Mfumo wa masaa Afrika Mashariki

Mfumo wa masaa Afrika Mashariki

Sio kwel bhn hata cc siku inazia iyo iyo saa 6 kamili siku
Kwa saa zetu siku inaanza asubuhi saa 1 asubuhi...wazungu wao siku inaanza saa 6 usiku ndiyo saa 1 inaingia sababu za wazungu kuchagua muda huo ni za kula bata na kiuchumi watu wanashinda sehemu za starehe wakitumia pesa usiku wakisubiri huo muda...hivyo wale wa saa 6 usiku wametupiga bao kwenye sababu.... kuu mbili za kiuchumi na kistarehe...kuhusu kidini siku inabadilika saa 12 jioni ndiyo inaingia siku mpya .....ila kimantiki sisi africa mashariki ndiyo tumechagua muda sahihi zaidi wa siku kuanza asubuhi japo kiuchumi na kistarehe tume feli...mfano kama mwaka mpya utaingia asubuhi mashamshamu yake hayawezi kunoga kama usiku pia kiuchumi inakuwa chini mikesha ya mwaka mpya inabusti matumizi ya pesa na anasa.
 
Sijui kama ilishawahi kujadiliwa humu lakini nimekuwa najiuliza sana na kukosa majibu, kwanini mfumo wa masaa wa Afrika Mashariki upo tofauti na sehemu zingine duniani? Sehemu zote siku inaanza saa 6 (0000) usiku lakini kwetu inaanza saa 1 (0700) asubuhi. Kuna sababu ya hii tofauti mahali?

Na tulipatia wapi huu mfumo na kwa nini? Tujiulize wanabodi na tunafaidika nini au tunapata hasara gani kwa hii? Karibuni kwa tafakuri.
Culture
 
Inaleta maana sana ila kama tunaanza siku jua likichomoza kwa nini siku inabadilika jina usiku wa manane?
Kiutamaduni, siku huanza asubuhi na kuisha jioni, usiku siyo siku bali ni muda wa kulala (ndiyo maana tunasema, siku imeisha, yaani baada ya hapo hakuna siku mpaka kukuche).

Hiyo ya kuanzia saa 0:00 tuliongeza maana tuu ili tuendane na wengine., haiko kiasili (yaani mgongano wa tamaduni) na ndiyo sababu ya hii mada kuletwa.
 
Kuendana na wengine inaleta maana sana, so tuna mifumo yote wetu wa asili na wa kuendana na mataifa mengine
 
Ila pia ungeuliza,kwann Ulaya ukifika mwezi November Kama hii,hurudisha saa moja nyuma halafu huku kwetu hatufanyi?
Yaani kwa mfano saa kumi na moja ya mwezi April mpaka octoba ukifika November mpaka machi katikati hubadilika na kuwa saa kumi na mbili???
 
Kweli kabisa kwa mfano Marekani usiku huu tunarusha muda nyuma wa lisaa, hiyo inaeleweka "daylight saving time" na imewekwa kisheria na kuna sababu but nimetaka kujua tu kuhusu kwetu na kama kuna reference zozote kiongozi
 
Reference Sina Ila pitia post #12 na #30 jamaa wamejitahidi kwa upande wao kukujibu.
 
Back
Top Bottom