Mgawo mkali wa umeme na maji unaoendelea nchini ni wazi kabisa watendaji wa Serikali mnaihujumu Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan

Mgawo mkali wa umeme na maji unaoendelea nchini ni wazi kabisa watendaji wa Serikali mnaihujumu Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan

Wanasema maji kwenye mabwawa yote matatu yamepungua (Magufuli alishaambiwa akakaza shingo) sasa kuna katazo kubwa sanaa hata kuanzisha chujio mpya za maji kwenye mito mbali mbali.

Inasemwa harakati za kuhahakisha kwamba maji yanafika kwenye Bwawa la Nyerere ndiyo kipaumbele kwa sasa. Na wataalam (Siyo wanasiasa) wanasema inawezekana kitaalam mitambo ya kuzalishia umeme kuwashwa mwaka 2027 chini ya hapo itawashwa kisiasa kuwafurahisha wajinga.

Maana kulijaza lile bwawa siyo shughuli ndogo ati!!
 
Na hapa ndipo tatizo lilipo!

Haya ndiyo matokeo ya kuunda serikali kwa kuhusisha ndugu na marafiki. Kamwe hutaweza kuwawajibisha punde wanapoboronga.
Siyo kweli. Mara hii mshasahau kama Magufuli alitengua uteuzi wa Rafiki yake Kitwanga?
 
Majibu yanaweza kuwa haya:
1. Wanatengeneza tatizo ila baadae mtu apewe sifa na nyimbo za pambio kwa kulitatua.
2. Uwezo wa utendaji wa wizara husika umefikia ukomo
3. Hujuma, wizi, ufisadi na mengineyo
 
Hiki kinachoendelea kimyakimya ni mchakato wa kuturudisha kuleee miaka ilee ya 2005, 2006, 2007...... miaka ambayo Dar Es Salaam na Tanzania kwa ujumla ilikua imepambwa na mikokoteni ilishosheheni madumu ya korie yaliyobeba maji na magari yenye matank ya maji kila kona.
Kwa kasi ya ajabu tunarudi miaka Ile ambayo mazingira yalikua yamepambwa kwa sauti za majenereta usiku na mchana

Au ndio ule mkakati wa kuutaka urais umeanza!? Acheni mambo yenu buana. Mama Samia yupo sana bado, ndio kwanza kumekucha

Hali ni mbaya sana na hatari kwa afya kwa jiji lenye wakazi wengi zaidi nchini, Dar Es Salaam. Watu tumepona kwenye corona lakini sasa mnataka kutulazimisha tufe kwa kipindupindu

Watendaji mnaohusika kwenye haya maeneo fanyeni kile kilichokua kinafanyika miaka mitano iliyopita hadi tukasahau kabisa kero ya umeme na maji. Kupewa nafasi ya kuhudumia wananchi kwa huduma muhimu kama umeme na maji halafu hao wananchi wakakosa hizo huduma ni wazi kabisa kwamba kufanya imeshindikana. Bora kuiacha office kuliko kukaa kwenye office halafu huduma asipatikane

Tanesco na idara za maji sisi wananchi tunamuamini rais wetu na yeye amewaamini nyie. Mnapopewa dhamana ya kutuhudumia halafu mnaamua kutuhujumu tutapaza sauti kwamba kazi imewashinda. Heri kuteua na kutumbua kuliko wananchi kuteseka kwa kukosa huduma za msingi tena ambazo wanazichangia kwa kodi zao wenyewe

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wetu Samia Suluhu Hasan
Kazi iendelee

Cc Wizara ya Afya Tanzania
Mimi nilidhani ni ukame kumbe ni hujuma😳 Halafu Chalamila anasema kuna waziri yuko nje anaitafuta hela za kampeni 2025.Mbogamboga mtauana wallah!
 
Mimi nilidhani ni ukame kumbe ni hujuma😳 Halafu Chalamila anasema kuna waziri yuko nje anaitafuta hela za kampeni 2025.Mbogamboga mtauana wallah!

Ukitaka kujua hii sio issue ya ccm tuu nenda akhera ukakutane na chachawangwe
 
Jamhuri ya Muuuungano,kazi ya kulamba asali iendelee!
Waache tu Watumishi wa serikali watutese,Mama anawaangalia kwa jicho legevu🤣🤣🤣
 
Tungebaki na gesi tu, hilo bwawa linaweza kuwa changamoto sana
Wanasema maji kwenye mabwawa yote matatu yamepungua (Magufuli alishaambiwa akakaza shingo) sasa kuna katazo kubwa sanaa hata kuanzisha chujio mpya za maji kwenye mito mbali mbali.

Inasemwa harakati za kuhahakisha kwamba maji yanafika kwenye Bwawa la Nyerere ndiyo kipaumbele kwa sasa. Na wataalam (Siyo wanasiasa) wanasema inawezekana kitaalam mitambo ya kuzalishia umeme kuwashwa mwaka 2027 chini ya hapo itawashwa kisiasa kuwafurahisha wajinga.

Maana kulijaza lile bwawa siyo shughuli ndogo ati!!
 
Tungebaki na gesi tu, hilo bwawa linaweza kuwa changamoto sana
Kabisa. Na kuna tetesi kwamba hilo bwawa likijazwa maji yake yatarudi nyuma toka kwenye kizuia maji cha bwawa kwa kilomita mia.

Kama ni kweli itakuwa ni balaa!!
 
Wanasema maji kwenye mabwawa yote matatu yamepungua (Magufuli alishaambiwa akakaza shingo) sasa kuna katazo kubwa sanaa hata kuanzisha chujio mpya za maji kwenye mito mbali mbali.

Inasemwa harakati za kuhahakisha kwamba maji yanafika kwenye Bwawa la Nyerere ndiyo kipaumbele kwa sasa. Na wataalam (Siyo wanasiasa) wanasema inawezekana kitaalam mitambo ya kuzalishia umeme kuwashwa mwaka 2027 chini ya hapo itawashwa kisiasa kuwafurahisha wajinga.

Maana kulijaza lile bwawa siyo shughuli ndogo ati!!
Una mavi mengi sana kichwani kaka.

Punguza kidogo mavi hayo huenda ukawa na pointi mbili tatu zenye ujazo.
 
Back
Top Bottom