Mgogoro wa Kariakoo sio rahisi kuumaliza, bado yataendelea

Binafsi nakubaliana na Mfanyabishara aambae analeta alternative ila sio kupinga tuu Kodi ,kama serikali imefanya uchambuzi na kuona hiyo alternative sio endelevu na Haina Tija hawawezi kuikubali.
 
Wafanyabiashara Sisi sio kama walimu au madaktari jipangeni
msije mkajiona mna nguvu ya kuitetemesha serikali, lipeni kodi stahiki mselete ujanjaujanja wa kukwepa. Iwe mwanzo na mwisho kugoma
 
Tz mfanyabiashara wa Kkoo anayeuza mzigo wa 5m kwa siku na faida si chini ya 2m kwa siku anataka kutoa kodi ya laki 5 kwa miezi 3, hao jamaa si wa kuwachekea, ni wakwepaji kodi wakubwa.
Hapa umetudanganya
 
Kama kila atakaye lia atabembelezwa nchi itakuwa ngumu, TRA wana sheria zao, na sekta zingine pia… sasa kama ukigoma una bembelezwa si na walimu, dala dala, boda boda na wengine watagoma pia
Kufunga biashara it’s not a crime, wangewaacha tu njaa ingewatoa mashimoni na si hivi… sasa wanajiona wao ni special
 
Nakuunga mkono na mguu,Nchi haiwezi kwenda Kwa staili hiyo
 
Tz mfanyabiashara wa Kkoo anayeuza mzigo wa 5m kwa siku na faida si chini ya 2m kwa siku anataka kutoa kodi ya laki 5 kwa miezi 3, hao jamaa si wa kuwachekea, ni wakwepaji kodi wakubwa.
Hesabu haiendani na uhalisia, mtaji wa million 5 faida ni laki 3 hadi laki 5 inafatana na biashara
 
Tz mfanyabiashara wa Kkoo anayeuza mzigo wa 5m kwa siku na faida si chini ya 2m kwa siku anataka kutoa kodi ya laki 5 kwa miezi 3, hao jamaa si wa kuwachekea, ni wakwepaji kodi wakubwa.
Duh... mzigo gani huo unalipa kiasi hicho Mkuu.. tupeane deal.
 
Duh... mzigo gani huo unalipa kiasi hicho Mkuu.. tupeane deal.
Mfano mdogo tu ni Pharmaceutical products, faida ni nusu almost ya mauzo. Kkoo akiuza mzigo wa 5m kwa siku faida si chini ya 2m, hao jamaa ni hawataki kulipa kodi, VAT ni ya mnunuzi ndio analipa, wao inawauma nini ?
 
Mi nakushauri wewe fungua duka Kariakoo, fanya kwa mwaka mmoja tu, halafu rudi usome hii comment yako. Mimi nipo tayari kukukopesha milioni 200 ufungue biashara Kariakoo, ulipe kodi zote na usikate kona hata kidogo, ukifanikiwa kutoboa mwaka wa pili, nakusamehe huo mkopo. Ila nataka dhamana ya nyumba.
 
Tz mfanyabiashara wa Kkoo anayeuza mzigo wa 5m kwa siku na faida si chini ya 2m kwa siku anataka kutoa kodi ya laki 5 kwa miezi 3, hao jamaa si wa kuwachekea, ni wakwepaji kodi wakubwa.
Ingekua rahisi hivyo kila mtu angefanya biashara kkoo
 
Tz mfanyabiashara wa Kkoo anayeuza mzigo wa 5m kwa siku na faida si chini ya 2m kwa siku anataka kutoa kodi ya laki 5 kwa miezi 3, hao jamaa si wa kuwachekea, ni wakwepaji kodi wakubwa.
Uuze 5m faida upata 2m. Sasa kwanini nyinyi wengine hamfungui hizo biashara, au nyie hamtaki faida? Mabenki mengi tu yanatoa mikopo, msisingizie hamna mitaji, kakopeni benki, wekeni nyumba zenu dhamana, kaanzisheni biashara na nyie mpate faida jamani
 
Halafu VAT threshold kuwa 100mil. miaka zaidi ya 20 tangu ianzishwe ni ujinga, thamani ya pesa imeshaku, hata machinga muuza maji anafikisha hii kwa mwaka, ilitakiwa walau 1bil. Mtu ukiuza 120mil. Kwa mwaka unaingizwa VAT uanze kulipa CPA akupelekee return kila mwezi, yaani ukipata 10% profit ni wastani wa 1mil. Kwa mwezi, sas akwa hii pesa ukipe pango, kodi zote na bado umlioe CPA kweli?! Inawezekana hii?!
 
Wengi wao hawa hawajawahi hata kufanya biashara ya kuuza vitumbua ndio maana utaona wanapitisha kodi na sheria za kijinga.
 
Ni kweli nimeshuhudia, Kuna kitu wanakuambia tunakupa risiti ya njiani

Kodi hazilipwi
 
Kodi iwe rafiki. Sasa unalipa Kodi mpaka mtaji unayumba, hiyo ni biashara gani? Serikali ipunguze au kuondoa mlolongo wa kodi juu ya kodi kama wana nia ya kukusanya mapato.
Kodi za ajabu ajabu, halafu zinaishia kuwalipa wanasiasa tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…