cassavaleaves
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 1,799
- 2,237
Sifa kubwa ya Wamarekani na West ni kukataa kuzikimbia nchi zao kuwakimbia watawala wabaya kwao, wanapambana na watawala kudai wanachokitaka wakiwa humohumo kwenye nchi hata ikiwalazimu kupoteza uhai wa baadhi yao kitu wanachokiita "stand for your right". Hii ni tofauti na vijana wetu kutoka Afrika, wao wanatafuta read made solutions kwa kuzisaliti nchi zao na kukimbilia ndizi na jibini kwenye nchi nyingine, na huu ndio udhaifu wa akili zetu wa kuangalia matumbo na njaa zetu za muda mfupi na kusahau kuwajengea mustakabali vizazi na vizazi vyao vijavyo kwenye taifa lao.
Kavulata, ngoja nikurahishie point zako ambazo unashindwa kuziweka vizuri.. unaposema " Hii ni tofauti na vijana wetu kutoka Africa, wao wanatafuta ready made solutions kwa kuzisaliti nchi zao...." Hivi unawatenga vipi vijana wa Kiafrica na viongozi wao, tena waliochaguliwa kwa maelfu ya kura, wanaowasaliti wananchi wao kwa ufisadi, mikataba mibovu, ubadhirifu nk! Ni nani hasa msaliti Kavulata! Mbona unakua kama mbuni uliyeingiza kichwa ndani ya udongo ukidhani huonekani!
Naomba ujiulize tena, ni nani hasa anayeisaliti nchi za Kiafrica kama sio hao viongozi wanaosaini mikataba ya kuja kuchimbiwa vyoo! Sijui uko katika msimamo upi katika swala la bandari Tanzania, Watanzania baadhi wanaona ni usaliti wa hali juu katika mkataba huo! Kama ni kweli miaka 100 kuweka bandari rehani inatisha! Nasema kama ni kweli! Ila kwako kijana aliyekuja Marekani kutafuta unafuu wa maisha yake na familia yake, kwako ndio msaliti wa Nchi.....Ufahamu wako unatisha!
Ninaweza kukupa mifano mingi, maana ya Tanzania unaijua sana, unajua ubadhirifu alioufanya Jacob Zuma, au ubadhirifu alioufanya Jose Santos kumwacha binti ya Milionea, au mwanamapinduzi wako Robert Mugabe ambaye kila kukicha unaona lindi la utajiri wake! Na list ndefu sana...! Hao ndio wasaliti! Wewe umekuwa kipofu na ubongo wako umekosa kufikiri kama umeshindwa kujua ni nani hasa msaliti Africa!
Mitazamo kama hiyo itafanya Africa isifike popote! Maana hujui kabisa kiini ya matatizo yetu na jinsi ya kuyatatua!