Mgogoro KKKT Dayosisi ya Konde nani alaumiwe?

Mgogoro KKKT Dayosisi ya Konde nani alaumiwe?

Man from cuba

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2021
Posts
571
Reaction score
1,394
Kanisa la kiinjili la kiluteri Tanzania KKKT dayosisi ya konde limeingia majaribuni baada ya mgogoro wa muda mrefu uliotokana na uamuzi wa askofu wake Dkt. Mwaikali kuhamisha kiti cha askofu kutoka Tukuyu kulipokuwepo makao makuu ya dayosisi ya konde kuyapeleka Mbeya mjini uamuzi uliozua mgogoro mkubwa kwa waumini wa KKKT Tukuyu mjini kumtimua askofu Mwaikali hadi kuokolewa na polisi.

Mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu licha ya juhudi mbalimbali za kusuluhisha.

Waumini wengi wanahoji kama viongozi wao wanakuwa kwenye mgogoro je kondoo nani wa kuwachunga?? Je dini kwa sasa zimekuwa biashara Hadi kuzusha ugomvi wa kuzomeana makanisani??
 
Migogoro ya kidini ni kitu cha kawaida sana pale kunapokua na viongozi wanakyusa.
Kwani mgogoro mkubwa kabisa Tanzania wa makanisa si ulikuwa wa Moses Kulola na Emmanuel Lazaro? Hivi walikuwa ni Wanyakyusa?

Mgogoro mwingine mkubwa ulikuwa wa Cheyo na Hitson Mwamlima wa Moravian, mgogoro huu uliamuliwa na Augustine Lyatonga Mrema, je Hawa pia walikuwa ni Wanyakyusa?
 
Kuna wakati kulikuwa na mgogoro huko upare hadi wakawa wanafyeka migomba, ikahamia bukoba huko japo sikuufuatilia, Sasa ni tukuyu.

Hili kanisa lina kitu kimepungua hata huku ninakisali hakujatulia japo ni kimya kimya.

Ngoja tuone
 
Kwani mgogoro mkubwa kabisa Tanzania wa makanisa si ulikuwa wa Moses Kulola na Emmanuel Lazaro? Hivi walikuwa ni Wanyakyusa?

Mgogoro mwingine mkubwa ulikuwa wa Cheyo na Hitson Mwamlima wa Moravian, mgogoro huu uliamuliwa na Augustine Lyatonga Mrema, je Hawa pia walikuwa ni Wanyakyusa?
Mwamlima ndo hao hao
 
Kanisa la kiinjili la kiluteri Tanzania KKKT dayosisi ya konde limeingia majaribuni baada ya mgogoro wa muda mrefu uliotokana na uamuzi wa askofu wake dr.Mwaikali kuhamisha kiti cha askofu kutoka Tukuyu kulipokuwepo makao makuu ya dayosisi ya konde kuyapeleka Mbeya mjini uamuzi uliozua mgogoro mkubwa kwa waumini wa KKKT Tukuyu mjini kumtimua askofu Mwaikali hadi kuokolewa na polisi.
Askofu huyo naye kichwani hazina

Hilo li kiti la Askofu angeliacha libaki huko huko Tukuyu angepungukiwa nini?

Ukorofi tu
 
Nyie wengine ni vitoto vidogo.

Hamjui mgogoro mkubwa wa Dayosisi ya Meru kujitenga toka Dayosisi ya Kaskazini miaka ya 90.

Kimsingi ukabila kati ya wachaga na wameru ambapo watu waliuana.
Mimi nimetembea na mama yako siwezi kua mtoto mdogo.

Mgogoro wa wameru kuchomeana kanisani wewe binti huna cha kunifundisha mimi
 
Nyie wengine ni vitoto vidogo.

Hamjui mgogoro mkubwa wa Dayosisi ya Meru kujitenga toka Dayosisi ya Kaskazini miaka ya 90.

Kimsingi ukabila kati ya wachaga na wameru ambapo watu waliuana.
mkuu umenukumbusha Askofu akyooo . Hii ilisababisha akaenda kupata hifadhi chuo cha biblia pale Mwika
 
Kwani mgogoro mkubwa kabisa Tanzania wa makanisa si ulikuwa wa Moses Kulola na Emmanuel Lazaro? Hivi walikuwa ni Wanyakyusa?

Mgogoro mwingine mkubwa ulikuwa wa Cheyo na Hitson Mwamlima wa Moravian, mgogoro huu uliamuliwa na Augustine Lyatonga Mrema, je Hawa pia walikuwa ni Wanyakyusa?
Mrema alikuwa master...kuna ule wa Meru nao ni yeye alisuluhisha.

Lutheran kwa migogoro tupo vizuri. Usisahau ule wa Same vs Mwanga
 
Back
Top Bottom