Shushani Ngomeni
Member
- Nov 24, 2014
- 45
- 18
Wana Jamvi Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Tanzania
Nimerudi kwa mara nyingine kukumbusha Mamlaka juu ya Mgogoro wa shamba la Kwa Ugoro kijiji kilichopo Wilaya ya Meru Mkoani Arusha. Siandiki kwa faida yangu, wala sina cha kupata isipokuwa furaha ya nafsi hasa pale haki inapotendeka kwa watu wanyonge.
Kitendo cha kuwanyanganya wananchi mashamba yao yote waliyolima tangu taifa hili lipate uhuru, na kimsingi wao ndio waliyofyeka na kufukuza wanyama wakali kipindi hicho, kwakweli ni dhambi mbele za Mungu kwa walioshiriki Unyanganyi huo na ni Laana kwa Taifa letu. Serikali inatengaje Heka 500 kwaajili ya waanchi kati ya heka zaidi ya elfu 4000 ambayo wananchi walikuwa wakilima miaka yote? Inawezekanaje Watu wa Kijiji A kupewa ardhi ndani kijiji B wakati wao pia wana mashamba yao katika kijiji A? Tamaa za Kisiasa na kujipenda nafsi Itawasukuma wengi kaburini na kuacha hiyo ardhi.
Najua Rais hafaham jambo hili hata kidogo, na wasaidizi wake yaani Waziri na Naibu wake hawafaham kwa undani kwasababu hawajapata nafasi ya kujua Lakini Naamini jambo hili litakapofika mezani litafanyiwa kazi kwa haraka.
Kwasababu wale wananchi wamenyamazishwa kwa vitisho vya bunduki, magari ya polisi na hata kuwekwa Jela, Kwakweli Mungu wao Hajamaza, Malaika wa mbinguni hawajanyamaza. Haki yao itatetewa na Mungu mwenyewe, itadaiwa kwa watu walioshiriki unyama huo na kwa familia zao.
Ukihitaji ufafanuzi zaidi juu ya Mgogoro huu Search Barua ya wazi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi kuhusu mgogoro wa ardhi kata ya Maroroni wilayani Arumeru.