huwanyiwa kazi na vyombo husika.
JE TAASISI GANI IKO TAYARI IKIWA TUNAJUA MADUDU YAO KILA SIKU JAPO YANAFICHWA..hapa kila mwaka viongozi watakuwa wanabadilika kwenye hizo taasisi na mtaanza kulaumu mamlaka za uteuzi.
NB. mifumo imara ni ngumu sana kwa nchi za Kiafrika,Asia na baadhi ya nchi za Amerika kusini.
Zote hugemea kiongozi mkuu anatakaje kuondesha nchi basi waliobakia wote hufuata mwelekeo wake.
Akiwa mzuri nchi itastawi ila akiwa mbovu nchi huzama shimoni.