Mfumo imara huhitaji watu imara. Tanzania tuna watu wavivu walalamishi, waongo na walafi

Mfumo imara huhitaji watu imara. Tanzania tuna watu wavivu walalamishi, waongo na walafi

Mfumo imara ni ngumu sana kwa nchi changa...tuko kwenye survival mode..kuanzia ngazi za juu za uongozi mpaka chini watu wanapambana kupata basic needs...hatuna accountability

JPM amejitahidi kurudisha nidhamu ya kazi, accountability na kuelimisha wajielewe kwanini wako kwenye hizo position...naamini tungeendelea nae miaka mingine 10 huenda tungenyooka vya kutosha na kukomaa uzalendo maana tabia huzaa mazoea, tungezoea kubana matumizi yasio ya lazima, tungezoea kuishi bila kupiga madili kwenye pesa za umma, tungezoea kutatua kero za wananchi bila kusubiria ziara ya Raisi ...na hapo ingekuwa mtelezo kutengeneza mifumo imara ambayo itaendesha nchi bila kutegemea tena aina ya kiongozi awe mpole ama mkali kazi zinaenda maana watumishi tayari wanajielewa...
Ukiangalia nchi kubwa kiuchumi zote zilipitia changamoto ya vita kuondoa tabaka la juu la kifalme, kifisadi, kihuni kwa ukatili ama kwa udikteta na kulinyoosha Taifa.

Ufaransa (1770), UK (1600), USA (1776) baadaye, pia Russia( 1917 - 1922), China (1927 - 1949)

Singapore, South Korea, Malaysia, zote zilikuwa na wababe wakaondoa kwa kiasi kikubwa matabaka, udini, ukanda.
 
Back
Top Bottom