Kavulata,
Ume generalize mno jamaa yangu Kavulata! Kuna nchi nyingi za Kiafrica zimepata uhuru pasipo msaada wa Urusi. Kumbuka Nchi nyingi za Kiafrica zimepata Uhuru miaka ya 60, ( Cameron, Togo, Madagascar, The Democtric Republic of Congo,Somalia Benin Niger,Burikina Faso, Ivory Coast,Chad, The Central Africa Republic,Gabon, Senegal, Mali, Nigeria) January hadi Dec 1960 kulikuwa na nchi kama 17 hivi zilikuwa zimejipatia Uhuru bila msaada wa Urusi na kulikuwa na sababu nyingi hata za ndani za nchi hizo kuachilia Makoloni yao pia.
Mrusi Kaingia baadaye kabisa miaka ya 80, na unauona mkono wake kwa Mataifa ambayo hayakupata uhuru miaka 60 Kama Zimbabwe, Angola, Mozambique, Namibia na South Africa. Kwa Kifupi mchango wa Urusi ni kwa nchi chache sana, Huu ni ukweli wa Kihistoria. Na hata Mrusi kuingia Zimbabwe na Angola ni baadhi ya Wananchi wa Nchi hizo kugawanyika wao wenyewe wafuate mfumo gani. In short influence ya Urusi inaanza miaka ya 80.
Na unaposema " Wazungu wanajua rafiki mkubwa wa Africa ni Urusi na China kuliko watu wa Ulaya Magharibi na Marekani" Sielewi una Maana gani, labda ungefafanua....maana nchi kama China interest yake kubwa kwa Africa imeanza miaka ya 90, ukiondoa nchi kama Tanzania kujengewa reli ya Tazara (1970) labda Ghana kipindi cha Nkurumah... Hivyo ni Wazungu wa wapi Hasa unaowazungumza?
Labda iweke sawa mada yako, kuna propaganda nyingi mno kila upande, lakini mojawapo ya propaganda inayoazagaa kwa baadhi ya Waafrica kuwa China na Urusi ni rafiki wa kweli wa Africa, bila kujua naye pia anataitafuta Africa kwa maslahi yao.