Mgawo mkali wa umeme na maji unaoendelea nchini ni wazi kabisa watendaji wa Serikali mnaihujumu Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan

Mgawo mkali wa umeme na maji unaoendelea nchini ni wazi kabisa watendaji wa Serikali mnaihujumu Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan

Maendeleo ya vitu kwa kutesa watu, kutopandisha watu madaraja na mishahara, kupuuza majukumu ya Bunge, kuvunja sheria za nchi ndiyo hatutaki.

Kama tungekuwa hatutaki maendeleo ya vitu si tungekuwa tunavaa matambara mpaka leo badala ya nguo??
Swadakta!
 
Aisee imenibidi nicheke sana.😂
Yani juzi nlikua naangalia taarifa ya habari nkaona mwanamke mwembamba kavaa suti nkauliza huyo nae nani ety naambiwa ndio spika wa bunge nkasema eeeeh na yule alokua spika yule Samwel Sitta yuko wapi nkaambiwa alishakufa kitambo na washapita maspika wawili nkasema na moyo mimi nilikua wapi kipind chote hicho
 
Ili maji yasambae yanahitaji pump ambazo zinakuwa powered na umeme. So shida ya maji hasa mijini inatokana na mgao wa umeme uliokithiri. Hivi mama aliwazaje kumpa hii wizara makamba?

Hii kutaka kuridhisha kila upande ndo inamuharibia mama saizi. Kama alikuwa anampenda sana makamba au alilazimishwa kumrudisha kwenye system, angemuweka tu ikulu akawa anamuandalia hotuba za kujazana ujasiri
 
Hiki kinachoendelea kimyakimya ni mchakato wa kuturudisha kuleee miaka ilee ya 2005, 2006, 2007...... miaka ambayo Dar Es Salaam na Tanzania kwa ujumla ilikua imepambwa na mikokoteni ilishosheheni madumu ya korie yaliyobeba maji na magari yenye matank ya maji kila kona.
Kwa kasi ya ajabu tunarudi miaka Ile ambayo mazingira yalikua yamepambwa kwa sauti za majenereta usiku na mchana

Au ndio ule mkakati wa kuutaka urais umeanza!? Acheni mambo yenu buana. Mama Samia yupo sana bado, ndio kwanza kumekucha

Hali ni mbaya sana na hatari kwa afya kwa jiji lenye wakazi wengi zaidi nchini, Dar Es Salaam. Watu tumepona kwenye corona lakini sasa mnataka kutulazimisha tufe kwa kipindupindu

Watendaji mnaohusika kwenye haya maeneo fanyeni kile kilichokua kinafanyika miaka mitano iliyopita hadi tukasahau kabisa kero ya umeme na maji. Kupewa nafasi ya kuhudumia wananchi kwa huduma muhimu kama umeme na maji halafu hao wananchi wakakosa hizo huduma ni wazi kabisa kwamba kufanya imeshindikana. Bora kuiacha office kuliko kukaa kwenye office halafu huduma asipatikane

Tanesco na idara za maji sisi wananchi tunamuamini rais wetu na yeye amewaamini nyie. Mnapopewa dhamana ya kutuhudumia halafu mnaamua kutuhujumu tutapaza sauti kwamba kazi imewashinda. Heri kuteua na kutumbua kuliko wananchi kuteseka kwa kukosa huduma za msingi tena ambazo wanazichangia kwa kodi zao wenyewe

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu Samia Suluhu Hasan
Kazi iendelee

Cc Wizara ya Afya Tanzania
Alishasema yeye sio wa kufukuzana fukuzana ! Kwahiyo wamemwelewa hivyo !!
 
Wafagiaji wa Lumumba nao wanauvizia Uraisi wa Maza.
 
Waziri wa Maji kaona "awazirie" Wamisri kwenye Mabwawa na Visima yeye awe anakata Mitaa tu.
 
Back
Top Bottom