KERO Mfumo wa Ajira Portal unatutesa, mamlaka husika ifanyie kazi changamoto hii

KERO Mfumo wa Ajira Portal unatutesa, mamlaka husika ifanyie kazi changamoto hii

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Wakuu, nahitaji nimsajili mdogo wangu ajira portal. Sasa kila nikitaka kufanya kwa simu nikiweka email inaandika email exist hivyo inagoma kuendelea na mchakato,vp nitengeneze email mpya au huu mchakato ni mpaka kutumia computer?
Tumia PC mkuu. Kwny cmu utahangaika sana.
 
Akiajiriwa kwa diploma atakaa mwak Mmoja athibitishwe kazini Kisha anawasilisha Ile degree kwa mwajiri Ili Ku upgrade
Kumbe ni hivyo, basi afanye

Je, mwajiri atakapomwambia kuwa tulihitaji mwenye Diploma na wakakataa kupokea hivyo vyeti vya Degree ili wamu upgrade, atakuwa sahihi kumlaumu mwajiri?
 
Kutokana na ujuzi mdogo nilionao, napenda kutoa malalamiko juu ya mfumo wa kuomba ajira za pamoja.
mfumo huu umekaa kibaguzi na haujakamiliki kwa kutumika, nasema hivi kwasababu zifuatazo
  1. Mwombaji mwenye taaluma zaidi ya moja haumtambui taaluma zake zote. mf. mtu kasomea diploma ya Education na degree ya Civil Engineering. hapo awali alijisajiri kupitia taaluma ya civil, lakini alipoongezea education, bado kazi za Education hawezi kuomba japo anavigezo(Mfumo kama huu ni mbovu katika ubora wa mifumo ya kuringanisha sifa za muombaji)
  2. Sehemu ya taaluma huwezi kuedit hata kama umekosea kutuma, kwa namna hiyo mfumo haumpi nafasi muombaji kuediti taalifa za taaluma pale anapokosea mwanzo
  3. Matokeo ya usahili wa mitihani upo kificho, kwa sababu matokeo hayawekwi wazikwa msailiwa aliyechaguliwa na asiyechaguliwa kuwa amepata alama ngapi na aliyechaguliwa kapata ngapi. kama mfumo huu ndio utaendelea katika kuajiri . ni janga kwa wasomi wengi. asilimia kubwa ya wasomi tanzania tuna taaluma zaidi ya moja.
 
Habari, niawasilisho juu ya changamoto ya mfumo wa ajira portal. Mfumo unaotumika kuombea ajira kielectroniki.

Changamoto ya kwanza ni mfumo kua mgumu Kwa wa tahini wa wengi. Hivyo kupelekea ugumu wakati wakuingiza taarifa na hata kukosea kutokana na baadhi ya taarifa za chuo na mwanafunzi kutokuwekwa kwenye mfumo. Mfano baadhi ya chuo havipo na instap vyeti na Mafunzo, pia baadhi ya taarifa zikiingizwa kwenye mfumo huwezi zifuta hivyo kufanya wanafunzi wengi kuzikosa fursa kutokana na ugumu huo.

Ombi langu Kwa wanaohusika, kuzitambua changamoto zote, kuzishughulikia baada ya kuzipokea, pia na lugha nzuri haswa kwa wote watakao hitaji kusaidiwa, na la mwisho eneo la upakiaji wa Cheti lipa te nafasi ya kufuta Cheti endapo umekosea kuingiza taarifa zako binafsi ili kuwezesha waombaji wa nafasi za kazi tofauti tofauti kuombea nakutopitwa na fursa hizo. Nawasilisha
 
Sio kwelii ipo friendly saana unawezaa kuedit vizurii tuu na kubadilisha chetii kitu ambacho huwezii kubadilisha ni Level yako ya elimu ukiweka huwezii kufutaa mpaka uwasiliane nao
Mkuu, cheti hakibadiliki kabisa yani. Hata mimi nina same problem, nataka nireplace vya zamani OG na hivi vya sasa ambavyo nimeUpdate. Yani ukimaliza kwenye kuView unakuta hamna badiliko IT'S SO FRUSTRATING
 
Anachokisema ni kweli. Huwezi kubadilisha documents .....ni shida ...kwa mfno mimi mwaka juzi niliweka vyeti ambavyo havikuwq verified kwa mwanasheria, Mwaka huu nimeverify sasa nataka nitoe vile vyet ambavyo havijakuwq verified haiwezekani kbs . Ni shidq
 
HUU MFUMO UMEFELI NA MBAYA ZAIDI WAHUSIKA NI WATANZANIA NA WANAPITA HUKU KWENYE MITANDAO NA WANAONA HAYA MALALAMIKO ACHILIA MBALI TUMEWATUMIA EMAILS NYINGI NA SIMU HAZIPOKELEWI, KWAHIYO WANAFANYA MAKUSUDI. CCM OYEEE
 
Nina changamoto kama yako na nikipiga simu hawapokei wapo busy sana hadi nashindwa nifanyeje...msaada pleasee
Simu zao zinachukua MDA kupokea ni kupiga mara Kwa mara na kuwa mvumilivu, Mimi niliwapigia ilichukua kama DK 5 Ila walipokea, kuna jamaa nae aliwapigia ilichelewa lakin walipokea, chamsingi ni kuwa mpole tu, alafu tumia zile namba za kiofisi walioweka pale Ile unaanza+26 Yan sio ya mitandao hii voda, TG, nk tupunguze lawama sometimes
 
Back
Top Bottom