Sababu ni mtazamo wa kifalsafa kuhusu siku inaanza wakati gani na kwa sababu gani?Sijui kama ilishawahi kujadiliwa humu lakini nimekuwa najiuliza sana na kukosa majibu, kwanini mfumo wa masaa wa Afrika Mashariki upo tofauti na sehemu zingine duniani? Sehemu zote siku inaanza saa 6 (0000) usiku lakini kwetu inaanza saa 1 (0700) asubuhi. Kuna sababu ya hii tofauti mahali?
Na tulipatia wapi huu mfumo na kwa nini? Tujiulize wanabodi na tunafaidika nini au tunapata hasara gani kwa hii? Karibuni kwa tafakuri.
Kwa falsafa za kizungu siku uanza midnight sijui ndio "usiku wa manane"!!!
Kwa falsafa za kiafrika siku inaanza kwa mwonekano wa jua ndio maana hiyo 7:00 a.m tunasema saa 1 maana yake ni saa 1 tokea jua limeonekana, tokea siku imeanza.
Wenzetu wanavyosema 7 o'clock wanamaanisha masaa 7 tokea siku imeanza!
Tatizo ya falsafa yetu ni kwamba pamoja na kusema saa 1 lkn bado tunaandika 7! Kwanini kama ni saa 1 mshale wa saa usionyeshe hiyo 1! Tunaonekana wajinga unaona 7 lkn unasema saa 1!!!!!!