Inashangaza kwamba emphasis kubwa inaekwa kwa mambo ya uchaguzi, as if vurugumechi za uchaguzi zikiishaga na vumbi kutulia matatizo ya mTz mlalahoi yatakuwa yametatulika. Inashangaza.
Pia inashangaza kwamba emphasis kubwa inaekwa kwa sula la mgombea binafsi, as if ni muarobaini flani hivi..Sielewi kwa nini tuhangaishwa na sheria ambazo zimekaa kia-academic zaidi badala ya matatizo halisi ya mTz wa kawaida ambayo yanafahamika. Sarakasi zinachezwa mahakamani, muda na fedha za walipa kodi zinateketezwa huko, makongamano yatafanyika, magazeti yataandika, tovuti zitaandika, bandwidth zitatumika na akili zitakuwa occupied na vitu ambavyo ni wazi havina impact yeyote ya maana.
Pia inashangaza mtu anasema kwamba eti hata Nyerere aliridhia hili suala. Nyerere anachukuliwa kama ndiye shareholder wa inchi hii as if the rest of us hatuna opinion au we don't matter, hii inatia kichefuchefu.
Nways, my 2 cents ni kuwa as long as tunaendelea kuukumbatia mfumo wa sasa kujiongoza kwa kupitia siasa, we are bound to fail, na hijalishi vizazi vingapi vitapita lakini we will continue to be POOR and MISERABLE. Trust me or not, thats a guaranteed fact.