Mfumo imara huhitaji watu imara. Tanzania tuna watu wavivu walalamishi, waongo na walafi

Mfumo imara unaweza kujengwa na watu waadilifu tu! Ubaya ni kwamba kuna kundi flani la raia ambao wao wanachoangalia ni maslahi yao tu kwanza! Maswala ya kuleta mifumo ambayo inaningilia ratiba zao za upigaji ndio hasa kilichofanya hayati Magufuli kuwa mwiba mkali kwao na kuchukiwa!

Watu wanataka siasa za kulindana zile ila sio mambo ya kuwajibishana! Waumie daraja la chini ila sio wale Top class ambao wameshikilia madaraka. Watu wakwapue mabilioni washindane kusimamisha mahotel mjini ila nyie makapuku mupige kelele tu na mkaushe wao yao yanaenda!
 
watu imara na majasiri hujenga mifumo imara,JE MNAO WATU IMARA WA KUIPIGANIA HIYO KATIKA IMARA(BORA) MNAITAKA.........?
 
Mfumo imara hautaki watu wavivu kama wewe
 
Wanaopewa dhamana ghafula wanakuwa manyumbu.Unyumbu ni huruka ya mnyama kujitoa ufahamu kwasababu ya hofu ama uoga (an occurrence of thoughtful people suspending their individual reasoning because of fear,'amygdala' in this case fearing their leaders or self-Absorbed group) , swali fikirishi hivi wale walio okotwa majalalani hatujifunzi toka kwao,wanauwezo mzuri sana wa kujenga hoja za kusafisha ubongo wa watu wasiojielewa wanajenga jamii mfu, 'brainwashing'
 
Uliongea vitu vikubwa sana ila comment nyingi hazikuulewa..
Kwa maana nyingine ni kwamba mpaka sasa kiufupi hatuna rasimali watu imara,wenye uthubutu na wazalendo ili kuweza kusimamia mifumo tuliyonayo japo hata kwa standard ya kati tu.

TANZANIA TUNA VITU VYA KUTUKWAMUA KWENYE UMASIKINI ILA TUMEKOSA WATU WAKUSIMAMIA HILI
 
Neno kubwa ulinena hapa
 
Kwa ripoti ya CAG na mauza uza ya Dkt tulia utajionea namna ilivyongumu kwa hizi nchi zetu kuwa na mifumo imara...kilichopo ni kulindana na kila mtu kupiga fedha za umma pale anapopata nafasi
 
Kwa ripoti ya CAG na mauza uza ya Dkt tulia utajionea namna ilivyongumu kwa hizi nchi zetu kuwa na mifumo imara...kilichopo ni kulindana na kila mtu kupiga fedha za umma pale anapopata nafasi
Sasa ndio maana anahitajika raisi ambaye ni kauzu kuliko Magufuli.

Wakifyekwa kuanzia kwenye shina basi shughuli itakuwa imeisha. Na kufyekwa kwenyewe ni kwa kusimika sheria ngumu kiasi kwamba mtu kabla hajafanya upumbavu anajifikiria mara 2.

Raisi awe imara tu na mahakama na bunge zifanye kazi kwa uhuru bila kuingiliwa na raisi. Hayo yanawezekana kama katiba itakuwa customized.

Kunakuwa na chombo ambacho kiko tied na funded na wananchi ili kuhakikisha hio mifumo na katiba haziwi compromised na yeyote na kama itatokea basi kinavunjwa na kuundwa kipya chenye watu wengine wapya huku walioharibu wakielekea moja kwa moja jela.
 
Huo ndio ukweli na ukiona kiongozi anaogopa jua nae ni mnufaika mkuu wa mfumo uliopo
 
Mfumo imara hutegemea wananchi imara wenye kujua sheria na taratibu za nchi zao na hasa haki zao za msingi na iwapo sheria, taratibu na haki zao katika nchi zikivunjwa au kuminywa hujua hatua stahiki inayopaswa kuchukuliwa.
Zimejaa maiti kisemeo cha jomo kenyata
 
Subiri arudi yesu kwa nchi labda
 
Kama ntakuwa nimemuelewa, anasema hivi mfumo si chochote Bali mtu ndo kila kitu, so tz bila mwendakuzimu mambo hayaendi, kama tunataka yaende, basi samia aachie ngazi kijiti akamate sabaya au makonda, au kikosi kazi cha kuteka na kuua.
Mfumu imara huanza na wewe katika taasisi unayoifanyia kazi...je unafuata sheria katika kitengo ulichopo? Na km haufuati na hauwajibishwi kuna haja ya kuwa na sheria,kanuni na miongozo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…