Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini?

Jaji Bomani alisema woga na hoja zinazotolewa na wapinzani kuhusu nafasi ya mgombea binafsi hazina msingi.

Ingawa Jaji Bomani hakuitaja serikali, kauli hiyo inaonyesha kuwa anayoizungumzia hapa ni serikali kwa kuwa ndiyo inayoendelea kuipinga hoja hiyo hata baada ya mahakama kuruhusu.

Kweli ni wazi kuwa Serikali ya JK ndio waoga anaowaongelea Jaji Bomani.

Lakini je, ni upi mzimamo wa Upinzani juu ya wagombea binafsi au Mtikila peke yake tu ndie anayetaka wagombea binafsi kwa upande wa upinzani?
 
- Wagombea binafsi sio solution ya matatizo yetu ya uongozi mbovu Tanzania, lakini tunaheshimu msimamo wa Bomani symbolically wa kuweza kusimama inapotakiwa yaani at the right time, Upinzani lazima wawe waangalifu sana na hii ishu kwa sababu wanaweza kuwa the victims au the winners wa huu uamuzi depending unatizama kwa angle gani ya siasa yetu ya Tanzania, ambayo huwa ni tofauti na zingine za dunia nzima..

- Symbolically wagombea binafsi ni kitendo kinachosimamia more freedom kwa wananchi, other than that one must be careful on how inaweza kuwa effective wka wananchi walalhoi wa Tanzania.

Respect.

FMEs!
 
Suala la mgombea binafsi ni suala la haki za msingi kwa wahusika (i.e. wananchi) na katika demokrasia ya kweli..........kwa nini uzime sauti za watu wasiopenda vyama vya Kijambazi..........Ukiritimba wa vyama vya siasa vilivyopo bado unatupeleka shimoni.

kwa nini unawang'ang'aniza watu watumie huo UKIRITIMBA wa KIJAMBAZI kuamua fate ya maisha halafu mijitu kama kina Chenge et al ipo ipo tu ikituona sisi wananchi ni wajinga only wavivu/waoga wa kufikiri tu ndio wanaoona kuwa suala la mgombea binafsi halina manufaa.
 
Kimsingi nakubaliana na Mzee Bomani. Naomba wanaJF mnisaidie. Siku chache zilizopita AG Werema alidai kuwa ile hukumu ya High Court is not binding kwa sababu wamekata rufaa. Nataka kujua kikanuni na kisheria yafuatayo:

1. Iweje mbunge aliyeshinda uchaguzi ushindi wake unapokuwa challenged mahakamani kwa njia ya petition, yule mbunge bado anatambuliwa kisheria hadi ushindi wake utenguliwe na mahakama baada ya petition? Halafu hukumu ya kuruhusu mgombea binafsi baada ya mashtaka na Mtikila yasiwe binding? Je kikanuni na kisheria is this not contradictory?

2.Iweje Babu Seya na wengineo ambao wamehukumiwa hukumu zao zinakubalika mpaka rufaa ije itengue na hii ya kuruhusu mgombea binafsi baada ya mashtaka na Mtikila yasiwe binding? Je kikanuni na kisheria is this not contradictory?

3. Kati ya Jaji Bomani Attorney General mstaafu na AG Werema yuko sahihi mbele ya sheria? Je mgongano huu wa uelewa ndiyo ishara ya viwango vya elimu ya wataalamu wetu wa siku hizi kuwa wamefulia ukilinganisha na wale waliosoma enzi hizo za Malkia Elizabeth?
 
Sahihisho hiyo ya 3 isomeke Kati ya Jaji Bomani Attorney General mstaafu na AG Werema nani yuko sahihi mbele ya sheria? Je mgongano huu wa uelewa ndiyo ishara ya viwango vya elimu ya wataalamu wetu wa siku hizi kuwa wamefulia ukilinganisha na wale waliosoma enzi hizo za Malkia Elizabeth?
progress.gif
 
Inashangaza kwamba emphasis kubwa inaekwa kwa mambo ya uchaguzi, as if vurugumechi za uchaguzi zikiishaga na vumbi kutulia matatizo ya mTz mlalahoi yatakuwa yametatulika. Inashangaza.

Pia inashangaza kwamba emphasis kubwa inaekwa kwa sula la mgombea binafsi, as if ni muarobaini flani hivi..Sielewi kwa nini tuhangaishwa na sheria ambazo zimekaa kia-academic zaidi badala ya matatizo halisi ya mTz wa kawaida ambayo yanafahamika. Sarakasi zinachezwa mahakamani, muda na fedha za walipa kodi zinateketezwa huko, makongamano yatafanyika, magazeti yataandika, tovuti zitaandika, bandwidth zitatumika na akili zitakuwa occupied na vitu ambavyo ni wazi havina impact yeyote ya maana.

Pia inashangaza mtu anasema kwamba eti hata Nyerere aliridhia hili suala. Nyerere anachukuliwa kama ndiye shareholder wa inchi hii as if the rest of us hatuna opinion au we don't matter, hii inatia kichefuchefu.

Nways, my 2 cents ni kuwa as long as tunaendelea kuukumbatia mfumo wa sasa kujiongoza kwa kupitia siasa, we are bound to fail, na hijalishi vizazi vingapi vitapita lakini we will continue to be POOR and MISERABLE. Trust me or not, thats a guaranteed fact.
 
Abdulhalim,
Hizo 2 cents zako zinashabihiana na yale yote mwenyewe unayopinga hapo juu. Mfumo wa sasa usioupenda ni upi na unaweza kubadilishwa vipi iwapo hili la mgombea binafsi (moja ya maswala ya mifumo ya uchaguzi) unalipinga na kusema lisiwe moja ya jambo la kuwekewa msisitizo??
 
Field Marshall ES,
Katika nchi iliyojaa uchama katika ngazi zote, na katika nchi ambayo mihimili na taasisi zote za Taifa ububu umezingira, hakika Jaji Bomani kaonesha ukomavu wa hali ya juu sana katika kusimamia haki, kupitia elimu yake, utu wake, uongozi wake, na mapenzi yake kwa nchi. This is truly symbolic, I just wish it is emulated by many of our leaders!!
 
Haya mambo ya CCM na Chadema yanatufunga wengine tutashindwa kujitokeza muda ukifika.Fanyeni hima wakulu mtuletee mgombea binafsi na sisi tusiofungamana na itikadi zenu tupate nafasi ya kuwakilisha matatizo ya wananchi na kuisimamia mguu sawa hii kitu serikali.
 
Hizo 2 cents zako zinashabihiana na yale yote mwenyewe unayopinga hapo juu. Mfumo wa sasa usioupenda ni upi na unaweza kubadilishwa vipi iwapo hili la mgombea binafsi (moja ya maswala ya mifumo ya uchaguzi) unalipinga na kusema lisiwe moja ya jambo la kuwekewa msisitizo??

Sio tu kuekewa msisitizo bali siasa ktk nchi yetu HAIHITAJIKI PERIOD!. Kama tungekuwa wakulima siasa ni kama panya walioeka makazi yao ktk gunia letu tulizohifadhi mbegu. Wanakula hizo mbegu, na wanafanya choo humhumo! Tatizo letu ni kuwa wengi wetu hatulioni hili na hili linanisikitisha zaidi.

I don't mean to sound crazy, but unaeza kutembelea kuona glimpse ya model ninayoi-propose (post #15)kutokana na uzoefu wangu wa miongo 4+ juu ya uso wa dunia. Ninayo hakika kua tukifuata mfumo kama huo, kabla ya wengi wetu hatujarudisha namba mabadiliko yataonekana kila mahali. Trust me. Ila kadr tunavochelewa ku-act ndio situation inavyozidi na itakavyozidi kuwa mbaya-Deterioration to static.
 
Muathirika mkuu wa wagombea binafsi atakuwa CCM. Kwani wanajua kuwa kwa kufanya hivyo watashindwa kuwadhibiti wabunge wenye msimamo wa kutetea wananchi badala ya chama. Kwa maana hiyo basi mgombea binafsi atafanya wabunge kuwa answerable to his/her constituent more than the party.

Utaratibu wa sasa ukifukuzwa katika chama unakosa na ubunge ndiyo unaowafanya wabunge wa CCM kuwa makondoo kwa kina makamba, ila kama mgombea binafsi ataruhusiwa basi hata kama mtu akijitoa kwenye chama bado ataendelea kuwa mbunge mpaka uchaguzi mkuu ujao, kwani waliomchagua kuwa mbunge si wanachama wa chama chake bali ni wananchi katika jimbo lake. Hili ndilo linalowaogopesha sana Viongozi wakuu wa CCM,
 
Hofstede,
- Mkuu Hofstede, heshima sana ni vyema tukawa waangalifu sana na tunayoyalilia kwanza tumelilia vyama vingi CCM wakaishia kutupiga bao, sasa tunalilia wagombea binafsi, mimi siamini hata kidogo kwamba inaweza kuwatikisa CCM kwa sababu the minute wakishindwa kuizuia, wataikubali halafu watatuchezea na the Mrema and Marando likes.

- Hakauna taifa lolote duniani linaloongozwa na mgobea binafsi, na wala hakuna taifa lenye wabunge wengi ambao ni independent, na wala hawajawahi kwua effective katika kubadilisha muelekeo wa siasa za taifa hasa kiuongozi, wasi wasi wangu ni kwamba hii ikipita bila some serious Federal regulations ku-control it, tutaishia hawa hawa matajiri wa CCM,

it about time sasa wale wanaolilia hii hoja watupe elimu nzito kuliko tuliyonayo on this ishu, yaani how Tanzania na hasa wananchi walalahoi tutafadika na wagombea binafsi, ingawa ninasema kwamba kuwa nayo symbolically ni bora zaidi kuliko kutokwua nayo! Na kwa sababu inawakera sana CCM, basi ni vyema kulilia tu mpaka wakubali!

Respect.


FMEs!
 
Muathirika mkuu wa wagombea binafsi atakuwa CCM. Kwani wanajua kuwa kwa kufanya hivyo watashindwa kuwadhibiti wabunge wenye msimamo wa kutetea wananchi badala ya chama.

Naomba unitajie Mbunge mmoja tu ndani ya CCM mwenye msimamo wa kuwatetea wapiga kura wake au watz kwa ujumla,stena itaki utaje wawili au watatu,nitajie mmoja tu nimjue!

Naomba nitajie Mbunge mmoja tu wa CCM ambaye hajaweka maslahi yake binafsi mbele eti akatanguliza mbele zaidi maslahi ya waliompeleka Bungeni!

Hofstede,kama utanitajia Mbunge huyo na jinsi alivyopigania misimamo yake iwanufaishe watz mm nipo tayari kukubali kuwajibishwa!
 
- Mkuu kwani ni wapi sheria zetu zinasema ni lazima mbunge kutanguliza masilahi ya wananchi wa jimbo lake kwanza?

Respect.

FMEs!

Kazi za Bunge ni

(1)Kutunga sheria

(2)Kuangalia sheria walizozitunga au tamko walilotoa zinafuatwa na serikali

(3)Kuisimamia serikali kuhusu ugawaji wa"keki ya Taifa"ili kupeleka maendeleo majimboni kwa haki na usawa

Hii hufanywa wakati wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha ikisomwa na Waziri wa Fedha na baadae Mawaziri na wizara zao wakionyesha pesa walizotengewa na zitagawiwa vipi Majimboni;kwa mfano waziri wa zamani wa Miundo Mbinu Basil Mramba kwenye bajeti yake ya mwaka 2006 alipeleka sehemu kubwa ya bajeti ya wizara yake kutengeneza barabara za jimbo lake la Rombo

Nae waziri wa Maji wa kipindi hicho hicho Steve Wasira nae akamega bajeti nono ya wizara yake na kuipeleka kwenye jimbo lake la Bunda

Hili jambo la 3 ndiyo linalompa nafasi Mbunge ama kushinda tena au kuangushwa kwenye uchaguzi unaofuata maana wapiga kura wake watamuuliza kwa miaka 5 ulilifanyia nini jimbo lako?Mbunge anatakiwa awe mstari wa mbele kuikumbusha serikali kwenye bajeti kuhusu matatizo ya jimbo lake

Kama Mbunge hatangulizi maslahi ya wapiga kura wake mbele hasa kuiomba serikali kulipa jimbo lake fungu la bajeti kwenye sekta za maendeleo kama vile barabara au malambo ya mifugo au madawa anakuwa hafanyi kazi yake vyema waliyomtuma wapiga kura wake!

Mbunge kusimamia maendeleo ya wapiga kura wake ni jambo lililo ndani ya katiba na wala hatuombi wafanye hivyo!Ila ni vigumu kuona haki hii inaendeka ndani ya Bunge la CCM maana lipo Dodoma kama rub stamp ya serikali tu na kuwajibika zaidi kwa Jk na wala sio wananchi waliompa kura!

Nchi zenye Wabunge wa ukweli kama vile USA na UKwanajua kabisa kuwa usipowasikiliza wapiga kura wako basi haushindi uchaguzi unaofuata,kwa sababu Wabunge wa nchi hizo wapo kwa ajili ya watu waliowapa kura na wala sio kama hawa wa kwetu
 
Haya mambo ya CCM na Chadema yanatufunga wengine tutashindwa kujitokeza muda ukifika.Fanyeni hima wakulu mtuletee mgombea binafsi na sisi tusiofungamana na itikadi zenu tupate nafasi ya kuwakilisha matatizo ya wananchi na kuisimamia mguu sawa hii kitu serikali.
Ile kazi uliyokuwa unatafuta uwt ulifanikiwa?
 
9th March 10
Hellen Mwango


Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustine Ramadhan, amewaandikia barua maprofesa wawili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akiwaomba wawe marafiki wa mahakama katika usikilizwaji wa rufaa ya mgombea binafsi itakayosikilizwa na Mahakama ya Rufaa Aprili 8, mwaka huu.

Maprofesa hao, ambao ni wanasheria kitaaluma na wahadhiri waandamizi, ni Jwan Mwaikusa na Palamagamba Kabudi, ambaye ni Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha UDSM.

Katika barua yake ya Machi 3, mwaka huu, Jaji Mkuu amewaomba maprofesa hao kuwa marafiki wa mahakama na wajielekeze katika hoja zao kama mahakama inaweza kutamka kifungu gani cha katiba kinakwenda kinyume cha Katiba.

Aidha, Aprili 8, mwaka huu, Profesa Mwaikusa na Kabudi watachangia hoja kuhusu shauri hilo, litakaposikilizwa na Mahakama ya Rufani, mbele ya jopo la majaji saba linaloongozwa na Jaji Mkuu.

Mahakama hiyo inatarajia kusikiliza rufaa ya serikali dhidi ya uamuzi uliotolewa na waliokuwa majaji wa Mahakama Kuu; aliyekuwa Jaji Kiongozi, Amir Manento, Salum Massati (sasa Jaji wa Mahakama ya Rufaa) na Thomas Mihayo (Mstaafu).

Majaji hao katika hukumu yao, walikubaliana na hoja zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Democrat (DP), Mchungaji Christopher Mtikila za kuwapo mgombea binafsi katika uchaguzi wa siasa nchini.

Jopo la majaji saba wa Mahakama ya Rufaa, wakiongozwa na Jaji Mkuu, linawajumuisha Jaji Eusebia Munuo, Januari Msofe, Nathalia Kimaro, Mbarouk Salim, Dk. Stephen Bwana na Benard Ruanda, watasikiliza rufaa hiyo.

Katika rufaa yake namba 45 ya mwaka jana, serikali imetoa sababu sita za kukata rufaa hiyo zikiwemo, Mahakama Kuu ilikosea kujipa mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo; ilikosea kutengua vifungu vya Katiba ya nchi; na ilikosea kisheria kwa kupunguza matakwa ya lazima ya Ibara 30 (5) na 13 (2) ya Katiba ya nchi.

Sababu nyingine ni kujipachika mamlaka ya kibunge ya kutunga sheria; kukosea kisheria kwa kuiweka Katiba ya nchi katika vyombo vya kimataifa; na pia ilikosea kuitolea maamuzi kesi hiyo bila kuweka suala hilo bayana.

Mara ya kwanza serikali ilikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu, katika Mahakama ya Rufaa mwaka 2007, ambapo ilidai mahakama hiyo ya chini ilikosea kisheria kutafsiri Ibara ya 21(1) (c), 39 (1) (c) (b) na 69 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Hata hivyo, rufaa hiyo ilitupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa baada ya kukubaliana na ombi la wakili wa Mtikila, Richard Rweyongeza, kwamba rufaa hiyo haina msingi na kwamba imejaa dosari za kisheria.

Awali, katika hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa Mei 2006, iliruhusu kuwapo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi, kwa sababu Katiba ya nchi inatoa haki hiyo.

Mahakama Kuu ilibainisha kuwa katiba inatamka wazi kuwa, kila mwananchi ana haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi na haiweki masharti kuwa hilo lifanyike kwa mtu kujiunga na chama fulani.

Hii ilikuwa mara ya pili kwa Mtikila kupigania mgombe binafsi mahakamani, mwaka 1993 alishinda kesi kama hiyo katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, lakini licha ya uamuzi huo wa mahakama, Bunge lilishindwa kutunga sheria ya kuruhusu mgombea binafsi, hivyo alifungua kesi hiyo ya Kikatiba Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam ambako alishinda tena.

Rufaa hiyo ya serikali ilitajwa Februari 8 na iliahirishwa hadi Aprili 8, mwaka huu, kwa ajili ya kusikilizwa.



Chanzo: NIPASHEhttp://www.ippmedia.com/frontend/functions/print_article.php?l=14288
 
kazi ipo mwaka huu.hivi kuna ugumu gani kuruhusu wagombea bionafsi au serikali inaogop anini juu ya suala la mgombea binafsi?
 
Back
Top Bottom