Mleta mada hana ushahidi ila wakati anakula 071 kwa mke wake ndo wazo tu likamjia.
Topic: Ruth H Mollel aliingia lini CHADEMA?
Wasalaam !
Kweli sasa nimeanza kuzeeka na kupitwa na matukio ya kisiasa na kijamii.
Nina swali la msingi kwa wadau makini hasa wana chadema asilia.
HIVI HUYU Ruth H Mollel ambaye kama sikosei(nitaomba kusahihishwa) alikuwa ni mtu mnene na msomi kwenye serikali kwa miongo kadhaa alihamia lini chadema?
Kwenye list ya wabunge wa viti maalum wa chadema nimeliona jina lake nikashtuka kidogo kwa maana ya kushangazwa.
Hivi mama huyu alianza harakati ndani ya chadema lini kiasi cha kuukwaa ubunge wa viti maalum?
Hivi Chadema ilikuwa inahubiri mabadiliko ya namna gani hasa kama kikundi chote cha waliokuwa madarakani wamehamia huko?
Kama ni yeye kweli ...kupata ubunge viti maalum kupitia chadema huku ukiwaacha vijana waliojaribu kuwekeza katika chadema kwa kukimbia mfumo wa kiccm inatoa picha gani?
Hebu wasemaji wa chadema asilia njooni mjadili hoja hii.
SAMAHANI:Kama huyu Ruth H Mollel sio yule aliyekuwa ofisi ya makamu wa Rais mazingira na CV zake lukuki.
OMBI:Mada ijikite katika mchakato wa kumpatia ubunge Ruth Mollel!
Kwa wale ambao ni kizazi cha bodi ya mikopo kaeni kando
Cc:
Pasco
Crashwise
Molemo
Mungi
Itafute hii thread iliokwisha anzishwa humu jf na ujibu hili swali