Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jaji Bomani alisema woga na hoja zinazotolewa na wapinzani kuhusu nafasi ya mgombea binafsi hazina msingi.
Ingawa Jaji Bomani hakuitaja serikali, kauli hiyo inaonyesha kuwa anayoizungumzia hapa ni serikali kwa kuwa ndiyo inayoendelea kuipinga hoja hiyo hata baada ya mahakama kuruhusu.
Hizo 2 cents zako zinashabihiana na yale yote mwenyewe unayopinga hapo juu. Mfumo wa sasa usioupenda ni upi na unaweza kubadilishwa vipi iwapo hili la mgombea binafsi (moja ya maswala ya mifumo ya uchaguzi) unalipinga na kusema lisiwe moja ya jambo la kuwekewa msisitizo??
Muathirika mkuu wa wagombea binafsi atakuwa CCM. Kwani wanajua kuwa kwa kufanya hivyo watashindwa kuwadhibiti wabunge wenye msimamo wa kutetea wananchi badala ya chama.
- Mkuu kwani ni wapi sheria zetu zinasema ni lazima mbunge kutanguliza masilahi ya wananchi wa jimbo lake kwanza?
Respect.
FMEs!
Ile kazi uliyokuwa unatafuta uwt ulifanikiwa?Haya mambo ya CCM na Chadema yanatufunga wengine tutashindwa kujitokeza muda ukifika.Fanyeni hima wakulu mtuletee mgombea binafsi na sisi tusiofungamana na itikadi zenu tupate nafasi ya kuwakilisha matatizo ya wananchi na kuisimamia mguu sawa hii kitu serikali.