Mkuu, hayo 👆👆 unayasema ww. Dunia nzima isipokuwa ww na wale wa aina yako tunafahamu chanzo cha Mgogoro wa Ukraine na Urusi na lengo la kila mhusika. Ukraine analengo la kukomboa Ardhi iliyokwapuliwa kimabavu/kibabe na Urusi lakini Urusi ana lengo la kumwadabisha Ukraine ili asimkaribishe au asijiunge na NATO kitu ambacho kwa mtizamo wa Urusi, kitahatarisha Usalama wa taifa la Urusi.Huna insight, unadhani haikuhusu, na hiyo ndio akili ya waafrika wengi. Wanaendeshwa na matukio mpaka liwafike. Uwezo wetu wa kufikiria critically ni mdogo sana. Mzungu anasafirisha mchanga hadi Ulaya lakini watu hawashituki. Neo mangungolism.
Sasa wewe hilo la eti ni kupima akili za Waafrika umelipata wapi?? Je, unaweza kutoa supporting evidence ya madai yako au ni umekaa na ukawaza tu halafu ukaja hapa chap na kupandisha uzi wako huu ukidhani ndo umewaza critically?
Hao wenye mgogoro baina yao(Ukraine vs Urusi) kila mmoja anawania ashinde (am-outweigh) mpinzani wake. Hawana time na madai yako ww bro.
Ndio nakubaliana na wewe kwamba huo mgogoro(vita) itatuhusu Waafrika kwa namna moja au nyingine lakini sio kwamba eti itakuwa ndo mtihani wa kutupima akili zetu.
Kumbuka msemo wa wahenga "wapiganapo fahali wawili nyasi huumia" nikimaanisha kwamba madume hayo yanapopigana lengo lao sio kuzivuruga, kuziharibu na kuziumiza nyasi. kuumia kwa nyasi ni "side effects" au ni "yatokanayo"
Labda nikuulize hvi; Hiyo vita ina athari gani za moja kwa moja (direct) kwako wewe?