Mfumo wa Udahili wa Mwaka 2025/26 Umekuwa Kandamizi: TCU Acheni Watu Waamue Wanaenda Wapi

Mfumo wa Udahili wa Mwaka 2025/26 Umekuwa Kandamizi: TCU Acheni Watu Waamue Wanaenda Wapi

TCU analazimishaje watu kusoma program ambazo hawazitaki? Kwanini waliziweka kwenye list wakati wa application? Yan kitu unapaswa kuepuka ni kujaza program kukamilisha idadi, unaweza kujaza course kimasiara sana na ukapata hiyohiyo tu. Husipokuwa makini huendi chuo mwaka huo.
 
Mdau anachosema ni ukweli. Mimi nina mdogo wangu aliyeomba vyuo viwili na amekubaliwa vyote. Tulipojaribu kuthibitisha programu ambayo tumekubaliana asome, mfumo ukaonyesha program full. Tulipopiga simu chuoni, wakasema uwezo (capacity) umejaa na kwamba suala hilo liko nje ya uwezo wao kwa sababu mfumo umeunganishwa na TCU na wao ndio wanaofunga.

Najiuliza, je, TCU inalazimisha watu wasome programu ambazo hawazitaki? Au kama ni suala la capacity, wamefanya nini kusaidia vyuo kuongeza uwezo huo? Au wamebaki kuwa walinzi wakali tu?

Haya mambo ya capacity tulizoea zaidi kwenye kada za afya, sawa na inaeleweka. Lakini sasa kuingiza mfumo huu hadi kwenye fani za kawaida hakutendi haki. TCU inapaswa kuwawezesha vyuo, siyo kuvizuia kana kwamba wao ni walinzi tu badala ya facilitators.
Kama moja imejaa, si anachagua nyingine ambazo zote aliomba yeye mwenyewe
 
Nimechagua course ya akwaida ya mawasiliano ya umma na sio mimi tuko wengi confermation zimeanza jana jana hiyo hiyo the same time tunaambiwa course imeajaa kuna nini hapo? Pia mtu anapaswa kua huru kuchagua anapo enda tunapiga vyuoni tunaambiwa wao nao hawajui mifumo imekua intergrated na TCU na hawana namna sasa nikama TCU wanaforce.
Msomi huyo anakuambia confermation . Usiseme typing error hili neno umelirudia mara nyingi! 🤣🤣🤣🤣
 
Moja imejaa, nenda kathibitisbe nyingine uliyochaguliwa ambayo nayo uliichagua wewe mwenyewe

Au zote ukithibitidha zinakataa?

Ukiendelea kulalamika humu utakuta hata hizo zingine ulizochaguliwa nazo zimejaa
 
Mfumo wa udahili wa mwaka 2025/26 na majibu yaliyotangazwa jana umekuwa kandamizi na unaumiza wanafunzi pamoja na wazazi. Wanafunzi wanapochaguliwa mara mbili au zaidi, wakijaribu kufanya confirmation kwenye chuo na programu wanayoitamani, wanapokea ujumbe “program imejaa”. Hii inakuwa kama kulazimishwa kusoma vyuo na kozi zisizo chaguo la mwanafunzi.

TCU mnakwenda mbali sana kuingilia maamuzi ya wazazi na wanafunzi. Kazi yenu ni kuratibu udahili, siyo kutulazimisha wapi watoto wetu wasome. Mzazi ndiye analipa ada na kugharamia masomo, kwa hiyo mzazi na mwanafunzi ndio wanapaswa kuamua chuo na programu sahihi kwa ajili ya maisha na ndoto zao.
View attachment 3465099

Marehemu Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliwahi kusisitiza wazi kwamba kila mwanafunzi apewe uhuru wa kuchagua chuo anachotaka. Kwa hali hii ya sasa, inaonekana mfumo unapingana na maelekezo hayo.


Tunawaomba Waziri husika na mamlaka zote za elimu kuingilia kati. Wanafunzi wetu wasilazimishwe kwenda vyuo au kusoma programu ambazo hawazipendi. Hii sio haki na inaleta mateso kwa familia na vijana.

Tunataka haki ya kuchagua chuo na programu izingatiwe, bila visingizio vya “program imejaa”.
Rushwa na biashara ya vyuo
 
Tatizo wanafunzi hamueleweki. Jana mtu mmoja alileta hoja kwamba kozi ya insurance and risk management ina watu wengi kama 513 hivi hivyo mamlaka husika zipunguze wanafunzi wabaki 30, alafu wengine wapelekwe kusomea uhasibu na ugavi

Wewe leo unaleta hoja, hutaki mamlaka husika zisimamie idadi ya wanafunzi kwenye kozi fulani. Yani mpewe uhuru wa kuchagua bila kujali uwezo ya kuhudumiwa.

Hizi moja mbili tofauti zinakinzana. Swali; je tukusikilize wewe unayetaka uhuru au tumsikilize huyo jamaa mwingine anayetaka udhibiti wa wanafunzi?
 
Back
Top Bottom