Mfumuko wa bei huku mtaani unashamiri, kuna nini kinaendelea?

Mfumuko wa bei huku mtaani unashamiri, kuna nini kinaendelea?

Hata deflation humgusa kila mtu.

Usililie deflation ni mbaya sana ndugu yangu, ni ujamaa ule wa kuleta umaskini. Unatakiwa kuchakarika kuikimbiza thamani ya pesa, ongeza uzalishaji wako.

Sikia mtaani pesa ikiwa nyingiiii hakuna bidhaa hiyo ni inflation mbaya sana. Hivyo hivyo kukiwa na bidhaa kila sehemu ila pesa hakuna ni mbaya sana. Pengine mbaya zaidi.

Inatakiwa inflation inavyoongezeka raia wachakarike na uzalishaji ili iwe sawa na uzalishaji na thamani ya pesa nje ya nchi ipande huku serikali ikihakikisha money supply haizidi uzalishaji. Mnakutana kwenye equlibrium.

Mfano , dola moja ss kwetu ni elfu mbili na ushee, ila parachichi unalonunua hapa mia tano marekani atalinunua dola mpaka mia almost laki mbili na ushee. Hiyo ni inflation kwao lakini isiyo na madhara kwenye uchumi wao bali faida.
Asante kwa upembuzi hii.Kwa hiyo inamaanisha hii ni dalili kuwa pesa itarudi kwa wananchi kwa wingi?
 
Huna ulijualo
Toka 2016 nina peleka mchele DRC, na RWANDA, hiyo mipaka iliyofungwa ni ya wapi?kinachotakiwa ni kibali tu toka wizara ya kilimo , labda kama mipaka ya angani , lakini ya barabarani na majini hakuna!!!msiwe mnakurupuka tu, kutaka kuongopea watu humu bila udhibitisho.
 
Salaamu watoto wa Jamhuri ya Muungano!

Kiukweli huku MTAANI vitu vinazidi kupanda bei siku Hadi siku.Nyama saizi 8000 Toka 7000. Juzi nimeenda dukani kununua Colgate naambiwa Sasa ni 5000/= ikiwa hapo awali nilikuwa nanuna 3500/.

Kwa ujumla vitu vingi bei vimepanda na sijaona tamko lolote kutoka mamlaka za serikali kuhusu hili. Je, Kuna inflation inapiga raia kimya kimya na serikali haitaki tamka rasmi?

Wataalamu naombeni uchambuzi ni ni kimesababisha Hali hii ghafla hivi.
Lile kundi wa mashetani alilopiga pin magufuli limerejeshwa na Amirat Jeshi.
 
Toka 2016 nina peleka mchele DRC, na RWANDA, hiyo mipaka iliyofungwa ni ya wapi?kinachotakiwa ni kibali tu toka wizara ya kilimo , labda kama mipaka ya angani , lakini ya barabarani na majini hakuna!!!msiwe mnakurupuka tu, kutaka kuongopea watu humu bila udhibitisho.
Hongera kwa kupereka mchele DRC nenda kahama au misungwi kanunue KILO mia saba mpaka 1200 na bei itaendelea kuporomoka
 
Karanga nilizokuwa nanua kilo moja TZS 2000 sasa hivi ni 3000 mpaka 3500! Unaweza kuwa mkweli mleta mada.

Hivi wale wakulima waliopewa bil 15 wauze mahindi yao, wamefanikiwa kuuza?
 
Huku kwetu tunaendelea kuchakazwa na bei ya mafuta ya kula. Lita 10 ni sh. 50,000/ na Sasa tunaelekea msimu wa kilimo Bei ya mbolea haitabiriki.
 
Hongera kwa kupereka mchele DRC nenda kahama au misungwi kanunue KILO mia saba mpaka 1200 na bei itaendelea kuporomoka
Tatizo hata soko la nje sio mahindi au mchele nalo limevulugika tu , ukiona hapa mazao ni mengi sana hata huko nako bei zinashuka sana!!!
 
Magufuli alidhibiti mazao na mifugo visiuzwe nje ya nchi kwa kufunga mipaka maana mazao yangeadimika, fikiria maisha yangekuwaje?

Japokuwa mkulima alikuwa hanufaiki lakini faida ni kubwa kuliko hasara, maana mahindi mchele mifugo n.k walahi tungetafutana
Ulikuwa uamuzi wa kijinga. Wacha mazao yaendelee kuuzwa nje. Kupanda kwa bei kutachochea uzalishaji. Uzalishaji ukipanda kuweza kutengeneza ziada kubwa, bei zitashuka tena.
 
Sera mbovu za kiuchumi zimeanza kuonyesha matokeo yake. Hali ngumu kama hizi ndiyo huzipa nchi akili.
 
Usisahauhata muda wa maongezi pamoja na bundle za internet nazo ni balaa hali so shawari
 
Uchumi NYOSO na huu ni mwanzo tu hali itazidi kuwa mbaya sana.

Salaamu watoto wa Jamhuri ya Muungano!

Kiukweli huku MTAANI vitu vinazidi kupanda bei siku Hadi siku.Nyama saizi 8000 Toka 7000. Juzi nimeenda dukani kununua Colgate naambiwa Sasa ni 5000/= ikiwa hapo awali nilikuwa nanuna 3500/.

Kwa ujumla vitu vingi bei vimepanda na sijaona tamko lolote kutoka mamlaka za serikali kuhusu hili. Je, Kuna inflation inapiga raia kimya kimya na serikali haitaki tamka rasmi?

Wataalamu naombeni uchambuzi ni ni kimesababisha Hali hii ghafla hivi.
 
12mm tulikuwa tunanunua 17,000 sasa ni 24,500.
Ni hatari sana, na mimi ndo kipindi nilikuwa nafanya ujenzi nondo ilikuwa around elf 18, sementi ya dangote elf 11 material ya finishing ndo hayakamatiki kwa sasa, ngoja niendelee kujikongoja kwenye gofu langu ilimradi umejikinga na mvua na jua.......hapa sasa nimetoka kununua gesi ule mtungi wa mihan nilionunua mara ya mwisho elf 43, leo nimetoa elf 50, tunaenda kutengeneza jangwa hivi karibuni maana watu ambao walikuwa wameanza kutumia gesi wanarudi kwenye mkaa kwa kasi ya 5G, na mimi ni mmoja wao...........
 
Karanga nilizokuwa nanua kilo moja TZS 2000 sasa hivi ni 3000 mpaka 3500! Unaweza kuwa mkweli mleta mada.

Hivi wale wakulima waliopewa bil 15 wauze mahindi yao, wamefanikiwa kuuza?
Hii Ni live bila chenga nanunua karanga 2500-2800 then nauza rejareja 4000 tutaheshimiana tu kwa kweli
 
Back
Top Bottom