Mgogoro KKKT Dayosisi ya Konde nani alaumiwe?

Mgogoro KKKT Dayosisi ya Konde nani alaumiwe?

Mrema alikuwa master...kuna ule wa Meru nao ni yeye alisuluhisha.

Lutheran kwa migogoro tupo vizuri. Usisahau ule wa Same vs Mwanga
KKKT pesa mbele na kila askofu ni mtemi kwenye dayosisi yake.Wanapenda Sana mademu.Mdegela Iringa ilikuwa balaa,Malasusa DMP usipime na Munga naye vile vile.Kuna Mngw'amba DMP naye alitisha.
 
Nimekuja kugundua askofu mwaikali japo simjui Ila alikuwa na Sababu za msingi Sana kuitoa hyo dayosis huko tukuyu na kuleta mbeya mjini
Ni vzr sna ingekuwa hvyo ili iwe rais kufikika kwa watu wote kuliko mtu kutokea ileje huko ndani huko au kamsamba ndani uko aje akatize mbeya Mjini na kwenda tukuyu kupata huduma za kidayosis wkt mbeya mjini ndiko kuliko center nzuri

Askfu mwaikali sijaona kosa lake la kuenguliwa ktk kiti chake cha halali kbsa na maono yake

Mpk imepelekea askofu kufukuzwa kwenye msiba wa askofu gehaz malazuza ambaye pia mwanae Alex gehaz malazuza alishapata kuwa mkuu wa kanisa hili akiliendesha kibabe San havyo hvyo hata Bab ake askof gehaz malazuza alishapata kuwa mkuu pia wa kanisa hili ktk kipindi Cha nyuma hvyo ikumbukwe kuwa hado dayossi imepelekwa kijijini huko tukuyu Ni kwamba kulianzia mbali San

Mgogoro huu engineer wake Ni Alex gehaz malazuza Bab askofu huyu Ni mkabila San na pia Yuko nyuma ya hili kuhakikisha kuwa makao hayaami katk kijij hicho Cha tukuyu

Wamemuonea sna. Asko Dr Edward mwaikali napanga kumchamgia pesa ili apeleke swala hili mahakamani
Na
Wanyakyusa acheni kuchafua kanisa kwa tamaa zenu za madaraka na Kama vip hameni tu huku ndio maaan makanisa Ni mengin sna huko sabubu kubwa ni kwamba mnapenda madaraka sna ktk kuongoza kanisa na uchawi muache pia kuapply
Malazuza ama Malasusa ?
 
Kanisa la kiinjili la kiluteri Tanzania KKKT dayosisi ya konde limeingia majaribuni baada ya mgogoro wa muda mrefu uliotokana na uamuzi wa askofu wake Dkt. Mwaikali kuhamisha kiti cha askofu kutoka Tukuyu kulipokuwepo makao makuu ya dayosisi ya konde kuyapeleka Mbeya mjini uamuzi uliozua mgogoro mkubwa kwa waumini wa KKKT Tukuyu mjini kumtimua askofu Mwaikali hadi kuokolewa na polisi.

Mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu licha ya juhudi mbalimbali za kusuluhisha.

Waumini wengi wanahoji kama viongozi wao wanakuwa kwenye mgogoro je kondoo nani wa kuwachunga?? Je dini kwa sasa zimekuwa biashara Hadi kuzusha ugomvi wa kuzomeana makanisani??
BARAZA la Vijana wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT, Dayosisi ya Konde, limemtupia lawama Mkuu wa kanisa hilo nchini, Askofu Dk. Fredrick Shoo, likidai kuongoza mkutano wa kumwondoa Askofu wa dayosisi hiyo, Dk. Edward Mwaikali, badala ya kutafuta njia sahihi ya kumaliza mgogoro ....

[https://res]

unaofukuta.

Akisoma taarifa ya msimamo wa vijana wa dayosisi hiyo jana, Marko Mahenge, alidai Askofu Dk. Shoo amekuwa sehemu ya kukuza mgogoro huo badala ya kutafuta njia sahihi ya kujadili namna ya kushughulika na jambo hilo ambalo linaendelea kuyumbisha Dayosisi ya Konde.

Alisema kwa muda mrefu vijana walikuwa kimya wakifuatilia mwenendo ya mgogoro huo huku wakitarajia kufanyika kwa hekima na busara katika kushughulikia maridhiano ya kuhamisha makao makuu ya dayosisi hiyo kutoka mjini Tukuyu katika Wilaya ya Rungwe na kupelekwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

“Sisi vijana wa Jimbo hili la Mbeya na maeneo mengine ya dayosisi hii tunapinga vikali uamuzi wa Mkuu wa Kanisa kumwondoa Askofu Mwaikali kwenye kiti chake kwa sababu mkutano uliofanyika Machi 22, katika Ushirika wa Uyole ulikuwa batili, tunamtambua Dk. Mwaikali kuwa ndiye askofu wetu na hapa jimboni haondoka wala mchungaji au Mkuu wa Jimbo,” alisema Mahenge.

Aidha, Mahenge aliliomba Baraza la Maaskofu wa kanisa hilo nchini kuingilia kati mgogoro huo kwa kuiita halmashauri kuu ya dayosisi na viongozi wengine ili kukubaliana mambo ya kufanya.

Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa Kuu la Ruanda, yalipo makao makuu ya Dayosisi ya Konde, Mkuu wa Jimbo, Mchungaji Nyibuko Mwambola, alisema Halmashauri Kuu haitambui mkutano ulioitishwa na Askofu Dk. Fredrick Shoo kwa madai kuwa ulikuwa batili.

Alimtupia lawama Askofu Dk. Shoo kama mkuu wa kanisa kwa kushindwa kusuluhisha mgogoro huo na kuwa sehemu ya kuchochea hali ambayo alidai inazidi kuongeza chuki na mfarakano.

Kadhalika, alisema baada ya mkutano wa kumchagua askofu mwingine, Geofrey Mwakihaba, Askofu Dk. Shoo alituma waraka kwa taasisi zote za kifedha kufunga akaunti za dayosisi.

Alisema hatua hiyo imewasababishia kushindwa kufanya malipo yoyote ikiwamo mishahara ya wachungaji na watumishi wengine wa dayosisi hiyo.

Vile vile, alidai kuwa Dk. Shoo amewatumia barua wachungaji wote wa Dayosisi ya Konde kuhudhuria kikao kinachofanyika kesho jijini Dodoma, bila kumpa taarifa Askofu wa Jimbo Dk. Mwaikali, na kwamba Halmashauri Kuu imesema naye atashiriki kikao hicho.

“Mkuu wa Kanisa ameonyesha dhahiri upande alipo kwa sababu ameshindwa kutukutanisha pamoja viongozi wa dayosisi na kujadili pamoja namna bora ya kumaliza huu mgogoro badala yake ameonesha wazi kushindwa kusimamia jambo hilo na kuchangia kuchochea suala hili, sisi tunamtambua bado Askofu Mwaikali ndiyo anasimamia dayosisi yetu ya Konde,” alisisitiza.

“Haiwezekani Mkuu wa Kanisa aitishe mkutano na kufanya uchaguzi wa kumchagua askofu mwingine, tena kwa siku moja, inaonyesha dhahiri kuna chuki binafsi na sio suala la kuhamisha makao mkuu ya dayosisi.”

Machi 22 mwaka huu Mkuu wa Kanisa la KKKT nchini, Askofu Dk Fredrick Shoo, pamoja na wajumbe 201 walifanya mkutano katika Usharika wa Uyole jijini Mbeya kwa lengo la kumaliza mgogoro huo ambapo liliibuka suala la wajumbe kutokuwa na imani na Askofu Dk. Edward Mwaikali.

Katika mkutano huo ambao uliendeshwa na Askofu Dk. Shoo na kudumu kwa saa 10, ulitumika kumchagua Askofu mwingine Mchungaji Geofrey Mwakihaba, ambaye alitangazwa mbele ya wajumbe wa mkutano.

Kutokana na uamuzi huo baadhi ya vijana wa KKKT mkoani Mbeya walieleza kuwa mchakato uliotumika kuwa ulikuwa batili.

Hata hivyo, Askofu Dk. Shoo alipotafutwa na Nipashe kwa simu jana, muda wote hakupatikana kuzungumzia suala hilo.

Mgogoro wa kwanini yahamishwe makao makuu ya dayosisi kutoka mjini Tukuyu katika Wilaya ya Rungwe na kwenda Halmashauri ya Jiji la Mbeya, ulianza kufukuta tangu mwaka 2017 hadi sasa.
 
Askofu Shoo amepata opportunity ya kuonyesha umahiri wake, kwa kumaliza changamoto za konde.
Huku kwingine huwa anaongea kwa amri na ubabe. Sijui kanisani kama atafanya hivyo🤣🤣🤣🤣
 
KKKT migogoro mingine inafukuta chini kwa chini, Jimbo la mafinga nalo lilijitoa dayosisi ya kusini linataka dayosisi yake. Sababu wanasema wamechoshwa na unyonyaji....yale yale ya Meru versus dayosisi ya kaskazini au upareni.

Huku tuendako wengi wataibuka
 
Back
Top Bottom