Mgogoro wa Mashariki ya kati waonyesha China ni kinara wa kutoa masuluhisho kwa nchi za Afrika

Mgogoro wa Mashariki ya kati waonyesha China ni kinara wa kutoa masuluhisho kwa nchi za Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
VCG111652796555.jpg


Kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu Marekani na Israel zilipozusha mgogoro wa Mashariki ya kati kwa kuishambulia Iran, bei ya mafuta kwenye soko la dunia ilipanda kwa ghafla na kuleta changamoto kwa maisha ya watu wenye mapato ya chini katika nchi mbalimbali duniani. Kati ya nchi zote kubwa duniani, China ni moja ya nchi ambazo wananchi wake hawajaathiriwa sana na ongezeko la bei ya mafuta. Kwanza ni kutokana na serikali kuwa na uwezo mkubwa kifedha kutoa ruzuku, na pili ni kutokana na matumizi makubwa ya nishati mpya kwenye usafiri wa umma.



Kwa nchi za Afrika zenye uwezo mdogo wa kutoa ruzuku ya mafuta, ongezeko dogo la bei ya mafuta linasababisha mfumuko wa bei ambao huathiri moja kwa moja maisha ya watu wenye mapato ya chini. Kumekuwa na habari kuwa baadhi ya wakazi wa Dar es salaam na Nairobi wameanza kutembea kwa miguu kwenda kazini, baada ya nauli za matatu na daladala kupanda.



Hata hivyo tukiangalia kwa undani, changamoto hii ya maisha ya watu kutatizwa kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta, isingekuwa kubwa kama baadhi ya sera zingetekelezwa katika nchi mbalimbali za Afrika, kama tahadhari ya kuepuka madhara ya kupanda kwa bei ya mafuta.



Nchini Tanzania, mfano mzuri upo kwenye bajaji. Kati ya bajaji zinazotumika mjini Dar es salaam, kuna zinazotumia betri na gesi, ambazo wakati huu wa changamoto ya mafuta kwao ni neema. Kwani hawana sababu ya kupandisha nauli, hasa kutokana na mgogoro wa mashariki ya kati kutokuwa na athari yoyote kwenye nishati wanayotumia.



Usafiri wa bajaji si usafiri wenye kubeba abiria wengi, kama ilivyo kwa daladala na matatu. Kwa hiyo mchango wake kwenye kupunguza makali ya ongezeko la bei ya mafuta ni mdogo sana. Kwenye miji mikubwa ya Tanzania na Kenya, daladala na matatu ni usafiri muhimu kwa watu wote wanaojikita kwenye shughuli za uchumi, iwe ni kwenye sekta za huduma au uzalishaji, kama usafiri huo ungetumia nishati za gesi na umeme, basi mtikisiko kwenye uchumi wa nchi hizo usingekuwa mkubwa sana.



Uzuri ni kwamba mji wa Dar es salaam tayari una mfumo wa barabara za mabasi ya mwendo kasi. Kama mabasi hayo yangekuwa ni yenye mifumo ya kutumia betri au gesi, kusingekuwa na maumivu makubwa kutokana na ongezeko la bei ya mafuta.



Kama kuna utashi, kilichowezekana China bila shaka kinawezekana Afrika. Kwa sasa China ina teknolojia kamili za kutengeneza mabasi hayo, na tayari China ina ushirikiano na nchi mbalimbali za Afrika kwenye eneo hilo. Kinachotakiwa kufanyika ni utekelezaji wa haraka wa sera za matumizi ya nishati mbadala, ili kupunguza changamoto ya mfumo wa bei kutokana na mgogoro wa mashariki ya kati, na kujiandaa kwa changamoto yoyote inayoweza kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta katika siku za baadaye.
 
Viongozi wa Afrika wanapendelea kuagiza mabasi ya dizeli yaliyotumika (dala dala chakavu) ili kulinda maslahi binafsi ya wafanyabiashara wa mafuta.
 
Back
Top Bottom