Mgogoro wa Bandari na Vita vya Misemo: Kupanguliwa kwa Mipango na Uongozi

Mgogoro wa Bandari na Vita vya Misemo: Kupanguliwa kwa Mipango na Uongozi

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu?

Kwa wale tuliokuwa tunafuatilia methali, na misemo mbali mbali ya wahenga shuleni. Bila shaka mnaukumbuka msemo huu unaosema kuwa siku ya kufa nyani basi miti yote atakayoshika itamtereza.

Msemo huu kwa wale vichwa nazi mnaweza kuuchukulia poa, lkn kiuhalisia una maana kubwa sana.

Hebu angalia mwenyewe jinsi wale jamaa zetu waliokuwa wameigeuza bandari yetu shamba la bibi, walivyohangaika kupambania ugali wao kupitia kwenye migongo ya watu mbali mbali walioamini kuwa wanaushawishi wa kuweza kuzuia mipango mizuri ya serikali yenye lengo la kuleta ufanisi, uchapakazi na usimamizi mzuri pale bandarini.

Jamaa walianza kwa kuwatumia wanasiasa uchwara kupigia jaramba tonge lao, walivyoona wanasiasa hao hawana impact yoyote na mikutano yao haifuatiliwi na wananchi, wakahamia kwa yule wakili njaa huku akiongozwa na yule Dr aliewahi kufilisiwa hela zote na hawara yake hadi kupelekea Dr huyo kuanza kulalia na kushindia mihogo.

Baada ya Dr mihogo nae wakili wake nao kuangukia pua, ndo likatafutwa kundi la wale wanaoitwa viongozi wa dini. Kundi hili ni miongoni mwa wafaidika wakubwa wa mfumo mbovu uliopo Sasa pale bandarini, hivyo kitendo cha kuingilia swala hili hakikuwashangaza raia wengi, kwani tulijua ni lazima kundi hili lingejitokeza tu hasa pale walipoona wanaotumwa wanachemsha kukamilisha mission.

Kundi hilo la wanaoitwa viongozi wa dini na wanufaika wa mfumo mbovu waliingia katika swala lenyewe kichwa kichwa bila kuwa na data, au kuweka data zinazoonesha ni % ngapi ya watanzania wanaopinga mkataba wa bandari na % ngapi wanapinga.

Najua viongozi hao huenda walifanya utafiti wao kupitia JF na mitandao mingine ya kijamii bila kujua kwamba mitandao mingi au naweza kusema yote haina idadi halisi ya member wake.

Mfano hapa JF ni kawaida kumkuta member mmoja ana ID 10, kwahiyo members 10 wenye ID kumi kumi wakikoment kwa kila ID moja moja utapata watu 100, hivyo viongozi hao wakiona hiyo 100 wanajua ni members tofauti tofauti, kumbe kiuhalisia ni members 10 tu wenye IDs kumi kumi.

Walitegemea ile idadi waliyojitungia ingesababisha uungwaji mkono kutoka kwa watu wengine mbali mbali, including viongozi wengine wa dini na madhehebu mbali mbali, bahati nzuri wale viongozi wenye akili na maono kama askofu Shoo wameshawaelewa na kuwapuuza viongozi hao, hali inayopelekea viongozi hao wa dini wawatumie chawa wao kuwashambulia kina askofu Shoo kwa kukataa kugeuzwa kondoo kwa masilahi yao wenyewe.

Kwa msururu huo nafikiri mmeshaona wenyewe jinsi jamaa kila wanachoshika au kupanga kinapanguliwa

Narudia tena, hayati Magufuli hakumchagua raisi Samia kuwa mgombea mwenza kwa bahati mbaya. Bali alifanya vile kutokana na kuijua vizuri misimamo thabiti ya huyu mama. Hayati Magufuli alipokufa watu wakajua labda mama atashikwa masikio kiurahisi na kutelekeza miradi yote aliyoianzisha jemedari wetu na mzalendo wetu wa kweli hayati John Pombe Magufuli.

Wakaja kushtuka masikio ya mama yanateleza hayashikiki, miradi kaisimamia imeisha na kuanzisha ya kwake yenye tija, kwahiyo kelele zenu ni za mfa maji huwa lazima atape tape.

Yale makaratasi yalioandikwa na viongozi hao wakwepa kodi, hayatobadilisha chochote, na hawatoweza kumfanya raisi chochote. Trust me 🤞
 
Wat
Habari zenu wanaJF wenzangu?

Kwa wale tuliokuwa tunafuatilia methali, na misemo mbali mbali ya wahenga shuleni. Bila shaka mnaukumbuka msemo huu unaosema kuwa siku ya kufa nyani basi miti yote atakayoshika itamtereza...
Wakati wewe uko busy hapa kukejeli harakati za kupinga ule mkataba wa kilaghai wa kuuzwa bandari zetu, unasahau kuwa mama na washauri wake huko presha zinapanda, sukari hazishuki, trip za kwenda toilet haziishi, jasho jembamba linawatoka, hawajui cha kufanya, woga umewajaa, hawaamini kama watanganyika wamekuwa jeuri kiasi hiki.

Ngoma bado mbichi.
Mkataba wa kilaghai hauwezi kutekelezeka.
 
Kukiri kwamba watumishi wanaopewa majukumu ya kusimamia upatikanaji wa mapato bandarini ni wezi, basi viongozi waandamizi wa serikali ndio viranja wa huo wizi maana wanawajibika kudhibiti kwa kuchukua hatua stahiki za kinidhamu na kisheria ikiwemo kuwapeleka mahakamani kitu ambacho wamekiogopa kwa kuwa wataumbuliwa kutajwa huko.
Bwashee mbona unaji quote mwenyewe?
 
Back
Top Bottom