Mgogoro mkubwa baina ya Serikali na wananchi waishio ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

Mgogoro mkubwa baina ya Serikali na wananchi waishio ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

Bikis

Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
52
Reaction score
74
Wasalaam kutoka Ngorongoro.

JF na Great thinkers wote wa humu wamekuwa na mchango mkubwa kwa matatizo yanayowakabili wananchi wa Tanzania kutoka maeneo mbalimbali...

Nawandikia hivi ikiwa kuna mgogoro mkubwa ndani ya Ngorongoro ikihusishwa na nia ya Serikali kutaka kuwaondoa wananchi hao wapata takriban 100,000 ili kupisha shughuli ya uhifadhi na utalii

Wananchi hawa wamedai baada ya ahadi ya kuhamishwa kutoka Serengeti kuja Ngorongoro hapakuwa na makubaliano ya kwamba baada ya kipindi fulani wataondolewa tena kutoka Ngorongoro kupelekwa pasipojulikana!!

Wananchi wameendelea kuwa na imani na Rais Samia Suluhu lakini wamekuwa wakilalamika kwamba huenda Rais anadanganywa na wataalam haswa mhifadhi mkuu bwana Manongi pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

Angalia malalamiko ya wananchi hapo chini
 
Watanzania wengi hawaelewi. Hawa watu wameshaharibu kabisa walipotoka mfano Monduli hata maji hamna kwasababu ya mifugo yaani kumekuwa kama jagwa.

Inabidi serikali itengeneze mbuga ambayo iwe makazi ya wafugaji lakini waweke utaratibu wa mazingira, wataalamu, visima vya maji ... bila hivi tutakuwa na matatizo. Nina shamba kidomole bagamoyo napigana na mvamizi wa kimang'ati aondoke kwenye shamba langu.

Nimepanda mitu sijui mingapi imeliwa! yaani tunajaribu kupanda miti mifugo inaharibu.
 
Mtoa mada hii sio rocket science,hapa tunahitaji political will na utafiti kidogo hasa wa kujifunza wenzetu wamemudu vipi kwa wild animals na human being to coexistence.

Nitatoa mfano wa Botswana,hii nchi ina mji inaitwa Kasane ipo karibu mno na mipaka ya Zimbabwe, Zambia na Namibia na pale wild animals wanavinjari katikati ya mji ila zile corridors zao hazijazibwa means wild animals wanaendelea na maisha pamoja na binadamu ila muhimu alama zipo wild animals they have a right of way.

Hii ngorongoro yetu tunaweza kabisa binadamu na wild animals wakaishi pamoja ni just to RESPECT wanyama hao, ile barabara ya Nasa hadi Kasane (Botswana) ni almost mbuga ya wanyama ila binadamu na mifugo yao wanaishi in harmony kabisa.Pls my minister of Tourism na mawasiliano tembeleeni hii nchi ili mjifunze maarifa mapya yatakayotusaidia, hakuna gharama kabisa just toyota fortune moja inatosha au H1(Hyundai).
 
Ngorongoro itakufa kabisa ndani miaka 10 ijayo kama Serekali itashindwa kuhamisha wamaasai ambao wamezidi kuongezaka na mifugo imekuwa mingi.

Tanzania ni kubwa ni vyema Serekali ikaunganisha Ngorongoro na TANAPA na kuondoa upuuzi wa uhifadhi wa wanyamapori na binadamu.
 
NGORONGORO ina uwezo wa kuhudumia idadi ya watu wapatao elfu 28 tu sasa wapo 120,000.

Mifugo inayoweza kupata malisho ni elfu 54 ( ng'ombe,punda,kondoo na mbuzi) sasa Hifadhi ina jumla ya wanyama wafugwao laki 2 na ushee.

Watu wamezidi
Makazi na ujenzi holela pia yamezidi
Ujenzi holela wa bati tena za kung'aa Usiku na mchana zimechochea kukimbiza wanyama kama swala nyumbu na twiga.
Vichaka vya swala kukaa kwenye vivuli vimepungua na sasa ni jangwa
Wamasai sasa wameanza kuwinda na kula wanyamapori
Mifuko ya plastic na vifungashio vingine kama karatasi za biskut (benteni ) zimekithiri na kuharibu mazingira na madhari mazuri ya NGORONGORO.

Njooni na suluhisho la nini kifanyike NGORONGORO ibaki hai nanyi muendelee kuishi bila kubugudhi hifadhi.

Shida ya wafugaji wa NGORONGORO mnadhani hamuwezi kuishi sehemu nyingine tofauti na NGORONGORO.
Hifadhi imewahi kuwasaidia nini ?
Kipato chenu duni
Maji ya shida
Makazi duni
Barabara duni
Hakuna kulima

Nendeni Meatu, Karatu mkaishi vizuri.
Mnaishije kwenye ardhi ambayo huwezi mrithisha mwanao ?
 
Hapa kwetu Tanzania tatizo siyo kurespect those two way rights to each ila tatizo lipo kwa hawa non-boundaries colleagues ambao waliambiwa jinsi ya kuishi na utaratibu wa pale mbugani although wanavuruga.

Mfano kuna wakati ilitakiwa hawa jamaa wawe (mfano wasizidi 20ppl) but wameongezeka na kuanza kugawana ardhi kwa kujenga nyumba huku mifugo ikizidi kuongezeka.

Pia hawa jamaa zetu wamekuwa hawaaminiki kila wakati wamekuwa wakienenda tofauti na mahitaji ya eneo la ngorongoro.
 
Waache kudekezwa hao watu wakimbizwe waje mtaani kuungana na binadamu wa kawaida au watengewe mapori yao maalumu
Mkuu nikwambie tu kama hujui, wengi wa hao jamaa wamewekeza sana hapa jijini Arusha, wana mijengo, biashara nk, na ndiyo hao hao wanaoongoza migomo au kushabikia migongano.
 
Wahamishwe kiungwana bila kutumia nguvu kupelekwa maeneo watakayokubaliana. Hii ni option best. Ikishindikana then option2 ndio itumike. Na hata hiyo kwanza watayarishiwe eneo lingine. Elimu pia muhimu. Una mifugo 500 na bado unalalia ngozi! ...ni uksefu wa elimu.
 
Wasalaam kutoka Ngorongoro.

JF na Great thinkers wote wa humu wamekuwa na mchango mkubwa kwa matatizo yanayowakabili wananchi wa Tanzania kutoka maeneo mbalimbali...

Nawandikia hivi ikiwa kuna mgogoro mkubwa ndani ya Ngorongoro ikihusishwa na nia ya Serikali kutaka kuwaondoa wananchi hao wapata takriban 100,000 ili kupisha shughuli ya uhifadhi na utalii

Wananchi hawa wamedai baada ya ahadi ya kuhamishwa kutoka Serengeti kuja Ngorongoro hapakuwa na makubaliano ya kwamba baada ya kipindi fulani wataondolewa tena kutoka Ngorongoro kupelekwa pasipojulikana!!

Wananchi wameendelea kuwa na imani na Rais Samia Suluhu lakini wamekuwa wakilalamika kwamba huenda Rais anadanganywa na wataalam haswa mhifadhi mkuu bwana Manongi pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

Angalia malalamiko ya wananchi hapo chini
Kwetu sisi twiga ana thamani sana
 
Nashauri Serikali iwahamishie Wamasai Pemba kule maana kuna mapori tu na makazi ya watu kidogo.
 
Wasalaam kutoka Ngorongoro.

JF na Great thinkers wote wa humu wamekuwa na mchango mkubwa kwa matatizo yanayowakabili wananchi wa Tanzania kutoka maeneo mbalimbali...

Nawandikia hivi ikiwa kuna mgogoro mkubwa ndani ya Ngorongoro ikihusishwa na nia ya Serikali kutaka kuwaondoa wananchi hao wapata takriban 100,000 ili kupisha shughuli ya uhifadhi na utalii

Wananchi hawa wamedai baada ya ahadi ya kuhamishwa kutoka Serengeti kuja Ngorongoro hapakuwa na makubaliano ya kwamba baada ya kipindi fulani wataondolewa tena kutoka Ngorongoro kupelekwa pasipojulikana!!

Wananchi wameendelea kuwa na imani na Rais Samia Suluhu lakini wamekuwa wakilalamika kwamba huenda Rais anadanganywa na wataalam haswa mhifadhi mkuu bwana Manongi pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

Angalia malalamiko ya wananchi hapo chini
unajua masai hata ukipeleka shule huwa haelimiki. kwamba wanasheria wote hawa hata kina Ole ngurumo, wanapambana waendelee kuishi na kuchungia mifugo ndani ya mbuga? kwa wale waliofika ngorongoro haiji kichwani kwamba kuna mtu anaweza kuamua kupigania eti haki ya kuishi kule, pamoja na wanyama, na hapohapo haelewi kuwa ardhi ni mali ya serikali, sisi wengine tunaazima tu. niliona juzi hapa wengine wameenda hadi mahakama ya africa mashariki. fukuzia mbali masai hao wanaharibi mbuga. serikali ifumbe macho ifukuze kabisa wasituletee mambo ya kiporipori hapa.
 
Back
Top Bottom