Mfumo wa udahili wa mwaka 2025/26 na majibu yaliyotangazwa jana umekuwa kandamizi na unaumiza wanafunzi pamoja na wazazi. Wanafunzi wanapochaguliwa mara mbili au zaidi, wakijaribu kufanya confirmation kwenye chuo na programu wanayoitamani, wanapokea ujumbe “program imejaa”. Hii inakuwa kama kulazimishwa kusoma vyuo na kozi zisizo chaguo la mwanafunzi.
TCU mnakwenda mbali sana kuingilia maamuzi ya wazazi na wanafunzi. Kazi yenu ni kuratibu udahili, siyo kutulazimisha wapi watoto wetu wasome. Mzazi ndiye analipa ada na kugharamia masomo, kwa hiyo mzazi na mwanafunzi ndio wanapaswa kuamua chuo na programu sahihi kwa ajili ya maisha na ndoto zao.
Marehemu Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliwahi kusisitiza wazi kwamba kila mwanafunzi apewe uhuru wa kuchagua chuo anachotaka. Kwa hali hii ya sasa, inaonekana mfumo unapingana na maelekezo hayo.
Tunawaomba Waziri husika na mamlaka zote za elimu kuingilia kati. Wanafunzi wetu wasilazimishwe kwenda vyuo au kusoma programu ambazo hawazipendi. Hii sio haki na inaleta mateso kwa familia na vijana.
Tunataka haki ya kuchagua chuo na programu izingatiwe, bila visingizio vya “program imejaa”.