Mfunze Mwanao kujiajiri, mwambie maisha hayaanzi akiajiriwa, wasomi wakiwa wengi ajira zinakuwa chache


Naungana na wewe kwenye swala na government bureaucracy, hata mimi nilikutana na hizo challenges wakati nataka kufungua biashara flani, nikabadilisha business model nikafungua biashara tofauti ziinapiga kazi vizuri. Hiyo ndiyo the biggest challenge kwa Tanzania, ila haimaanishi wanakukaba kwa biashara zote, kuna biashara chache ambazo watakusumbua, nyingi mtu unakua free tu kuanza, ni kitendo cha kuregister kampuni yako na kuanza kupiga kazi. Huyo ndugu yako muulize vizuri yaweza kua ni mvivu tu, water purification isn't something complicated kuanzisha company, mimi nilikua nawatuma ndugu kudeal na mambo ya serikali wakawa wanaleta excuse kila siku, nimetoka nje nikaja Tz mwenyewe nikamaliza kila kitu bila usumbufu wowote.

Watu wengi sio risk takers, na vijana wengi wanadharau baadhi ya kazi wakiziona kama zipo chini yao vile.
 
Unafanyaje? nifundishe na mimi nitafute hela
Una skills gani? Hua napenda kuanzia hapo, ukisema uige nachokifanya doesn't mean utaweza kukifanya, nina computer science skills natengeneza app zangu mwenyewe, websites e.t.c. Sio lazima uwe na hizo skills though, ukiwa hata na marketing skills nzuri online kuna kupiga hela sana tu. Hamuoni insta millionaires siku hizi walivyojaa bongo?
 
Sahihi kabisa
 
Kuna kajirani yangu kamoja kapo chuo.
Yaani ukisikiliza maongezi yake tu.
Anajua akimaliza chuo.vup bin vup.anapata kazi.
Hajui wenzie wapowapo tu mtaani.
Akigombana na mtu tu.
Utasikia wewe umefika chukoo🤣🤣🤣 huwa nakacheka sana
 
Hawataki kazi pia
Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Maneno yana nafasi katika mabadiliko.

Sio lazima vitendo,al muhimu wapo waliojiajiri inatosha kuangalia kwao.

Lakini kumbuka kuwa unaambiwa ujiajiri kwa faida yako mwenyewe na sio kwa faida ya anayekuambia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Maneno bila mifano ya vitendo ni kazi bure. Baba yako unamuona kila siku ana vaa shati anaenda ofisini na kurudi jioni anaajura yake safi anakusomesha kwa ajira hiohio nyumbani mnaishi vizuri kwa ajira hiohio unadhani ata akikuambia vipi kuhusu kujiajiri utanwelewa?? Baba huyo huyo anamwambia mwanae akafungue duka auze au afanye biashara online au ajiendeleze na skills flan ili ajiajiri mwenyewe wakati huyo baba ata duka hajawai miliki anasubiria mishahara na maisha fresh unadhani mtoto wake ataelewa chochote?? Huo si unafiki wa waziwazi? Mwanao akikuuliza kama kujiajiri ni rahisi zaidi kwa nini usiache io kazi yako baba ufanye kama unavyosema utanwambia nini??

Tujifunze kwa waindi wale sio wanafiki kabisa anaekwambia ujiajiri unamwona kabisa anajiajiri hivyohivyo nknknk

Wasiwasi wa vijana wengi ni credibillity ya taarifa mnazowapa kuhusu kujiajiri. Wewe hujawai kujiajiri ata siku moja unamwambia mtu ajiajiri sijui ni rahisi sijui atatoboa nk wewe una uhakika gani na taarifa hizo wengi wenu huwa mnaongea kwa kufata mikumbo na kusambaza uongo tu.
Wewe kama muajiriwa ulieajiriwa credible info kutoka kwako iwe kumwelekeza kijana anayetaka kuajiriwa afanye nini na nini ili iwe rahisi kwake kupata ajira na sio kujiajiri waache waliojiajiri wachache ambao ni living proof waseme na vijana kuhusu kujiajiri


Sent using Jamii Forums mobile app
 


Sasa kumbe inahitajika Skills tena? Kumbe elimu bado inahitajika?
nimesoma elimu ya utawala.
 

Mkuu ushauri wako ni mwema nimeupokea na nitakufanyia kazi.
Tatizo hawa watu wanaboa sana na ndio wapo wengi mitaani wanawananga sana vijana ambao hawajabaatika kupata ajira kama vile ni makosa yao kukosa ajira. Kila siku vijana ooh waache kutegemea ajira serikalini hazina tija ooh sijui hazilipi ooh sijui nn ukiwaangalia wao wamekalia izo nafasi miska nenda miaka rudi maofisini uko wanaota tu vitambi. Wanaongea vitu ambavyo hawaviishi wanawaambia vijna wajiajiri biashara zinalipa nk wakati wao kutwa kusubiria mishahara hawajawai kuuza ata vocha.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhalisia 100% tazama jamii zinazokuzunguka.

Mtoto wa mfanya biasha
ra hata akisomea udaktari eventually elimu yake ataielekeza kwenye biashara zaidi.

Huwezi mfundisha mtoto kwa maneno matupu. Mtoto huiga kiurahisi zaidi.

Huyo anaetoka veta akitokea ukoo wa wafanya biashara kuna uwezekano mkubwa akaja kuwaajiri wenzake aliokuwa nao veta wanaotokea ukoo wa waajiriwa.

Mleta mada poyoyo na bado hajayaona maisha kiuhalisia wake.
 
Uhalisia 100© tazama jamii zinazokuzunguka.

Mtoto wa mfanya biasha
ra hata akisomea udaktari eventually elimu yake ataielekeza kwenye biashara zaidi.

Huwezi mfundisha mtoto kwa maneno matupu. Mtoto huiga kiurahisi zaidi.

Huyo anaetoka veta akitokea ukoo wa wafanya biashara kuna uwezekano mkubwa akaja kuwaajiri wenzake aliokuwa nao veta wanaotokea ukoo wa waajiriwa.

Mleta mada poyoyo na bado hajayaona maisha kiuhalisia wake.
 
Sasa kumbe inahitajika Skills tena? Kumbe elimu bado inahitajika?
nimesoma elimu ya utawala.

Biashara yoyote inahitaji skills hasa online business. Uzuri si lazima kila biashara uende kuchukua degree ya biashara ila ni vizuri ujue angalau watu wanafanyeje marketing, wanaanzaje kutengeneza product au kubuild business from scratch. Bila kujifunza itakua ngumu sana kuchomok, biashara 95% hua zinakufa so usishangae kwa nini nakwambia unahitaji skills, hata mi zilifeli nyingi hadi moja ilivyonitoa nikasahau.

Kwa nini usiingie online uongeze skills za biashara, soma entrepreneurship upate basics, kaa ki entrepreneur yaani wakati wote ni kufanya kitu productive. Tafuta TV Show inaitwa Shark Tank uone wafanyabiashara wanavyo-pitch ideas zao kupewa investment uta-gain mengi sana. Kuanza business bila skill yoyote aisee utaishia njiani coz huna strength hata moja atakuja mwingine atakupita
 
Utakuwa raia wa kigeni bila shaka, ila kama ni wale wale wenzangu na mie from "Kithomboko" huwezi niambia kujiajiri ni rahisi namna hio hapa bongo.
Caucasians ama wazawa na watoto wa wazawa walio explore maisha katika 1st world countries ndio wanaziona fursa kirahisi tofauti nasie wa humu humu nchini ndio maana yule binti toka USA aliamua kufungua kijiwe cha kuuza kande kwao huko Mwanza.

Alilifanya direct baada ya kutoka chuo sidhani kama alipoteza muda wa kusaka ajira maana aliiona hela tayari. Sasa jiulize kuna raia wangapi Mwanza ambao ni graduates wa Masters na hawakuwaza hata kupiga kiwi.

Halafu kingine hili swala linachangiwa na koo mtu uliyotokea. Mfano mie Baba mkubwa Professor (Mwajiriwa), Baba Agro-Economist(mwajiriwa) Baba mdogo Lawyer now ila ana foundation ya education ashashika sana chaki, Shangazi mtu wa Social Science ila ana foundation ya education ni mwalimu wa Kilakala girls kitambo, Babu alikuwa mhasibu, babu mzaa babu karani. Katika ukoo shangazi mmoja ndio mfanyabiashara ila wote wametoka katika same route ya kuajiriwa, haya watoto tuliosomeshwa waliozaliwa mapema wengi waajiriwa.

Hivi hio spirit ya kujiajiri naitoa wapi? Ni ngumu sana jamani. Japo hamna namna ni kujikaza tu.
 
Nimezaliwa Tanzania kijijini, nikasoma nikafaulu nikajisomesha mwenyewe, nikaenda kusoma chuo nje nikakomaa fungua bishara kibao zikafeli hadi siku moja moja ikahit. So najua vizuri struggle za maisha nimetokea kwenye umasikini hata 500 kuna muda ilikua shida, hiyo ndiyo ilikua drive ya kunisukuma naona umasikini ni ka ujinga hasa kwa kijana mdogo mwenye nguvu.
 

Ngoja nikimbie haraka sana kama wanavyofanya hawa jamaa kwa Vijana wao.Hakuna kuchelewa..Shule itabki kuwa Shule ila isimfanye Mwanangu apitie nilikopitia Mimi.
Kuna mambo mengi ndani ya Shule na Nje ya Shule.Zubaa uone kinachotokea.
 
Elimu imekuwa rahisi sana nowadays ndo maana kila mtu anasoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…