imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 55,997
- 88,219
Mvua zilinyesha vizuri mara nyingine zikichelewa kidogo.Miaka mitano iliyopita mvua kubwa zilinyesha miaka yote?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mvua zilinyesha vizuri mara nyingine zikichelewa kidogo.Miaka mitano iliyopita mvua kubwa zilinyesha miaka yote?
Yani tuumie kwa kukosa huduma na kura tutoe?Wameshashindwa kabla hata ya kuanza
Huwezi tafuta cheo kwa gharama ya kumuumiza mwananchi
Jenereta hata enzi za Magufuli zilikuwepo ila watu walizibwa midomo. Hume JF ziko makala za watu wakielezea zama zile kwamba maeneo ya kwao kuna mgao wa umeme.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Haya sawa.Ya Mtwara kuchele
Kina cha maji kimeshuka Ruvu chini na juu, maji yanazalishwa kwa 40% tu, hakuna mvua hii huwezi kuita hujuma.
Issue ya umeme Makamba amewekwa na mama kwahiyo kama ni hujuma basi mama anajihumu mwenyewe, huwezi kuweka wahuni kwenye wizara nyeti kama ya Fedha na ya nishati.
Kuna umuhimu wa kutocheka na watendaji wa maeneo muhimuq ya Serikali yanayowaagusa waTanzania wengi na walio na vipato hafifu!Hiki kinachoendelea kimyakimya ni mchakato wa kuturudisha kuleee miaka ilee ya 2005, 2006, 2007...... miaka ambayo Dar Es Salaam na Tanzania kwa ujumla ilikua imepambwa na mikokoteni ilishosheheni madumu ya korie yaliyobeba maji na magari yenye matank ya maji kila kona.
Kwa kasi ya ajabu tunarudi miaka Ile ambayo mazingira yalikua yamepambwa kwa sauti za majenereta usiku na mchana
Au ndio ule mkakati wa kuutaka urais umeanza!? Acheni mambo yenu buana. Mama Samia yupo sana bado, ndio kwanza kumekucha
Hali ni mbaya sana na hatari kwa afya kwa jiji lenye wakazi wengi zaidi nchini, Dar Es Salaam. Watu tumepona kwenye corona lakini sasa mnataka kutulazimisha tufe kwa kipindupindu
Watendaji mnaohusika kwenye haya maeneo fanyeni kile kilichokua kinafanyika miaka mitano iliyopita hadi tukasahau kabisa kero ya umeme na maji. Kupewa nafasi ya kuhudumia wananchi kwa huduma muhimu kama umeme na maji halafu hao wananchi wakakosa hizo huduma ni wazi kabisa kwamba kufanya imeshindikana. Bora kuiacha office kuliko kukaa kwenye office halafu huduma asipatikane
Tanesco na idara za maji sisi wananchi tunamuamini rais wetu na yeye amewaamini nyie. Mnapopewa dhamana ya kutuhudumia halafu mnaamua kutuhujumu tutapaza sauti kwamba kazi imewashinda. Heri kuteua na kutumbua kuliko wananchi kuteseka kwa kukosa huduma za msingi tena ambazo wanazichangia kwa kodi zao wenyewe
Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu Samia Suluhu Hasan
Kazi iendelee
Cc Wizara ya Afya Tanzania
Atoke tuHujuma dhidi ya Samia zimekuwa nyingi tena ni haohao Wanaccm wenzake wameanza kampeni.
Kama ana masikio angesikia huu unumbe. Tuko pamoja nae atumbue tu watu. Alone tutakavyo mpenda.Hii comment sio ya kupuuza, hii ndio picha wanayopewa watanzania kuhusu serikali yao, na ujumbe uwafikie
#WaziriMwenyeDhamanaYaUmeme
#WaziriMwenyeDhamanaYaMaji
#IdaraZoteZinazohusika
Sisi wananchi tunasema mama yetu Samia anza kuwashughulika wote wanaoshindwa kuhudumia wananchi. Tumbua mama uteue walio tayari kufanya kazi usiku na mchana kuondoa hizi kero ndogondogo kwa wananchi
Hebu acha upimbi basi. Hivi na wewe unamke na watoto? Mbona unaongea kama team upinde was mvua?!Maendeleo ya vitu kwa kutesa watu, kutopandisha watu madaraja na mishahara, kupuuza majukumu ya Bunge, kuvunja sheria za nchi ndiyo hatutaki.
Kama tungekuwa hatutaki maendeleo ya vitu si tungekuwa tunavaa matambara mpaka leo badala ya nguo??
Shetani hana rafikiNashukuru mateso ya ufisadi wa ccm yanawanyoosha hadi wana ccm lialia
Hivi mwigulu hajakamatwa tu ? Maana aliwaongopea WB kuhusu inflation na bado anadunda mtaaniWaziri wa maji na nishati ni akina nani?!
Maan vitu vimepanda bei hadi napoteza kumbukumbu
Angeupiga mwingi angeshafukuza wizara ya Nishati, Fedha, Ardhi na Habari na TCRA vinginevyo ni kuendeleza machukizoWasaidizi ndio wanamhujumu mama...ila mama kama mama anaupiga mwingi
Hiki kinachoendelea kimyakimya ni mchakato wa kuturudisha kuleee miaka ilee ya 2005, 2006, 2007...... miaka ambayo Dar Es Salaam na Tanzania kwa ujumla ilikua imepambwa na mikokoteni ilishosheheni madumu ya korie yaliyobeba maji na magari yenye matank ya maji kila kona.
Kwa kasi ya ajabu tunarudi miaka Ile ambayo mazingira yalikua yamepambwa kwa sauti za majenereta usiku na mchana
Au ndio ule mkakati wa kuutaka urais umeanza!? Acheni mambo yenu buana. Mama Samia yupo sana bado, ndio kwanza kumekucha
Hali ni mbaya sana na hatari kwa afya kwa jiji lenye wakazi wengi zaidi nchini, Dar Es Salaam. Watu tumepona kwenye corona lakini sasa mnataka kutulazimisha tufe kwa kipindupindu
Watendaji mnaohusika kwenye haya maeneo fanyeni kile kilichokua kinafanyika miaka mitano iliyopita hadi tukasahau kabisa kero ya umeme na maji. Kupewa nafasi ya kuhudumia wananchi kwa huduma muhimu kama umeme na maji halafu hao wananchi wakakosa hizo huduma ni wazi kabisa kwamba kufanya imeshindikana. Bora kuiacha office kuliko kukaa kwenye office halafu huduma asipatikane
Tanesco na idara za maji sisi wananchi tunamuamini rais wetu na yeye amewaamini nyie. Mnapopewa dhamana ya kutuhudumia halafu mnaamua kutuhujumu tutapaza sauti kwamba kazi imewashinda. Heri kuteua na kutumbua kuliko wananchi kuteseka kwa kukosa huduma za msingi tena ambazo wanazichangia kwa kodi zao wenyewe
Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu Samia Suluhu Hasan
Kazi iendelee
Cc Wizara ya Afya Tanzania
Tumia lugha yenye staha ujumbe utafika tuUna mavi mengi sana kichwani kaka.
Punguza kidogo mavi hayo huenda ukawa na pointi mbili tatu zenye ujazo.
Ahsante kwa ufafanuzi07 Septemba 2022
Ni kweli kumekuwepo uhaba wa mvua uliojitokeza kwenye maeneo mengi ya nchi yetu kwenye miezi ya hivi karibuni, uhaba huu umesababisha kuwepo kwa upungufu wa kina cha maji kwenye mabwawa ya kufua umeme kwa kutumia maji hivyo kuathiri hali ya uzalishaji wa umeme kwenye baadhi ya vyanzo vinavyotumia maji.
Aidha, ili kuhakikisha kuwa utoaji wa huduma ya umeme inaimarishwa nchini, Shirika limeshachukua hatua mbalimbali za muda mfupi na za muda mrefu kama ifuatavyo;
Mipango ya muda mfupi
[emoji625] Kuanzisha kituo cha kuzalisha umeme kwa njia ya Gesi asilia cha Ubungo III ambacho kimeshakamilika na kuingiza jumla ya Megawati 112 za umeme kwenye Gridi ya Taifa tangu mwanzoni mwa mwaka 2022.
[emoji625]Kuanzisha kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia Gesi asilia cha Kinyerezi I Extension kitakachozalisha jumla ya megawati 185.
Tayari megawati 45 zimeshaingizwa kwenye Gridi ya Taifa na megawati zilizobakia zitaingizwa kwenye Gridi ya Taifa hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka ujao.
[emoji625]Mradi wa kufua umeme wa Rusumo kwa kutumia maji.
Mradi huu unaozihusisha nchi tatu (Tanzania, Rwanda na Burundi) utakapokamilika, unategemewa kufua jumla ya megawati 80 za umeme, ambapo kwa upande wa Tanzania, tutapata megawati 27 za umeme zitakazoingizwa kwenye Gridi ya Taifa.
[emoji625]Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya jua wa Kishapu, Shinyanga.
Mradi huu unategemewa kuanza ujenzi wake Novemba 2022 na kukamilika Disemba 2023, utaingiza jumla ya megawati 150 za umeme kwenye Gridi ya Taifa.
[emoji625]Mradi wa kupeleka Gridi ya Taifa kwenye wilaya za mkoa wa Kigoma.
Tayari umeme wa Gridi ya Taifa umeshapelekwa kwenye wilaya ya Kibondo.
Serikali imeanza kuokoa jumla ya Tsh.9.44 bilioni kwa mwaka zilizokuwa zikitumika kununulia mafuta ya dizeli na kutengeneza mitambo (jenereta).
Mpango uliopo ni kuufikisha umme wa Gridi ya Taifa kwenye Wilaya ya Kasulu hadi Kigoma mjini kabla ya mwisho wa mwaka huu wa 2022 kufika.
Mipango ya muda mrefu
[emoji625]Mradi wa kufua umeme kwa kutumia maji wa bwawa la Julius Nyerere (JNHPP).
[emoji625]Mradi huu umefikia asilimia 71 ya utekelezaji wake.
Mradi utakapokamilika mnamo mwezi Juni 2024, unategemewa kuingiza megawati 2115 za umeme kwenye Gridi ya Taifa.
[emoji625]Kwa hatua hizi Shirika ilizozichuka zimesaidia kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini na iwapo jitihada hizi zisingechukuliwa, basi ya upatikanaji umeme nchini kwa sasa ingekuwa ipo vibaya zaidi.