Mgawo mkali wa umeme na maji unaoendelea nchini ni wazi kabisa watendaji wa Serikali mnaihujumu Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan


Sababu ya kwamba kina cha maji kimeshuka imekua ikitolewa kila mara
Kuendelea kutoa hiyo sababu inamaanisha tuna viongozi wasioweza kutatua matatizo na hao hawatufai
 
Kuna umuhimu wa kutocheka na watendaji wa maeneo muhimuq ya Serikali yanayowaagusa waTanzania wengi na walio na vipato hafifu!
Hii mambo ya kutowajibika kunaleta sintofahamu!

Pole pole alisema sana swala la uongozi, uongozi lakini akaonekana mchochezi na kufungwa fhibiti mwendo ya Balozi.

Hii biashara ya teua teua kila mara ni uhuni tu na wateuliwa ni walewale waliostaafu!!
 
Kama ana masikio angesikia huu unumbe. Tuko pamoja nae atumbue tu watu. Alone tutakavyo mpenda.

Ila siku zote wanawake ni wadhaifu; kwa upande mwingine tusimlaumu
 
Maendeleo ya vitu kwa kutesa watu, kutopandisha watu madaraja na mishahara, kupuuza majukumu ya Bunge, kuvunja sheria za nchi ndiyo hatutaki.

Kama tungekuwa hatutaki maendeleo ya vitu si tungekuwa tunavaa matambara mpaka leo badala ya nguo??
Hebu acha upimbi basi. Hivi na wewe unamke na watoto? Mbona unaongea kama team upinde was mvua?!
 
Hakuna kuhujuamiana wala maharage mabovu, TZ hakuna umeme wa kutosha na mitambo imechakaa sana na CCM hawana sera yeyote ya kututoa hapo tulipo, akili za kimaskini zinaongoza Tanzania
 
Wasaidizi ndio wanamhujumu mama...ila mama kama mama anaupiga mwingi
Angeupiga mwingi angeshafukuza wizara ya Nishati, Fedha, Ardhi na Habari na TCRA vinginevyo ni kuendeleza machukizo
 
Nguvu yake ya kulikomboa Taifa hili upo wapi, hadi ahujumiwe?

Ujue hatimizi majukumu yake au hakubaliki.
 
Mabadiliko ya hali ya hewa yamehujumiwa? Hamuoni mabadiliko ya hali ya hewa? Nyie endeleeni kuua vyanzo vya maji afu baadae mkikosa mvua mje mseme mmehujumiwa
 

07 Septemba 2022

Ni kweli kumekuwepo uhaba wa mvua uliojitokeza kwenye maeneo mengi ya nchi yetu kwenye miezi ya hivi karibuni, uhaba huu umesababisha kuwepo kwa upungufu wa kina cha maji kwenye mabwawa ya kufua umeme kwa kutumia maji hivyo kuathiri hali ya uzalishaji wa umeme kwenye baadhi ya vyanzo vinavyotumia maji.

Aidha, ili kuhakikisha kuwa utoaji wa huduma ya umeme inaimarishwa nchini, Shirika limeshachukua hatua mbalimbali za muda mfupi na za muda mrefu kama ifuatavyo;

Mipango ya muda mfupi

[emoji625] Kuanzisha kituo cha kuzalisha umeme kwa njia ya Gesi asilia cha Ubungo III ambacho kimeshakamilika na kuingiza jumla ya Megawati 112 za umeme kwenye Gridi ya Taifa tangu mwanzoni mwa mwaka 2022.

[emoji625]Kuanzisha kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia Gesi asilia cha Kinyerezi I Extension kitakachozalisha jumla ya megawati 185.

Tayari megawati 45 zimeshaingizwa kwenye Gridi ya Taifa na megawati zilizobakia zitaingizwa kwenye Gridi ya Taifa hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka ujao.

[emoji625]Mradi wa kufua umeme wa Rusumo kwa kutumia maji.
Mradi huu unaozihusisha nchi tatu (Tanzania, Rwanda na Burundi) utakapokamilika, unategemewa kufua jumla ya megawati 80 za umeme, ambapo kwa upande wa Tanzania, tutapata megawati 27 za umeme zitakazoingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

[emoji625]Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya jua wa Kishapu, Shinyanga.
Mradi huu unategemewa kuanza ujenzi wake Novemba 2022 na kukamilika Disemba 2023, utaingiza jumla ya megawati 150 za umeme kwenye Gridi ya Taifa.

[emoji625]Mradi wa kupeleka Gridi ya Taifa kwenye wilaya za mkoa wa Kigoma.
Tayari umeme wa Gridi ya Taifa umeshapelekwa kwenye wilaya ya Kibondo.
Serikali imeanza kuokoa jumla ya Tsh.9.44 bilioni kwa mwaka zilizokuwa zikitumika kununulia mafuta ya dizeli na kutengeneza mitambo (jenereta).
Mpango uliopo ni kuufikisha umme wa Gridi ya Taifa kwenye Wilaya ya Kasulu hadi Kigoma mjini kabla ya mwisho wa mwaka huu wa 2022 kufika.

Mipango ya muda mrefu

[emoji625]Mradi wa kufua umeme kwa kutumia maji wa bwawa la Julius Nyerere (JNHPP).

[emoji625]Mradi huu umefikia asilimia 71 ya utekelezaji wake.
Mradi utakapokamilika mnamo mwezi Juni 2024, unategemewa kuingiza megawati 2115 za umeme kwenye Gridi ya Taifa.

[emoji625]Kwa hatua hizi Shirika ilizozichuka zimesaidia kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini na iwapo jitihada hizi zisingechukuliwa, basi ya upatikanaji umeme nchini kwa sasa ingekuwa ipo vibaya zaidi.
 
Ahsante kwa ufafanuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…