DOKEZO Mfumo wa Mtandao kuomba uhamisho Serikalini ni tatizo, unatakiwa kuboreshwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kuna changamoto ya Mfumo wa Employee Self Service (ESS), Watumishi wa Serikali tunateseka.

Nimeanza kutumia Mfumo kwa ajili ya kuomba Uhamisho wa kuhama kutoka ‘Taasisi A’ kwenda ‘Taasisi B’ kwa takribani miezi sita sasa tangu kuanza kwa Mfumo huo rasmi bila ya mafanikio huku nikikumbana na changamoto zifuatazo:

1. Mfumo unaonekana hautambui Professional za Watu (Sifa za Kielemu), badala yake unatambua Vyeo tu vya Kimuundo kwa Taasisi husika.

Hali hiyo inaleta ugumu kwa Watu wenye sifa za Kielemu kuingia kutumia Mfumo kuomba uhamisho kutoka Taasisi moja kwenda nyingine ambako pia sifa za Kielemu anazo za kufanyakazi Taasisi anayotaka kwenda.

Kwenye kipengele hiki Mtumishi akiingia kwa ajili ya kuanzisha maomba tu kwenye Mfumo katika zile menu zinazohusu Uhamisho Mfano:

i. Request Vacancy

ii. Transfer Request zinamletea message inayosomeka: "Designation not found on Destination Organization"

Hivyo, inatuwia vigumu Watumishi kuhama kwenda kutafuta changamoto nyingine nje ya taasisi tulizopo, pia kuongeza hali na kuufanya ubongo uchangamke zaidi na kujifuza vitu vipya.

View attachment 2951237
Huu ni mfano ninapokuwa nafanya mchakato wa uhamisho
2. Baadhi ya Watumishi imeonekana wakifuatilia mara kwa mara katika Ofisi za Utumishi bila ya Mafanikio.

Ombi letu ni waweze kutatua Mfumo kuwa imara kama ilivyo kwa matumizi mengine ya kimfumo, vinginevyo itakuwa haina maana kwa hiki walichofanya kuhamishia shughuli katika njia ya Mtandao.

Kingine mfumo unatambua elimu uliyoingia nayo tu wakati taarifa zako zinaingizwa, ukijiendeleza ukataka kuboresha taarifa za ziada hilo haliwezekani, mfumo unakataa.

Malalamiko yalikuwa mengi wakati mfumo wa analojia ulipokuwa unatumia, sasa hii solution nayo imekuwa ni sehemu ya tatizo.

Kuna baadhi ya nafasi ukiomba kwa ajili ya uhamisho unajibiwa “Vacancy is not Available” yaani hakuna nafasi, hata uombe kwenye taasisi ambayo unajua ina uhaba wa Watumishi majibu yatakuwa ni hayohayo.

Just imagine Mwalim au nurse anaambiwa Vacancy is not available? Ni wapi huko ambako hakuna mahitaji ya hao Watumishi.

Pia soma:
Ni hujuma tu zinafanyika, mbona kwa wanafunzi wako faster kwa nini watumishi?

Wanazingua sana! Yaani ni bora warudishe mfumo wa makaratasi basi. Huu ni unyanyasaji.
 
Vipi ulishafanikiwa kuhama?
 
Jamani naomben msaada nimefika hatua ya kuandoka transfer request lakini Kila nokituma ombi inaniandikia error initiating transfer request msaada please
 
Attachments

  • Screenshot_20241219-180236.png
    Screenshot_20241219-180236.png
    99 KB · Views: 7
  • Screenshot_20241219-180220.png
    Screenshot_20241219-180220.png
    97.5 KB · Views: 8
Back
Top Bottom