NGORONGORO ina uwezo wa kuhudumia idadi ya watu wapatao elfu 28 tu sasa wapo 120,000.
Mifugo inayoweza kupata malisho ni elfu 54 ( ng'ombe,punda,kondoo na mbuzi) sasa Hifadhi ina jumla ya wanyama wafugwao laki 2 na ushee.
Watu wamezidi
Makazi na ujenzi holela pia yamezidi
Ujenzi holela wa bati tena za kung'aa Usiku na mchana zimechochea kukimbiza wanyama kama swala nyumbu na twiga.
Vichaka vya swala kukaa kwenye vivuli vimepungua na sasa ni jangwa
Wamasai sasa wameanza kuwinda na kula wanyamapori
Mifuko ya plastic na vifungashio vingine kama karatasi za biskut (benteni ) zimekithiri na kuharibu mazingira na madhari mazuri ya NGORONGORO.
Njooni na suluhisho la nini kifanyike NGORONGORO ibaki hai nanyi muendelee kuishi bila kubugudhi hifadhi.
Shida ya wafugaji wa NGORONGORO mnadhani hamuwezi kuishi sehemu nyingine tofauti na NGORONGORO.
Hifadhi imewahi kuwasaidia nini ?
Kipato chenu duni
Maji ya shida
Makazi duni
Barabara duni
Hakuna kulima
Nendeni Meatu, Karatu mkaishi vizuri.
Mnaishije kwenye ardhi ambayo huwezi mrithisha mwanao ?