cassavaleaves
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 1,799
- 2,237
Wazungu Wana viwanda vikubwa sana vya silaha vinavyolipa Kodi na mishahara kwa wafanyakazi wake. Moja ya kazi ya viwanda hivyo ni kutafuta masoko ya bidhaa zao kama ilivyo kwa biashara zote nyingine. Soko la silaha ni watu wanaopigana full stop!!. Vita hivi vya wenyewe kwa wenyewe vinachochewa na nchi zenye viwanda vya silaha.
Silaha zinaingizwa kwa njia mbalimbali kama vile zana za uchimbaji madini, ndege za kubeba maua na samaki, misaada kwenye majanga kama matetemo, njaa na mafuriko, utalii na vifaa vya ujenzi.
Kavulata:
Umenifungua macho kuhusu Mwafrica..... " Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinachochewa na nchi zenye viwanda vya silaha" Sasa huyu mwafrica yeye ni zezeta kukubali kuchochewa na mzungu! Miaka 60 toka ajipatie uhuru wake ameshindwa kabisa kujitambua na kuwa na fikra zake....! Kushindwa kutatua matatizo yake ya ndani na kuruhusu mtu toka nje kuja na kuzidi kuwagonganisha vichwa!
" Silaha zinaingizwa kwa njia mbali mbali " Kweli akili ya Mwafica ina matatizo! Ina maana nchi za Kiafrica hazina Immigration unit (Idara za Uhamiaji) Hazina watu wa Customs! Miaka mingi toka tujipatie Uhuru tunashindwa kulinda mipaka yetu! Ni nani wa kumlaumu hasa! Maana hata kuendesha bandari tu inaonekana shida hapa kwetu Tanzania! Yaani kupokea mizigo na kusafirisha tunahitaji usaidizi! Kweli tutafika! Ni nani wa kumlaumu!
Asante kwa kunifungua macho kuhusu akili ya Mwafrica, uko sawa kabisa, na Mzungu hata kututupia ndizi kama ulivyosema ametuhurumia sana! Maana kisha jua akili zetu!