Mfumuko huu wa bei nchini, Watanzania tumekuwa wapole mno. Tunahitaji maandamano ya amani

Kazi kulalamika mitandaoni tu...mkiambia tuandamane mna fyanta mkia misili ya mbwa koko. Tuendelee hivi hivi tu maana Mkiambia SERIKALI YA CCM NI YA KIDIKTETA hamuamini
 
Af hii Ni kelele Kama kelele zingine tu. Nchi hii Ni ya Hovyo kabisa katika kumjali mtu wa Hali ya chini kabisa yaan anaeshi kwa dola moja. Na toka kipindi Cha kampeni za urais Hadi uchafuzi mkuu wa 2020 nimewasikiliza Sana wagombea, Hakika nchi hii ya Tanzania inahitaji mtu Kama TUNDU LISSU awe rais ingawa katika Sera zake zote moja tu ndio mbaya kidogo nayo Ni Sera ya MAJIMBO. Ila note kwa yote TUNDU LISSU anastahili kuwa rais.
 
Naishi mpakani mwa Tanzania na Zambia (Tunduma) hii nchi inhitaji katiba Kama ya Zambia ambapo kiongozi mkubwa Kama rais anachunguzwa pindi amalizapo mda wake na Kama mambo yameenda ndivyo sivyo anashtakiwa vizuri tu. Na katiba Yao inamsikiliza mno mwananchi wa kawaida na matakwa yake kwa maslahi ya nchi. Nways kuhusu kupanda bei vitu nmalize kwa kusema acha vitu vipande bei tu Maana inasemekana Ni "Acha inyeshe tuone panapo vuja".
 
Wakati huo cheif hangaya anakula bata tuu na ndege zetu.
 
Wananchi wanataka sana katiba mpya
 
Ni sahihi, ni mtanzania mwenyewe ndio anaweza kujikomboa kwenye udhalimu wa hawa tuliowapa mamlaka, shida sisi hatujitambui, wala hatujui tunachokitaka.
 
Lini yalishawahi kufanyika «maandamano ya amani» ya malalamiko dhidi ya serikali? Unaishi kwenye free market economy ambapo Serikali haiwezi kupanga bei ya bidhaa zote hadi peremende na dawa ya mswaki. Labda muandamane kudai Serikali ipandishe mishahara ya Watumishi wake.
 
asili% ya watanzania hawajui haki zao na ndo maana tutaonewa mpaka mwisho wa ccm kuangusha utawala
 
Mbona mchina kaimiliki nchi
 
Bei zimepanda sehemu nyingi duniani
Hata Ulaya ni haya haya na zaidi maana mpaka NI zitapanda April
Gas, Fuel na maji yote bei juu halafu mishahara palepale wataalamu wa fedha wanatuambia wakipandisha mishahara ni mbaya zaidi

Ila wote tunanyooka bali tunatofautiana
 
Dunia sasa inaenda kuwa kitu kingine
 
Leo nimeulizia ndizi za kupika saba saba dom muuzaji ananiambia ndizi tatu buku nimekimbia nikasimamia cbe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…