KERO Mfumo wa Ajira Portal unatutesa, mamlaka husika ifanyie kazi changamoto hii

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma iangalie vizuri mfumo wa Ajira Portal unatutesa tunashindwa kutuma maombi, kila ukijaza taarifa hazifiki asilimia 70 na pia hakuna mfumo wa kubadili vyeti ulivyoviweka ili kuweka vingine.

Sijui inakuwaje na ajira zote zinatumwa huko.

Habari, niawasilisho juu ya changamoto ya mfumo wa ajira portal. Mfumo unaotumika kuombea ajira kielectroniki.

Changamoto ya kwanza ni mfumo kua mgumu Kwa wa tahini wa wengi. Hivyo kupelekea ugumu wakati wakuingiza taarifa na hata kukosea kutokana na baadhi ya taarifa za chuo na mwanafunzi kutokuwekwa kwenye mfumo. Mfano baadhi ya chuo havipo na instap vyeti na Mafunzo, pia baadhi ya taarifa zikiingizwa kwenye mfumo huwezi zifuta hivyo kufanya wanafunzi wengi kuzikosa fursa kutokana na ugumu huo.

Ombi langu Kwa wanaohusika, kuzitambua changamoto zote, kuzishughulikia baada ya kuzipokea, pia na lugha nzuri haswa kwa wote watakao hitaji kusaidiwa, na la mwisho eneo la upakiaji wa Cheti lipa te nafasi ya kufuta Cheti endapo umekosea kuingiza taarifa zako binafsi ili kuwezesha waombaji wa nafasi za kazi tofauti tofauti kuombea nakutopitwa na fursa hizo. Nawasilisha
 
Attachments

  • a8ba825a40ebfeb27f1abdf75ab126db.png
    a8ba825a40ebfeb27f1abdf75ab126db.png
    68.7 KB · Views: 35
Watu wameenda kufanya mamitihani mara kibao kilasiku nikutumatu taarifa. Huo mfumo bora simu ndogo tecno ukirudia kuingiza namba ya simu tecno inatambua
 
Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma iangalie vizuri mfumo wa Ajira Portal unatutesa tunashindwa kutuma maombi, kila ukijaza taarifa hazifiki asilimia 70 na pia hakuna mfumo wa kubadili vyeti ulivyoviweka ili kuweka vingine.

Sijui inakuwaje na ajira zote zinatumwa huko.
Huu ni ulalamishi au kero isiyokuwa na maana yoyote. Huo mfumo hauna shida yoyote kwa upande wa kujaza taarifa labda mhusika ndiye mwenye shida.

Mhusika ajaze taarifa zake zinazohitajika kuanzia taarifa zake binafsi na viambata vyake, picha hadi uzoefu wa kazi kama anao aone kama hazifiki. Kinachotofautisha asilimia kati ya mhusika mmoja na mwingine ni zile sehemu ambazo mmoja hana cha kujaza na mwenzake anazo. Mfano asilimia ya asiye na experience ya kazi haiwezi kuwa sawa na mwenye experience sababu asiye na experience hana cha kujaza. Vilevile anayejaza sehemu ya professional qualifications, e.g. madaktari, wafamasia, wenye CPA, n.k. haiwezi kuwa sawa na anayejaza sehemu ya academic qualifications tu.

Kuhusu kubadili vyeti hilo nalo ni tatizo la mtoa kero sababu mfumo unaruhusu kuhariri (edit) taarifa zake na kuweka attachment upya. Kama hajui ni suala la kuomba usaidizi wa nini cha kufanya badala ya kulalamika. Zaidi kumewekwa mwongozo wa namna ya kujaza taarifa na namba za kuwasiliana nao pale unapokumbana na changamoto, wanapokea na kutoa usaidizi wakati wa masaa ya kazi.

Nayasema haya sababu nimekutana na vijana wenye malalamiko kama ya aliyetoa kero na walifanikiwa kukamilisha maombi yao bila shida yoyote. Kilichokuwa kinawafanya washindwe kufanikisha ni wao kwenda kwenye internet cafes na maduka ya stationaries na kuacha wafanyiwe maombi na waendesha hizo cafes badala ya kufanya wenyewe huku wakilipa hela kila wakienda.
 
Wizara inayohusika na mfumo wa ajira potal hebu isikie kero za watu juu ya huo mfumo, imekuwa shida kubwa sana kutuma maombi ya kazi kupitia mfumo huo maana huwezi kutuma maombi mpaka ufike asilimia 70% kila ukijaza hazifiki lakini pia huwezi kuondoa vyeti ulivyoviweka kuweka vyengine pia huwezi kufuta account ni shida tu.
 
Huu ni ulalamishi au kero isiyokuwa na maana yoyote. Huo mfumo hauna shida yoyote kwa upande wa kujaza taarifa labda mhusika ndiye mwenye shida.

Mhusika ajaze taarifa zake zinazohitajika kuanzia taarifa zake binafsi na viambata vyake, picha hadi uzoefu wa kazi kama anao aone kama hazifiki. Kinachotofautisha asilimia kati ya mhusika mmoja na mwingine ni zile sehemu ambazo mmoja hana cha kujaza na mwenzake anazo. Mfano asilimia ya asiye na experience ya kazi haiwezi kuwa sawa na mwenye experience sababu asiye na experience hana cha kujaza. Vilevile anayejaza sehemu ya professional qualifications, e.g. madaktari, wafamasia, wenye CPA, n.k. haiwezi kuwa sawa na anayejaza sehemu ya academic qualifications tu.

Kuhusu kubadili vyeti hilo nalo ni tatizo la mtoa kero sababu mfumo unaruhusu kuhariri (edit) taarifa zake na kuweka attachment upya. Kama hajui ni suala la kuomba usaidizi wa nini cha kufanya badala ya kulalamika. Zaidi kumewekwa mwongozo wa namna ya kujaza taarifa na namba za kuwasiliana nao pale unapokumbana na changamoto, wanapokea na kutoa usaidizi wakati wa masaa ya kazi.

Nayasema haya sababu nimekutana na vijana wenye malalamiko kama ya aliyetoa kero na walifanikiwa kukamilisha maombi yao bila shida yoyote. Kilichokuwa kinawafanya washindwe kufanikisha ni wao kwenda kwenye internet cafes na maduka ya stationaries na kuacha wafanyiwe maombi na waendesha hizo cafes badala ya kufanya wenyewe huku wakilipa hela kila wakienda.
Ww unaweza nikupe hy kazi ufanye halafu uone km inawezekana? Shida sio kuedit taarifa nataka kuondoa kabisa hicho kisiwepo wewe unaweza maana ukiona mtu anasema ujue amejaribu
 
Wakuu account yangu ipo inactive nafanyaje msaada please
 
mimi nina 100 percent ila inanigomea ku apply inaandika APPLICATION FAILED na nina kila kitu.
 
Labda wewe ni mgeni mkuu! Lakini ukiweka nida vizuri na paspotsize na kujaza hizo nafasi unafika 80% fasta, huo mfumo umeandaliwa kama Maandalizi ya Cv sasa unataka utume maombi cv yako haijakamilika??? Haraka ya nini mkuu?? Kwa sisi wazoefu kuijaza hiyo ni ndani ya dakika tano tu umefika 90% ! Kuwa mpole
 
Back
Top Bottom