Mfumo wa mwendokasi unakata fedha mara mbili kwenye kituo kimoja kimakosa

Mfumo wa mwendokasi unakata fedha mara mbili kwenye kituo kimoja kimakosa

Mstahiki Mea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
6,559
Reaction score
12,518
Kuna changamoto kwenye kituo cha mwendokasi ambapo wakati wa ku scan inatoa notification haijafanikiwa ukirudia ku scan ikikubali wanakata fedha mara mbili. Leo nilikuwa naelekea kivukoni sasa nikaweka tsh 2000 ambapo cashier amedhibitisha hela iliwekwa kwenye card ,, sasa wakati nimeenda ku scan ili nipite ikagoma na kuandika haijafanikiwa. Nikarudia ku scan ikakubali nikaendelea nasafari muda wakurudi nikakuta salio ni 00. ikabidi niweke fedha nyingine niliporudi kwenye kituo husika ambapo nilipandia akacheki kwenye mfumo akakuta fedha ilikatwa mara mbili na hakuna utaratibu wakurejesha. Hii ni changamoto inayotakiwa kushughulikiwa kwa haraka. Kwa kuweka mifumo sawa na hata kama ni hitilafu ya muda mfupi kuwe na uwezo wa mifumo ya uendeshaji kutambua matukio yasiyo ya kawaida. Asanteni .
 
Back
Top Bottom