Mgogoro wa Ukraine na Urusi unapima akili za Waafrika

Mgogoro wa Ukraine na Urusi unapima akili za Waafrika

Huwezi kuelewa maana akili zako zipo ulaya
Africa haipo hapa ilipo kwa uzembe na uvivu wa Waafrika au ujinga wa viongozi wa Afrika TU, bali kwa woga wa waAfrika na viongozi wa Afrika. Viongozi wetu ni waoga, cowards na wabinafsi kama vile kundi kuuuuubwa la nyumbu linavyomkimbia fisi mmoja TU. Kama akitokea nyumbu mmoja aliyeamua kusimama kupambana na fisi nyumbu huyo atashindwa vibaya sana kwakuwa wakati nyumbu wote wanatimua mbio na kumuacha nyumbu mwenzao akipambana na fisi kundi la fisi wanamkimbilia fisi mwenzao kumsaidia amshinde nyumbu ili fisi wate wanufaike kwa kupata chakula cha nyumbu yule.

Waafrika na viongozi wa afrika ni wengi kama walivyo nyumbu lakini wanashindwa kuungana dhidi ya mkoloni/fisi mmoja kutetea bara lao na nchi zao. Hii inatoa mwanya kwa fisi/mkoloni kumla nyumbu mmoja baada ya mwingine hasa wale nyumbu wanaosimama dhidi ya fisi/mabeberu wanaosaidiana kuweka vikwazo, kunyimwa mikopo na hata kupigwa kwa mabomu wale nyumbu/waafrika wanaosimama kidete dhidi ya beberu mmoja au mabeberu wengi. Tumeona kwa Nkrumah, Nyerere, Mugabe, Gaddafi na wengine wengi wakishuhulikiwa hadi wanakwisha wakati nyumbu/viongozi wengine wa kinafika wakigongeana glasi za mvinyo na watesi wa Waafrika wenzao.
 
Back
Top Bottom