Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
MUUNGWANA AKIVULIWA NGUO HUCHUTAMA.
Tukubali tukatae ila Tanzania tuna media za kipuuzi kuwahi kutokea, sio Clouds, IPP Media, mwananchi ila Media za Tanzania kwa 90% ni utumbo kabsa.
Mwaka uliopita, wakati Tanzania ikipitia kipindi kigumu cha mvutano wa kisiasa baada ya uchaguzi, taarifa zilienea kuhusu watu kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika matukio ya vurugu ambayo walihusika ji vyombo vya dola. Katika mitaa na vijiji, familia zililia wapendwa wao walipata matatizo na wengine kufariki.
Majirani walishuhudia damu ikimwagika magetini. Lakini katika vyumba vya habari vya televisheni na redio nyingi nchini, kulikuwa na ukimya mzito, hakuna ambaye alitangaza sio TBC wala ITV.
Cha kushangaza zaidi ni kwamba baadhi ya wanahabari wenyewe waliguswa moja kwa moja na matukio hayo. Wengine walikuwa na ndugu waliojeruhiwa au hata kupoteza maisha. Hata hivyo, bado sauti zao zilibaki kimya mbele ya umma.
Lakini mwaka huu tunashuhudia kitu tofauti kabisa. Mgogoro wa kimataifa kati ya Iran na Israel umekuwa habari kubwa katika vyombo vya habari vya Tanzania. Vipindi maalum vinaandaliwa, wachambuzi wanaitwa studio, ramani zinaoneshwa, na maelezo yanatolewa kana kwamba waandishi wa habari wapo moja kwa moja Mashariki ya Kati.
NI ghafla, vyombo vya habari vinaonekana kuwa na ujasiri wa kuchambua vita, diplomasia, na siasa za kimataifa kwa undani mkubwa. Wanaeleza harakati za kijeshi, maamuzi ya viongozi wa dunia, na athari za kiuchumi za mgogoro huo.
Swali kuu ninalojiuliza ni: ikiwa tunaweza kuzungumza kwa ujasiri kuhusu vita vilivyo maelfu ya kilomita kutoka nyumbani, kwa nini tulishindwa kuzungumza kwa ujasiri kuhusu damu iliyomwagika karibu nasi?
Je, umbali wa kilomita 4,000 unafanya ukweli uwe rahisi kusema kuliko ule uliotokea barabarani kwetu? Je, ni rahisi kuchambua mateso ya watu wa mbali kuliko mateso ya jirani yako?
MNGEKAA KIMYA TU, MAANA NI KAMA UNAONESHA NYIE NI WANAFIKI KWA KIWANGO KIPI.