KERO Mfumo wa DAWASA wa kuomba kuunganishiwa Maji ONLINE haufanyi kazi

KERO Mfumo wa DAWASA wa kuomba kuunganishiwa Maji ONLINE haufanyi kazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mongason

New Member
Joined
Aug 19, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Sehemu ninayokaa hamna bomba kuna mtu wa nyumba ya pili alikuwa amevuta maji akawa anatuuzia maji ila baadaye akaja kuzuliwa na DAWASA DAWASA kuwa hana kibali cha kuuza maji lakini pia sisi sehemu tulipo tupo ndani ya mita 50 kutoka bomba kubwa hivyo tunatakiwa kuvuta maji yule mtu akakatiwa maji.

Baada ya hapo nikaanza process za kuomba maji baada ya kufuatilia nikaambiwa kuna njia mbili either uende ofsin kwao na documents au wanao mfumo (online system) kwahyo siyo lazima uende ofsini.

Kutokana na kazi yangu natoka na kurudi usiku nikaona ni vyema nifanye online application nikafanya process zote nikamaliza nikatumia confirmation email na application namba kwaajili ya kujua status ya maombi yangu cha kushangaza toka nifanye application ni miezi 3 sasa sijawai kujibiwa tena chochote na pia kila nikiangalia kwenye system kupitia application namba naambia tu OMBI LAKO LIMEPOKELEWA KWA HATUA ZA AWALI.

Nilijaribu kutafta majibu nikaingia instagram wameweka namba yao ya WhatsApp kwaajili ya wateja kila nikituma sms hazijawai kujibiwa.

Haikutosha nikapiga huduma kwa wateja kupitia namba 180 yule dada aliyenipokelea kuna kitu alichoongea hapo ndipo nikajua mfumo wao wa online haufanyi kazi nanukuu "Kaka kama kweli upo serious unagaka maji nakushauri tembelea ofsi iliyopo karibu na wewe"

Sasa hivi tunalazimika kwenda kuchota maji nyumba za jirani mda ambao ni jioni au usiku au asubh sana kwa sasa huyu anayetuuzia sasa hivi naye anaogopa kufungiwa.

Pia kama mfumo wao wa online haufanyi kazi ni vyema waseme tujue.

View attachment 3656203
View attachment 3656204
 
Back
Top Bottom