Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Makubi: Wananchi chukueni tahadhari za kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya magonjwa, msisubiri matamko

Mbona matamko kinyemela!
Serikali ijivue aibu iliyosababisha vifo vingi hivi karibuni.
Ati tumeomba kwa Mungu na Tanzania hakuna covid!

Matamshi kama hayo tayari yameua watu wengi.

Tukubali kuwa inabidi tuwasikilize wataalam wa Afya na madaktari.
Wewe acha ujinga wewe Kama huwasikilizi wataalam wa afya na madaktari shauri yako...watanzania wote tunazingatia miongozo yao..usiendelee kwa punguwani jomba kwa kukosa maarifa
 
Serikali hii ni vurugu tupu. Mollel yeye kachemka vibaya mno huko AZAM TV.

Anasema Nchi ipo salama kabisa, chapeni kazi na eti msiwasikilize hao wanaoongea tu bila kuwa na data kutoka maabara
 
Marekani na nchi za ulaya zote wanachukua tahadhari na bado watu wao wanakufa balaa..sasa ije iwe sisi..tuambie kwanini wanakufa sana licha ya tahadhari hizo
 
Wewe acha ujinga wewe Kama huwasikilizi wataalam wa afya na madaktari shauri yako...watanzania wote tunazingatia miongozo yao..usiendelee kwa punguwani jomba kwa kukosa maarifa
Nyie ndio kwenye mtihani mkiulizwa Lagos iko nchi gani, mnajibu Brazil.
 
mkuu nitajie nchi walochukua tahadhali zote na wapo salama.
Hakuna nchi ya namna hiyo, ila tahadhari inakufanya ujiandae, kwa mfano ujue majani ya kutengeneza nyungu yanapatikana wapi na namna ya kuipiga nyungu, vilevile kama ni limao, tangawizi na vinginevyo viwe karibu.
 
Marekani na nchi za ulaya zote wanachukua tahadhari na bado watu wao wanakufa balaa..sasa ije iwe sisi..tuambie kwanini wanakufa sana licha ya tahadhari hizo
Huoni kwamba wasiochukua tahadhari hali itakuwa mbaya zaidi? Mganga mkuu wa serikali kasema tuchukue tahadhari
 
Marekani na nchi za ulaya zote wanachukua tahadhari na bado watu wao wanakufa balaa..sasa ije iwe sisi..tuambie kwanini wanakufa sana licha ya tahadhari hizo
Jaribu kuufikirisha ubongo wako kwenye side nyingine, fikiria wao wanachukua tahadhari lakini wanakufa vile wewe ambaye uchukui tahadhari utakuaje
 
Hakuna nchi ya namna hiyo, ila tahadhari inakufanya ujiandae, kwa mfano ujue majani ya kutengeneza nyungu yanapatikana wapi na namna ya kuipiga nyungu, vilevile kama ni limao, tangawizi na vinginevyo viwe karibu.
mkuu kwa apo upo sawa sawia usisahau mazoezi
 
Back
Top Bottom