Battor
JF-Expert Member
- Mar 21, 2019
- 1,964
- 3,496
Wao wananunuliwa hadi barakoa, unadhani watakuelewa ukisema maisha ya mtanzania yamezidi kuwa magumu.Hali mtaani inatisha sana, karibu kila kitu kimepanda bei, kuanzia maduka ya ujenzi hadi maduka ya vyakula, hadi pipi zimepanda bei.
Kipato cha Mtanzania kiko palepale na asilimia kubwa ya vijana hawana ajira wala kipato chochote.
Sahivi ukininunua mafuta ya elfu moja ya kupikia hayatoshi kabisa kwenye mboga. Na baadhi ya maduka ya mitaani yameaacha kabisa kuuza mafuta reja reja kutokana na madai kuwa wanashindwa wauzeje kwani wateja wao Wamekuwa wakilalamika kuwa kupunjwa na Kuona kuwa wanaibiwa.
Kwenye kilimo huko wakulima wanalalamika jua limekuwa kali hakuna mvua wala mavuno, huku pembejeo zikiwa hazikamatiki kwa bei.
Kwa ujumla hali ni tete tena sanana wananchi wamekuwa wapole kupita kiasi.
Viongozi wetu wametulia tulii kama hakuna wanachojua wala kuona vile,
Kwa serikali inayojali wananchi wake tayari wangeshafanya namna yoyote iwayo kama vile kupunguza kodi kwa bidhaa zote, na haswa upande wa kodi ya mafuta na vipuri vya magari bandarini.
Kwa vile serikali yetu haipendi kukosolewa wala kunyooshewa kidole basi wananchi tutaendelea kutaabika tu.
Lakini kiukweli hali mtaani sio nzuri kwa Mwananchi wa kawaida
Unafiki na mipasho ndo vitu wanavyojua wao.